Sasa ni wakati wanaCCM tujitafakari na kuchukua hatua. Je, chama chetu ni mali ya wakulima na wafanyakazi? Au ni mali ya wajanja wachache?

Sasa ni wakati wanaCCM tujitafakari na kuchukua hatua. Je, chama chetu ni mali ya wakulima na wafanyakazi? Au ni mali ya wajanja wachache?

Na ndio maana chadema wanalilia katiba mpya, ili kutenganisha chama na dola.
Sawa, inaweza kusaidia ila ikivunjwa na watu wasiandamane nani atahakikisha wanapata haki iwapo hawana plan ya kuwa na ushawishi kwenye dola? Plan sahihi ni kujitengenezea ushawishi kwenye dola ili kutengeneza mazingira ya kulazimisha dola kuwa neutral.
 
Ccm Ya Matajiri
Hii ccm mtu masikini ukiwa na akili utapata kipato. Matajiri kwa asilimia kubwa watatumia pesa nchini, katika matumizi yao ukiwa na akili pesa zitakufikia. Watu waache kukaa tu na kulalamika badala yake waumize vichwa wananufaika vipi na mabadiliko ya mfumo.
 
Hicho chama kilishazeeka kinachofanyika sasa nikujaribu kukilisha lisha chakula lishe ambacho ni madaraka ya mwenyekiti ila bado haiwezi kusaidia kwasababu bado hawajui lishe inayohitajika niya aina gani.Kinachosikitisha nikuona bado kuna watu wanakiamini nakutegemea jambo jipya wakati kila kitu kiko wazi.Poleni sana.
 
Wakulima na wafanyakazi tulibahatika kukomboa chama chetu lakini kwa sababu sisi sio wajanja tumewarudishia.

Pombe Magufuli kumpa umakamu yule Mama asiyemfahamu lilikuwa ni kosa kubwa la kizezeta.

Tunapaswa kukuza wakulima na wafanyakazi wajanja.
Huyo hawala wa "kuchekacheka" nilikuwa sijuhi kwanini wanamuita Delilah sasa nimeelewa!
 
Mkuu 'Idugunde',
Samahani sana, watu kama wew, huko ndani ya chama kama bado mpo, tukiwahesabu hamfiki hata kumi. Sana sana tutawaona labda watu, tena wazeezee, kama Warioba, na nani tena, sijui!

Hicho chama siku nyingi sana kimekuwa ni chama cha maslahi, chama cha ,"huyu ni mwenzetu".

Kama unadhani Magufuli, labda, kuwa alikuwa na nia ya kukiongoza chama hicho kukirudisha kwenye misingi yake, basi njia/mbinu zake hazikuwa sahihi. Matokeo yake sasa, ndiyo haya. Wamerudi jamaa na njaa zao kali sana, kwa KASI MPYA..., na nini tena? "ARI MPYA"

Sasa sijui watu kama wewe mtaanzia wapi tena kuyasema hayo ya "CHAMA CHA WAKULIMA NA WAFANYA KAZI"!

Inabidi tu, tuwape pole yenu, huku nasi huku 'ukulimani' tukiendelea kukumbuka na kusononeka juu ya chama chetu kilichoporwa.

Sana sana tunachoendelea kuambulia siku hizi ni hayo mashati na kanga za njano na kijani. Hizo ndizo kifuta jasho chetu.
Kwa kweli wewe ni Kalamu 1 umenielimisha sana ndugu yangu,hawa jamaa tuwape pole kwa siasa za majitaka ambazo badala ya kufikiria maendeleo ya nchi na wananchi wake wanafikiria tu kushinda uchaguzi ama kwa njia halali au haramu ilimradi tu waendelee kutawala kwa kisingizio kuwa ccm inapendwa.Too late.
 
Bila hata ya kutumia hadubini sasa ndio wakati wa kuchambua pumba na mchele.

Chama chetu kilianza na madhumuni mazuri kabisa ya kuwa chama cha kuwatumikia watanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi.

Ndio ilikuwa dhima kuu kuleta maendeleo kwa manufaa ya kila mtanzania.

Hakikuwa mali ya wajanja wachache huko nyuma ambao wao ni kushibisha matumbo yao.

