Sativa alipia matangazo Instagram kuanika uchafu wa Jeshi la Polisi

Sativa alipia matangazo Instagram kuanika uchafu wa Jeshi la Polisi

Ujinga unakusumbua sio kosa lako mtu akuteke akupige risasi upone alafu useme mhusika ujinga unamsumbua kwa hiyo ulitaka awasifie waliomteka aiseee

Kuandika kwenye twitter is the best approach kwa mtazamo wako? Atapata faida gani? Atapata haki yake kuandika huko X?

Endeleeni kumjaza sifa za kijinga wakati nyie mmeweka miguu juu tu makwenu, atayeumia ni yeye na familia yake.
 
Adui yetu ni mfumo siku ambayo vyombo vya Dola vitakapo kua independent na sio kua affiliated na chama Dola ( CCM) solution ya kwanza Ni kupata KATIBA MPYA.

Sasa kamanda wa police anapokea maelekezo kutoka CCM unadhani utapata haki?

Yame shuhudiwa mengi itoshe kusema SATIVA ATULIZE BALL AISHI MAISHA YAKE OTHERWISE AOMBE KWENYE KUISHI SEHEMU SALAMA HUKO EUROPE NA CANADA TRUST ME Akiendelea kua ELEMENT wata mu ELIMINATE na kumuondosha ni very easy Kama KUPULIZA KIBATARI mwenye Masikio na asikie.
Yani watu wanachukulia easy system..ila hao jamaa sio wakucheza nao...ubaya ukute Kuna wahuni wanamtumia na kumpump na huku madhara yake wanayajua
 
Wata mu eliminate "juzi juzi nilikua natembea hapo gerezani kwenye treni nikaona watu wengi sanaaa watu kibao"
Sativa atulize ball Aishi Maisha yake otherwise ataumia.

Haki huinua taifa.
Hakuna mtu anahangaika naye, ana nini cha maana. Hivi bado ana kazi yake ya udalali, au kaingizwa kwenye payroll ya Maria kwa wazungu? Mana kikukicha tu anaubunifu kimtandao zaidi
 
Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa ambaye ni muhanga wa matukio ya utekaji, leo hii amelipia matangazo ya Instagram ili kuanika uhalifu unaofanywa baadhi ya askari wa jeshi la polisi.

Haya ameyaeleza Sativa katika ukurasa wake wa Twitter (X) leo tarehe 06/10/2024, ambapo ametenga bajeti ya Tshs. 135,000/= kwa muda wa siku tano kulipia matangazo hayo.

Ifuatayo ni nukuu kutoka kwenye ukarasa wa X wa Sativa:

MULILO TIME YO SHINE.🔥
Mnalipa CHAWA 20k wanichafue.

Mimi nawalipa INSTAGRAM kuaniaka uchafu wenu.

@tanpol u messed w/ GEN Z.

Budget $50 = 135,000/= TSH.
Duration: siku 5.

@tanpol shindaneni na Technology.😁

Let's Cruise🤝

Mwisho wa kunukuu.
Analipia yeye au da Maria?
 
Mijitu ni mipuuzi sana ,mtu ameumizwa vibaya sana ,nawashauri warudie kuiona ile video sativa yupo chini hata kutembea hawezi analia wampeleke hospital kwa sababu ya maumivu makali wauvae ule uhusika kama wao kisha warudi kutoa mashudu yao hapa jukwaani.

Sativa kashamtambua Mtumishi X wa kituo Y kwanini achukuliwi hatua za kisheria? Zaidi ya J4 kusema tu sativa alitekwa na washikaji ,je hao washikaji wanaweza kumpeleka kitupo cha polisi na kwenda kumuhoji? Kwani kuna kosa sativa kusema waliomteka ni washikaji maana hapo mwanzo alikuwa hajawajua ,mbona hata Zakaria alivyotaka kutekwa taarifa ya awali walisema watu walisiojulikana lakini baadae walikuja kutambulika kwamba ni TISS ,je Zakaria akihojiwa ataendelea kusema alitaka kutekwa na watu wasiojulikna?
Kaka ww acha tu kuna watu waoga yaan viongozi wanawaona kama Mungu vile kumbe nao ni watu tena tumewapa sisi wenyewe hiyo jeuri..
 
Kwani huyo dogo umemsikia anataja CCM??Yeye si anataja watu anaowashuku..CCM unaiingizaje hapo..au nyinyi mnawaza siasa tu muda wote hata kama maisha ya watu yako hatarini??
Wewe unaandika maneno kihisia mkuu.

Ugumu wa maisha usikuchanganye Mzee wangu...CCM ni dude kubwa
 
Sio chadema ni maria ana kakesi kake amemfungulia IGP akishinda alipemwe tubilioni kana mvimbisha kichwa shauri yake
Dogo yuko kina kirefu cha bahari time will tell
Wakili wake amasidie dogo namna wa kujibu na kubehave makubwa mitandaoni anaharibu sana
Hyo ID yako nimecheka sana...😃😃😃
 
Na hivyo walimpiga shaba ya taya..possibly hata kuongea vzr inaweza kuwa shida kwa sasa..ngoja basi afanye maangamizi ya mtandaoni...
 
Sasa Sativa ana kipi kiasi cha kushawishi Polisi wamteke? Au kumuua?
Sasa na yule aliyechoma picha yake aliyechora Mbeya ana impact gani? Hadi Prof Lwaitama kauliza mtu kama Soka mtoto mdogo ambaye hawezi kufanya chochote hana hata kisu wamemuua kwa kipi? Dawsonm Kumbusho alitaka kutekwa kisa tu alipiga picha Expansion Joint Hostel za JIWE na asingepiga kelele angeenda kuuliwa.

Hakuna kosa lolote litakalomfanya mtu atekwe au auawe na watu wasiojulikana ,makosa yote yana adhabu yake kwa mujibu wa sheria ,hao wasiojulikana huwa hawatumii akili yaani mtu akiikosoa serikali wanamteka na kumuua....Kwahiyo wao wanateka kisa kuiokosa sirikali tu na hakuna kingine.......Yaani hata mtu kajamba nani mtaani akiisema serikali vibaya wanamteka...mfano mzuri ni Kijana wa mbeya kachoma picha aliyeichora yeye wameenda kumuua.
 
Una uhakika wote hao wameuawa?
 
Back
Top Bottom