Sasa wageni kununua dhamana za serikali

Sasa wageni kununua dhamana za serikali

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Serikali imefanya marekebisho kwa sheria ya Benki kuu.

Kuruhusu watu nje ya nchi kununua treasury bonds.

Hii ni hatari kwa uchumi wetu.

We are officially sold out.
IMG-20220609-WA0002.jpg
 
Kwamba tumewaruhusu wageni kuja kuwekeza kwenye dhamana zetu ili nasi tupate sababu ya kwenda kuwekeza kwenye dhamana zao, sijui kama nchi zilizotajwa nao wanaruhusu hiki kitu.

Hatua hii ya serikali kwangu naona ni sawa na kuweka uchumi wetu rehani, itakuwa vipi hao wawekezaji wakiamua kuondoa dhamana zao bila serikali kujiandaa?

Hali hii naona inasababishwa na udogo wa uchumi wetu, tumekuwa tegemezi sana, kuanzia kuchukua mikopo kwenye mabenki ya biashara, hadi kwenye taasisi za kimataifa, na kwa vile wapo wanaoona kukopa ni sifa, basi tujiandae kudumaa zaidi.
 
Wageni kumiliki uchumi wetu.

Nipe mfano wa nchi inayoruhusu mgeni kununua hati fungani za serikali??
Soma vizuri na kwa usahihi aya ya pili ya hilo Tangazo. Unadhani kwanini Tangazo limeeleza kwa nchi za SADC tu? Tangazo limeruhusu Mtanzania pia anaweza kuwekeza huko. Unadhani wangeandika hivyo kama hizo nchi haziruhusu? Sasa hilo swali lako la kutaka mfano wa nchi lina maana gani?
 
Soma vizuri na kwa usahihi aya ya pili ya hilo Tangazo. Unadhani kwanini Tangazo limeeleza kwa nchi za SADC tu? Tangazo limeruhusu Mtanzania pia anaweza kuwekeza huko. Unadhani wangeandika hivyo kama hizo nchi haziruhusu? Sasa hilo swali lako la kutaka mfano wa nchi lina maana gani?
Hii inasaidia nini kama watanzania hawana uwezo wa kushindana na watu wa nje kwa mitaji??

Si ndio tunazidi kuwafanya maskini kwenye nchi yao??
 
Wageni kumiliki uchumi wetu.

Nipe mfano wa nchi inayoruhusu mgeni kununua hati fungani za serikali??
Nchi zote tajiri duniani ndio zinavyokopa ivyo kwa kuuza hati fungani kwa yeyote mwenye uwezo wa kununua duniani. Be it wanunuzi wakubwa ni pension funds zenye mitaji mikubwa, mabank, other investment institutions na serikali ya China.

Nchi maskini hazina uwezo wa kuuza kwenye soko la dunia, ideally kila mtu angependa kuuza huko ni kukopa kwa mtindo wa kujipangia interest za deni mwenyewe.

Huko na kwenyewe kuna rating agencies wenye majina kama ‘Moody’s’, Fitch na ‘Standard and Poor’ wenye kuliambia soko huyu AAA anauewezo wa kulipa deni kirahisi, na huyu ana credit CCC una mkopa at your own perils.

F5816308-ACD6-4408-990E-FE2191C8C91D.jpeg


Tanzania ipo ranked kwenye number 15 last time we tried to get access into international market. Sasa kama kuanzia number 5 kupata mkopo kutoka makampuni makubwa utata ukiwa number 15 sahau kabisa.

Kwa ivyo nadhani lengo ni kukopeshana wenyewe kwa wenyewe ndani ya jumuiya ni jambo zuri, ila bond zetu zina interest kubwa sana kwa sababu ya poor credit rating. Otherwise tumechelewa.
 
Hii inasaidia nini kama watanzania hawana uwezo wa kushindana na watu wa nje kwa mitaji??

Si ndio tunazidi kuwafanya maskini kwenye nchi yao??
Unaleta ujinga sasa. Wewe ulisema tukupe mfano wa nchi zilizoruhusu jambo hilo, tukakutajia hizo nchi, sasa unaleta hoja ya uwezo! Wewe unajua uwezo wa watanzania wote?
 
Navyoelewa mimi kuwekeza katika hati fungani mtu yeyote anaweza kuwekeza tu popote,yaani utoke hapa uende marekani,uingereza,Japan,au China au Australia ukawekeze kwenye hati fungani zao wakukataze hilo halipo.
Kimkakati inawezekana sana tu watu kuwekeza nchi yoyote kwenye hati fungani.
Zingatia Neno kimkakati.
Kwa hapa Tanzania wawekezaji wakubwa wa Hati fungani ukiachana na Tàasisi za kifedha kubwa kubwa na makampuni makubwa watu binafsi wengi tu wanawekeza hasa hasa wahindi,na hao hao ndio wanawekeza sana katika hati fungani nchi za nje hasa hasa Uingereza na Canada.
Kimkakati unawezaje kuwekeza nje ya Tanzania kwenye hati fungani?
Wao wanakwenda kufungua offshore companies huko nje alafu wanaweka mtaji katika hizo companies then hizo companies ndizo sasa kisheria zinaruhusiwa kuwekeza katika hati fungani katika nchi hizo za nje.
Na hata wao sasa wageni wengi hata kabla ya hii kanuni nao waliweza kufanya the same strategy ya kuja kuja na offshore companies ambazo zinanunua shares kwenye holdings companies za hapa bongo wakiwa shared na wabongo then wanaweka capital ambazo hizo holding companies za hapa bongo zinawekeza katika hati fungani za hapa.
Hizo ni international business strategies tu ambazo mara nyingi hata zinawafanya wasilipe kodi nyingi sana kwenye uwekezaji wao.
Mimi naona hii notisi ni kama kutia chachu tu kwa investors wa ndani na nje hasa residents kutoka sadc and east Africa member countries kuja kuwekeza sana kwenye hati fungani zetu.
Ila practically hata pasipo hiyo notisi pia mimi kama mimi kama nina capital yangu kubwa sihitaji kanuni ya bank of Tanzania inipe approval nikawekeze kwenye treasury Bonds za Kenya,Japan,UK,Canada,USA popote pale.

It is possible.

Sent from my SM-J610F using JamiiForums mobile app
 
Wageni kumiliki uchumi wetu.

Nipe mfano wa nchi inayoruhusu mgeni kununua hati fungani za serikali??
Hata wewe unaweza nunua hatifungani za US,,, mfano tu, china ndo wanaingoza kwa kununua hatifungani za US,, na haina maana china inamiliki uchumi wa US,,
Kuuza hatifungani kwa watu wa nje kutatuletea pesa za kigeni lukuki
 
Serikali imefanya marekebisho kwa sheria ya Benki kuu.

Kuruhusu watu nje ya nchi kununua treasury bonds.

Hii ni hatari kwa uchumi wetu.

We are officially sold out.View attachment 2255809
Tuache uoga.. vile ambavyo wanafanya kwetu na sisi tunaruhusa ya kufanya hivyo kwao, ukizingatia ni kwa nchi za jumuia ya Afrika mashariki na SADIC

Sent from my SAMSUNG-SM-J327A using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom