Sativa alipia matangazo Instagram kuanika uchafu wa Jeshi la Polisi

Sativa alipia matangazo Instagram kuanika uchafu wa Jeshi la Polisi

Yeah ,sehemu alipo siyo salama sana ,namshauri aongee vizuri na ubalozi aondoke aende Europe kama aliyoenda Jasusi Chahali na Ngurumo au aende State alipo Da Mange ,huko ni salama kuwapa Makavu kina mafwele na Muliro....kwa E.A Sir100 akipiga simu moja tu kwa Hustler, Sativa anadakwa kama kuku wa MDONDO.
Hata wakimkamata na kumuua ukweli umeshajulikana alafu sio kila mtu atakimbia nchi wengine watabaki hapa hapa
 
Wengi wanaongea hivyo hawajawah pitia tundu la kifo wengi ni wabinafsi na ndo tatizo kubwa la nchi hii
NOMA SANA...

Hivi akikaa kimya, maisha yakaendelea atapungukiwa nini?
Kwa madhila mabaya Sana aliyofanyiwa huyo mtu kukaa kimya ni ngumu Sana, akikaa kimya ataendelea kupata maumivu makali zaidi kuliko akiendelea kuongea ongea Kama afanyavyo hivi sasa.
 
Nimesoma comment za mwanzo nikasema kweli tz mapoyoyo yamejaa kibao!??!.Mtu kapigwa kaumizwa.. kawtambua watu walio mfanyia unyama ule lakini hakuna hatua zinachukulia anaamua kupiga kelele..inatokea mbuzi mbulukenge mazafanta inasema ohooo dogo anapotea dah.....kweli tumelogwa.Hii nchi mtu anaweza akatuuza na hakuna atakaye sema lolote maama imejaa machizi yaan yanawogaaa na heshima za kipuuzi ....
Mijitu ni mipuuzi sana ,mtu ameumizwa vibaya sana ,nawashauri warudie kuiona ile video sativa yupo chini hata kutembea hawezi analia wampeleke hospital kwa sababu ya maumivu makali wauvae ule uhusika kama wao kisha warudi kutoa mashudu yao hapa jukwaani.

Sativa kashamtambua Mtumishi X wa kituo Y kwanini achukuliwi hatua za kisheria? Zaidi ya J4 kusema tu sativa alitekwa na washikaji ,je hao washikaji wanaweza kumpeleka kitupo cha polisi na kwenda kumuhoji? Kwani kuna kosa sativa kusema waliomteka ni washikaji maana hapo mwanzo alikuwa hajawajua ,mbona hata Zakaria alivyotaka kutekwa taarifa ya awali walisema watu walisiojulikana lakini baadae walikuja kutambulika kwamba ni TISS ,je Zakaria akihojiwa ataendelea kusema alitaka kutekwa na watu wasiojulikna?
 
Kwamba kulikuwa na haja gani ya kuacha mapori yote ya karibu na kumpeleka Katavi?

Mbona Dr Ulimboka hakupelekwa katavi na alipona? Issue siyo kupelekwa katavi au mabwepande au ununio ,issue ni dhamira yao ilikuwa nini....Dhamira ya kumteka Sativa ilikuwa kumuua whether huko huko Dar au katavi whatever.

Je kwanini Katavi? kwanini Mbugani? Kwanini kwenye Bwawa la Mamba na viboko? Dar Shememu gani kuna Bwala la Mamba na viboko? Hivi unaangalia channel ya ID? Angalia ili utanue ufahamu kuhusu mauaji ,walichofanya kwenda kumtupa bwawa la viboko ni kupoteza ushahidi mazima maana fisi wa kule wangekula hadi mifupa.
 
Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa ambaye ni muhanga wa matukio ya utekaji, leo hii amelipia matangazo ya Instagram ili kuanika uhalifu unaofanywa baadhi ya askari wa jeshi la polisi.

Haya ameyaeleza Sativa katika ukurasa wake wa Twitter (X) leo tarehe 06/10/2024, ambapo ametenga bajeti ya Tshs. 135,000/= kwa muda wa siku tano kulipia matangazo hayo.