Sasa tutafakari na kufanya tathimini juu ya CcM ya leo. Ambayo ni mali ya familia ya wajanja wachache.
Wewe tulikuonya sana lakini Kibri kikakujaa , na bado
 
Magufuli hana balls zozote ni ubabe tu. Amekiri wazi choice yake ya umakamu alikuwa Ni Hussein mwinyi, lakini chama kikataka mwanamke. Kama angekuwa na balls angekomaa.
Hakuwa na balls ?

Halafu mbabe ?

Unakuwaje mbabe na huna balls ??????

Pombe Magufuli had brass balls. Mtu ambae haogopi kufa lazima awe na balls. Alisema nimejitoa maisha yangu kwa ajili ya Tanzania, akaanza kupambana na CCM corrupt establishment, akafunga biasharaza zao za kupiga hela za NHC, NSSF, TPA, TANAPA, BOT, ulanguzi, madawa, pembe za ndovu, ujambazi wa polisi.

Hakukuwa na mtu mwenye bigger ndani ya Afrika, hakuwepo wa kumlazimisha kumpa yule mama umakamu mara ya pili, it was his own epic blunder. The peasants and the downtrodden of this nation are paying a hefty price.

Unampaje umakamu wa Rais mtu humjui ?????
 
Pendekezo au shinikizo la chama lilikuwepo wakati wa uchaguzi wa kwanza, Pombe akiwa hana nguvu ya kukataa lolote.

Muhula wa pili Pombe Magufuli alikuwa on top of the world. Vingunge vyote vya chama alishavizima, Kinana, Makamba, Membe, Nape, aliwatilisha adabu. Mwinyi alishapoteza umakini wa akili, Mkapa alishakufa.

Kikwete naye alishapigwa pini. Taarifa zinasema Pombe alimwita IGP aje kumbeba Salma aliyekuja Ikulu kufoka na kulazimisha makontena yake yapite bila kodi, IGP akampigia simu Kikwete, ambae alijibu kama anataka kumkamata mwache amkamate. IGP akampikia Mkapa ambae ndie aliyezima sakata.

Kama Pombe Magufuli alikuwa na balls za kusimama wima mbele ya Kikwete ni nani kwenye chama angemlazimisha kumchukua huyu Mama Samia kuwa makamu safari ya pili ????

Wakulima na Wafanyakazi tulipewa chama, lakini tulivyo mazezeta tukawarudishia, tukampa umakamu Mama tusiyemjua. Again, tunataka wakulima na wafanyakazi wajanja.
Kama haya ni ya kweli, yeye mwenyewe alikosea kutombadilisha makamu wake maana uwezo alikuwa nao.
 
Ccm Ya Matajiri
Utajiri sio dhambi na wala sio kikwazo cha kutokuwa kiongozi bora.

Tatizo ni wale waliotajirika kwa kuwa wezi, mafisadi na wapiga dili haramu wengine.
 
Utajiri sio dhambi na wala sio kikwazo cha kutokuwa kiongozi bora.

Tatizo ni wale waliotajirika kwa kuwa wezi, mafisadi na wapiga dili haramu wengine.
Majizi Yapo Ndugu Zangu
 
Kikwete naye alishapigwa pini. Taarifa zinasema Pombe alimwita IGP aje kumbeba Salma aliyekuja Ikulu kufoka na kulazimisha makontena yake yapite bila kodi, IGP akampigia simu Kikwete, ambae alijibu kama anataka kumkamata mwache amkamate. IGP akampikia Mkapa ambae ndie aliyezima sakata.
Hili siamini kabisa , kama ni kweli hili lilitokea mbona JPM alimpa Salma ubunge ?
 
Kama haya ni ya kweli, yeye mwenyewe alikosea kutombadilisha makamu wake maana uwezo alikuwa nao.
Ni kweli kabisa, uwezo alikuwa nao muhula wa pili, angeweza kumtupilia mbali Samia ambae alikuwa chaguo la CCM establishment for their own self-serving motives.

Sasa Mama anatembea anatukana utawala wa Pombe Magufuli, anarudisha wakina Mchechu, Mafuru na Kinana kwenye sehemu nyeti ili wapige hela za kampeni za CCM na zingine wakwapue wampelekee Ikuku na pia purpose nyingine ni ku safeguard ajira za watoto wao walioko kwenye pipeline za ku graduate Malaysia, Marekani, UK, UD, UDOM etc. etc. etc….

