Sasa wageni kununua dhamana za serikali

Tuweni optimistic aisee!! Kwamba kuruhusu EAC au SADC kununua Hati fungani ndio kutegemea wageni?? Mbona ni reforms kote Africa mashariki why sisi ndio tuone tunaibiwa? Kwanini tusione ni fursa kununua Hati fungani za Burundi huko au Kenya??

Tujifunze kuaminiana, Sheria zile zile zinazotumika kwa Mtanzania zitatumika kwa wageni. Mbona hatuogopi waTanzania kuondoa dhamana zao ila tuogope wa nje? Hizi mentality za kwamba wageni ni wezi sio sahihi otherwise waTanzania wasingepewa ajira huko ulaya maana wangesema watahujumu nchi!!!
 
Siku zote tulikuwa hatujaruhusu wageni kununua dhamana za Serikali na tukafika hapo tulipofika. Sasa tunajaribu kudikiria nje ya sanduku kuwa "what if" tukiruhusu wageni nao washiriki minada ya dhamana za Serikali.

Personally naamini BOT wamefanya research na wameangalia nchi nyingine zinafanyaje na ndiyo wameona na sisi tujaribu. Naamini wame assess risk na kuweka mitigation measures.
 
Marekani kule kiboko

Ukinunua municipal bond ya dola laki tano unapewa green card na permanent resident permit

Bond wanatumia kuuza uraia
Ila siku ukiwekewa vikwazo na pesa zako zinakuwa 'frozen'
 
Kumpa mgeni haki sawa na mwenyeji ni makosa ambayo hakuna serikali inafanya hapa duniani.
Serekali nyingi zilizobaki Africa ni za Kibepari siyo za kijamaa tena, is all about mkwanja! Lolote lile linawezekana!!!
 
Mawazo ya kimaskini
Huu ndio ukweli.

Hizo hati fungani walizonunua Ma-oligarch wa Urusi huko Marekani na Ulaya zote zimepigwa kufuli na huenda zikataifishwa hapo baadae na kupewa Ukraine.
 
Kote duniani wananunua Kama hujui soma u humi ili ujue parameters za u humi. Mgeni kuwekeza kwenye bonds ni sawa na fdi yaani foregn direct investment ambapo Kuna risk zake na faida zake pia. Kwa hiyo unataka kusema tusiruhusu hata wawekezaji waje kwa sababu wanaweza kuondoka ghafla!! Sasa nini maana ya sheria za uwekezaji kuwekwa. Kuna kitu kinaitwa security policies ambazo ndo zinagovern uwekezaji huo.

Huo ni uninga wako tu kutoelewa Mambo. Soma hata certificate ya financial management au economics.
 
Huyu mleta Mada asipokuelewa tena, bora basi tu
 
Watanzania tuache uvivu
Umeambiwa hata wewe unaweza kufanya kwa nchi zingine za Afrika Mashariki na Jumuiya ya kusini mwa jangwa la Sahara hii SERA sio ya Tz pekee yake ni makubaliano ya nchi zote hizo.
Kama mtanzania una vigezo kanunue pia Rwanda Kenya Uganda n.k
 
Hati fungani means treasury bonds, Unawekeza fedha zako kwa lengo ili upate faida kwa uwekezaji wako, risk yake ipo wapi hapa? Mtaji wako unakuwa umeshikwa na Bot, kwa kipindi maalumu,huku ukilipwa percentage zako,
BINAFSI SIONI UHATARI WAKE
Kitaalamu ni Risk free investment, watu inabidi wasome mambo ya bond and bills kidogo kutanua knowledge maana mtu anaona kama ametekwa kumbe yeye ndo kateka [emoji1787]
 
Chief wabongo wengi bado wana mawazo km nyerere ya kijamaa hawaelewi uchumi wa wa kisasa unavyoendeshwa kwa kifupi wana mawazo mgando, ya kijima hawataki mawazo mapya....na izo bond zipo miaka na miaka na walikuwa hawanunui. Leo hii zimewekwa sokoni kila mmoja anunue imekuwa nongwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…