Ifuatayo ni nukuu kutoka kwenye ukarasa wa X wa Sativa:

MULILO TIME YO SHINE.🔥
Mnalipa CHAWA 20k wanichafue.

Mimi nawalipa INSTAGRAM kuaniaka uchafu wenu.

@tanpol u messed w/ GEN Z.

Budget $50 = 135,000/= TSH.
Duration: siku 5.

@tanpol shindaneni na Technology.😁

Let's Cruise🤝

Mwisho wa kunukuu.
Mungu alimrudisha duniani ili amalizie Kazi Na familia yake Sasa naona kasahau anarudia Yale Yale.

Safari hii ataenda mazima huyu Dogo.Unajua Kuna wakati mwingine unapewa tahadhali ya kwamba hapa Kuna hatari Na usiguse Wala kusogelea lakini Kwa kuwa Ni mkaza fuvu basi litamkuta kitu.

CCM ni dude kubwa ambalo MTU mmoja hawezi kulibeba Wala kulisukuma.
 
In my view, Sativa has nothing to lose because he has already lost each and everything during his abduction and when he kept into hostage.
He has nothing to loose? Vipi akivunjwa miguu, vipi wakimtoa macho, vipi wakimuua kabisa, ushajiuliza pengo lake kwenye familia na wanaomtegemea?
 
Hao amabao wako tayari kumwaga ubongo wa watu nakuhakikishia hawataishi milele wote ni wapitaji

Mwache sativa aongee yaani utekwe upelekwe kituo cha polis alafu kamanda wa polisi aje aseme kwa dharau eti ni washikaji ndo wamemteka mambo mengine yanakera
Ni kweli yanakera na kuumiza, hakuna atakaeishi milele, ila bora akae kimya aishi maisha yake.

Ho watu wanatetea madaraka na heshima yao, wako tayari kwa lolote.
 
Kwamba kulikuwa na haja gani ya kuacha mapori yote ya karibu na kumpeleka Katavi?
Binadamu anapotaka kufanya unyama huwa hana sababu, anaweza kuwaza kukupeleka popote. Yule dogo wa madini wa kule masasi aliteuliwa ulisoma mkasa wake wote? Uliona jinsi polisi walivyomchukua huko kwao na sehemu aliyoenda kuuliwa na kutupwa?
 
Mbona Dr Ulimboka hakupelekwa katavi na alipona? Issue siyo kupelekwa katavi au mabwepande au ununio ,issue ni dhamira yao ilikuwa nini....Dhamira ya kumteka Sativa ilikuwa kumuua whether huko huko Dar au katavi whatever.

Je kwanini Katavi? kwanini Mbugani? Kwanini kwenye Bwawa la Mamba na viboko? Dar Shememu gani kuna Bwala la Mamba na viboko? Hivi unaangalia channel ya ID? Angalia ili utanue ufahamu kuhusu mauaji ,walichofanya kwenda kumtupa bwawa la viboko ni kupoteza ushahidi mazima maana fisi wa kule wangekula hadi mifupa.
Sasa Sativa ana kipi kiasi cha kushawishi Polisi wamteke? Au kumuua?
 
Sasa Sativa ana kipi kiasi cha kushawishi Polisi wamteke? Au kumuua?
Kutekwa sio lazima uwe na cha maana Sana, jambo dogo tu linaweza kufanya ukatekwa. Moni centrozone nae aliwahi kutekwa miaka iliyopita, alikua na cha maana kipi?

Hata Ben saa nane alitekwa alikua na kipi cha maana?
 
Twende specifically Kwa Sativa, yeye alikuwa na threat ipi mpaka asumbue hao unaousema walitaka kumuua kiasi cha kumpeleka Hifadhini Katavi
 
Siwaelewi wanaombeza sativa . Huyu mtu ni Mungu tu ndio kamnusuru muwaxheni atoe yake ya moyoni.
 
Back
Top Bottom