Wakulima na wafanyakazi tujilaumu wenyewe kwa kurudisha madaraka kwa maharamia na ma mafioso waliopo kwa kujinufaisha wao na familia zao.

Unampaje madaraka ya vice president mtu humjui, baadae anakuja kukutukana majukwani ukishakufa !
 
Ni kweli kabisa, uwezo alikuwa nao muhula wa pil, angeweza kumtupilia mbali Samia ambae alikuwa chaguo la CCM establishment for their own self-serving motives.

Sasa Mama anatembea anatukana utawala wa Pombe Magufuli, anarudisha wakina Mchechu, Mafuru na Kinana kwenye sehemu nyeti ili wapige hela kupeleka kwenye kampeni na mifukoni mwao na kulinda future za watoto wao.

Wakulima na wafanyakazi tujilaumu wenyewe kwa kurudisha madaraka kwa maharamia wabinafsi.

Unampaje madaraka ya vice president mtu humjui, baadae anakuja kukutukana majukwani ukishakufa !
... anyway...ni funzo nzuri kwa kizazi cha viongozi wajao.
 
Sukuma geng acheni propaganda za hovyo hovyo. Kubalini kushindwa. CCM ina wenyewe.
 
Ni kweli kabisa, uwezo alikuwa nao muhula wa pili, angeweza kumtupilia mbali Samia ambae alikuwa chaguo la CCM establishment for their own self-serving motives.

Sasa Mama anatembea anatukana utawala wa Pombe Magufuli, anarudisha wakina Mchechu, Mafuru na Kinana kwenye sehemu nyeti ili wapige hela za kampeni za CCM na zingine wakwapue wampelekee Ikuku na pia purpose nyingine ni ku safeguard ajira za watoto wao walioko kwenye pipeline za ku graduate Malaysia, Marekani, UK, UD, UDOM etc. etc. etc….

Wakulima na wafanyakazi tujilaumu wenyewe kwa kurudisha madaraka kwa maharamia na ma mafioso waliopo kwa kujinufaisha wao na familia zao.

Unampaje madaraka ya vice president mtu humjui, baadae anakuja kukutukana majukwani ukishakufa !
CCM NI ILEILE ACHA CHADEMA WAENDELEE KUIOMA NAMBA
 
Bila hata ya kutumia hadubini sasa ndio wakati wa kuchambua pumba na mchele.

Chama chetu kilianza na madhumuni mazuri kabisa ya kuwa chama cha kuwatumikia watanzania ambao ni wakulima na wafanyakazi.

Ndio ilikuwa dhima kuu kuleta maendeleo kwa manufaa ya kila mtanzania.

Hakikuwa mali ya wajanja wachache huko nyuma ambao wao ni kushibisha matumbo yao.

Sasa tutafakari na kufanya tathimini juu ya CcM ya leo. Ambayo ni mali ya familia ya wajanja wachache.
Dawa imeanza kuwaingia ndani kabisa. Subirini, hakika mtapona
 
Hoja hapa mezani ni CcM ya wafanyakazi na wakulima. Habari za hayati Magufuli zinatoka wapi?
CCM aka TANU kilijipambanua kama chama cha wakulima wadogo na wafanyakazi.Lakini bila ufadhili wa wafanyabiashara wakubwa kama John Rupiah na watoto wa mjini kama Bibi Titi Mohamed na akina Sykes labda historia ya Uhuru wa Tanganyika igejiandika vingine.

Lakini hata CCM ya baadae ya enzi za Mwalimu Nyerere wakati wa Chama kimmoja ilipambanua kwa alama ya Nyundo yaani wafanyakazi haswa wa viwandani,na jembe ikimaanisha mkulima mdogomdogo.

Lakini baada kuzika Azimio la Arusha na kusimika Azimio la Zanzibar CCM imegeuka Chama cha mission town.Huwezi kukiita Chama cha wafanyakazi kwani viwanda vikubwa vingi vilivyokuwa vinaajiri malaki ya wafanyakazi vimefungwa.

Huwezi kukiita Chama cha wakulima kwa kuwa mazao yao hayapewi soko wala hawapati pembejeo kwa bei ilio nafuu wengi wao wameachana na kilimo.
Labda unaweza kukiita Chama cha wanaotangatanga yaani Bodaboda, Mama Lishe na Wamachinga.Ambso hutumiwa wakati wa kupiga kura,lakini baada ya hapo.....
 
Back
Top Bottom