zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Tuweni optimistic aisee!! Kwamba kuruhusu EAC au SADC kununua Hati fungani ndio kutegemea wageni?? Mbona ni reforms kote Africa mashariki why sisi ndio tuone tunaibiwa? Kwanini tusione ni fursa kununua Hati fungani za Burundi huko au Kenya??Kwamba tumewaruhusu wageni kuja kuwekeza kwenye dhamana zetu ili nasi tupate sababu ya kwenda kuwekeza kwenye dhamana zao, sijui kama nchi zilizotajwa nao wanaruhusu hiki kitu.
Hatua hii ya serikali kwangu naona ni sawa na kuweka uchumi wetu rehani, itakuwa vipi hao wawekezaji wakiamua kuondoa dhamana zao bila serikali kujiandaa?
Hali hii naona inasababishwa na udogo wa uchumi wetu, tumekuwa tegemezi sana, kuanzia kuchukua mikopo kwenye mabenki ya biashara, hadi kwenye taasisi za kimataifa, na kwa vile wapo wanaoona kukopa ni sifa, basi tujiandae kudumaa zaidi.
Tujifunze kuaminiana, Sheria zile zile zinazotumika kwa Mtanzania zitatumika kwa wageni. Mbona hatuogopi waTanzania kuondoa dhamana zao ila tuogope wa nje? Hizi mentality za kwamba wageni ni wezi sio sahihi otherwise waTanzania wasingepewa ajira huko ulaya maana wangesema watahujumu nchi!!!