Je, hilo ndio litakuwa suluhisho sahihi juu ya tatizo analolalamikia? Vipi kuhusu nafuu ambazo anapaswa kuzipata kutokana na madhara makubwa Sana ambayo amepata??
I'm in unshakable view that running away from the problems is not a way of solving them.
Ni kweli kabisa unachosema.
Hivi vyombo vinavyotuhumiwa kuhusika na vitendo vya utekaji, utesaji na mauaji ya watu kwa hakika vinasababisha janga kubwa sana la kuwepo kwa kujengeka kwa chuki kubwa Sana kati ya Wananchi dhidi ya watawala. Siyo Siri hata kidogo, ipo chuki kubwa sana Kati ya raia dhidi ya Serikali/watawala hususani Jeshi la Polisi, Tiss na watawala wa kisiasa ambao moja kwa moja wanaonekana wananufaika kutokana na kuwepo kwa vitendo hivi vya utekaji Watu na kuwaua. Watu/raia Wana hasira sana dhidi ya vitendo hivi vya utekaji, hali ya kutaka kulipa visasi inazidi kujengeka kwenye mioyo ya Watu wengi wanaoguswa na madhila haya ya vitendo vya utekaji na mauaji, utangamano wa kitaifa unazidi kupotea, uhasama mkubwa kati ya watawala na watawaliwa unazidi kushika kasi hapa nchini, watu wengi wanazidi kupoteza Imani na matumaini dhidi ya Serikali, kila mtu raia wa kawaida kwa Sasa wanaanza kuhisi kwamba adui yake mkubwa zaidi ni Serikali, naiona hatari kubwa sana ipo mbele yetu.
Hali siyo shwari kabisa kwa kweli.