Sativa kutolewa Dar mpaka Arusha kisha kwenda kutupwa Katavi. Inawezekana aliyefanya utekaji huu ndiye aliyepanga shambulio la Lissu?

Sativa kutolewa Dar mpaka Arusha kisha kwenda kutupwa Katavi. Inawezekana aliyefanya utekaji huu ndiye aliyepanga shambulio la Lissu?

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Naamini wote tumeshapata taarifa juu ya tukio la kijana Sativa kupatikana, ambapo alitekwa na watu wasiliojukana na kupatikana leo katika hifadhi ya Katavi.

sativ.jpg

Edga Sativa (Sativa)

Pia soma: Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na watu wasiojulikana

Swali ni kwamba KWANINI ARUSHA? Yaani katika sehemu zote akapelekwa ARUSHA, why? Je, mtesi wake alikuwa Arusha? Na baada ya kuona watu tutaanza kuhoji basi wakamtoa mbali na hapo na kwenda kumtupa Katavi. Fahamu tu kwamba, kwa makadirio kutoka Arusha mpaka katavi ni kama masaa kumi hivi!

Kuna nini hapa katikati?

Kupata taarifa ya polisi soma: Kamanda wa Polisi Katavi: Sativa anasema alichukuliwa Dar akapelekwa Arusha na kutupwa Katavi

====

Hii hapa chini ni tweet iliyowekwa tar 23, na chawa maarufu wa Ummy. Wanapata wapi nguvu ya kutamba waziwazi hivi? Huyu asingekuwa kutoka CCM wangemkamua kisawa sawa, ila sababu ni mtu wao bado anaendelea na kazi zake kama kawaida.

Huyu ilitakiwa aende kuisadie polisi kufanya uchunguzi

ben.jpg

====

Mnakumbuka Mwenyekiti UVCCM Kagera alishawahi kutoa kauli wanaweza kuwapoteza watu na wakifanya hivyo polisi isiwatafute? Ndio wameanza kutekeleza kazi zao?

Kama utakuwa umesahau tamko lile au hukuwahi kuliona pitia hapa: Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

Wakuu #KataaUchawa #KataaUozo2025 #KataaWatuWasiyojulikana #KataaWauaji
 
Kwahy mkuu wa mkoa wa Arusha wa sasa angekuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma kipindi kile mngeunganisha matukio 😂 haya mbona huzungumzii kuhusu Katavi?
 
Mamluki hufuata amri ya anayewalipa.
Alipokufa kiongozi wa Wagner la Urusi kazi yao inaendelea chini ya uongozi mpya na jina jipya ila kazi ni Ile Ile.
Sawa, tuzungumzie Bongo sasa
 
Kwahy mkuu wa mkoa wa Arusha wa sasa angekuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma kipindi kile mngeunganisha matukio 😂 haya mbona huzungumzii kuhusu Katavi?
Soma kwa step nyuki wa Mama.... ila pia ukumbuke "There are no coincidences",. Mimi nimeleta mjadala kwa Ma Great Thinker wa JF
 
Soma kwa step nyuki wa Mama.... ila pia ukumbuke "There are no coincidences",. Mimi nimeleta mjadala kwa Ma Great Thinker wa JF
Sasa ulvosema hayo matukio yanaweza yakawa yamefanywa na watu walewale ulikuwa una maana gani tofauti na hiyo
 
Sasa ulvosema hayo matukio yanaweza yakawa yamefanywa na watu walewale ulikuwa una maana gani tofauti na hiyo
Hata mi sijui, ni swali nimeliacha kwenu Wakuu... inawezekana kuna mtu ana mchele wa kutumwagia hapa.... matukio ya watu wasiyojulikana hayajaisha... mtesi atakuwa anadunda tu mtaani. Hatupendi kuona matukio haya yakiendelea nchini.

Watanzania wote tumehuzunika na kububujikwa na machozi
 
Kama mmeshaijua account na mwenye akaunti jiongezeni tu.
Kazi kazi aiseee))
 
Mimi ni Bora nibaki nashida zangu tu matatizo yangu yananisumbua halafu nikaanze kupapalikia maslahi ya watu hapana! Jamaa alipewa warning akaipost Ile dm ya warning akawa kama amaeikejeli hivi nahisi jamaa ndo wakaanza kumvutia Kasi
 
Huyu kaka ni nani mbona maruweruwe tu ila nmeelewa kinamna
 
Hii mitandao ifungwe tu.

Wazazi tumbo la uchungu linauma.
 
Back
Top Bottom