Sativa alipia matangazo Instagram kuanika uchafu wa Jeshi la Polisi

Sativa alipia matangazo Instagram kuanika uchafu wa Jeshi la Polisi

Hiyo ndiyo silaha ya mnyonge. Wao wana majeshi na silaha yeye anajitetea kwa kinywa chake. Au unataka pamoja na unyama wote aliotendewa asilie? Akae kimya kwa sababu maneno hayatamfikisha popote? Huyu ni mtu walikuwa wamepanga auawe kwa kumpiga risasi ya kisogo lakini kwa muujiza wa Mungu alipona.
Wangetaka kumuua wasingeshindwa😔
 
Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa ambaye ni muhanga wa matukio ya utekaji, leo hii amelipia matangazo ya Instagram ili kuanika uhalifu unaofanywa baadhi ya askari wa jeshi la polisi.

Haya ameyaeleza Sativa katika ukurasa wake wa Twitter (X) leo tarehe 06/10/2024, ambapo ametenga bajeti ya Tshs. 135,000/= kwa muda wa siku tano kulipia matangazo hayo.

Ifuatayo ni nukuu kutoka kwenye ukarasa wa X wa Sativa:

MULILO TIME YO SHINE.🔥
Mnalipa CHAWA 20k wanichafue.

Mimi nawalipa INSTAGRAM kuaniaka uchafu wenu.

@tanpol u messed w/ GEN Z.

Budget $50 = 135,000/= TSH.
Duration: siku 5.

@tanpol shindaneni na Technology.😁

Let's Cruise🤝

Mwisho wa kunukuu.
Kwa nchi zetu za kiafrika ni kujitafutia matatizo
 
Dogo kapoteza uelekeo huwezi kushindana na watu wazima Muliro jana kamprovoke dogo kama mzazi na dogo kaingia upepo vibaya mno
Wazazi jitahidini kukaa na vijana wenu muwafundishe ukakamavu namna ya kusema na kujibu watu wazima
....watu wazima wanaoteka watu......
 
Huyu dogo maandiko yake mengi hayana mashiko kama mwanaharati. Ana utoto/usela nondo fulani hivi. Hauwezi kucheza na Dola kama Hauna nidhamu na hekima ya hari ya juu.
 
Najua anaumia kwa yale waliyomfanyia, ila mie ningemshauri apotezee tu, watanzania wenyewe tunaopambaniwa ni zaidi mgonjwa wa nusu kaputi, sisi na maiti tofauti yetu ni mwendo tu, watanzania sisi ni maiti zinazoJONGEA.
 
Apotezee kumbuka anajipigania yeye na sio watanzania
Kirahis rahis tu apotezee nchi tuna mazombi wengi
 
Apotezee kumbuka anajipigania yeye na sio watanzania
Kirahis rahis tu apotezee nchi tuna mazombi wengi
Wakati mwingine kukaa kimya ni bora zaidi. Unadhani anaweza shindana na mamlaka katika taifa hili lililojaa wahuni kwenye mamlaka? Ili kulinda hadhi na vyeo vyao wako tayari kumwaga ubongo wa mtu bila kusita..
Ogopa sana mtu anaepambania madaraka na cheo.
 
Back
Top Bottom