Navyoelewa mimi kuwekeza katika hati fungani mtu yeyote anaweza kuwekeza tu popote,yaani utoke hapa uende marekani,uingereza,Japan,au China au Australia ukawekeze kwenye hati fungani zao wakukataze hilo halipo.
Kimkakati inawezekana sana tu watu kuwekeza nchi yoyote kwenye hati fungani.
Zingatia Neno kimkakati.
Kwa hapa Tanzania wawekezaji wakubwa wa Hati fungani ukiachana na Tàasisi za kifedha kubwa kubwa na makampuni makubwa watu binafsi wengi tu wanawekeza hasa hasa wahindi,na hao hao ndio wanawekeza sana katika hati fungani nchi za nje hasa hasa Uingereza na Canada.
Kimkakati unawezaje kuwekeza nje ya Tanzania kwenye hati fungani?
Wao wanakwenda kufungua offshore companies huko nje alafu wanaweka mtaji katika hizo companies then hizo companies ndizo sasa kisheria zinaruhusiwa kuwekeza katika hati fungani katika nchi hizo za nje.
Na hata wao sasa wageni wengi hata kabla ya hii kanuni nao waliweza kufanya the same strategy ya kuja kuja na offshore companies ambazo zinanunua shares kwenye holdings companies za hapa bongo wakiwa shared na wabongo then wanaweka capital ambazo hizo holding companies za hapa bongo zinawekeza katika hati fungani za hapa.
Hizo ni international business strategies tu ambazo mara nyingi hata zinawafanya wasilipe kodi nyingi sana kwenye uwekezaji wao.
Mimi naona hii notisi ni kama kutia chachu tu kwa investors wa ndani na nje hasa residents kutoka sadc and east Africa member countries kuja kuwekeza sana kwenye hati fungani zetu.
Ila practically hata pasipo hiyo notisi pia mimi kama mimi kama nina capital yangu kubwa sihitaji kanuni ya bank of Tanzania inipe approval nikawekeze kwenye treasury Bonds za Kenya,Japan,UK,Canada,USA popote pale.
It is possible.
Sent from my SM-J610F using
JamiiForums mobile app