GE2025 Sativa na Nuruvan wamehujumu maandamano na kuonekana ni uhalifu

GE2025 Sativa na Nuruvan wamehujumu maandamano na kuonekana ni uhalifu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
33,977
Reaction score
67,600
Mwanzo maandamano yalikuwa yanaenda vizuri watu hawakufanya uharibu lakni sativa alitoa maelekezo kuwa waanze kuchoma vituo vya mwendoksi kisha wakaandika tena mtandaoni watu watembelee vituo vya mafuta na kuchoma, kila muda kwenye account yake alikuwa akitoa taarifa za kuharibu miundombinu na biashara za watu binafsi

Haikutakiwa kuwa hivyo bali yeye angewaambia waandamaji wasiguse mali za watu wala za serikali bali wabaki barabarani ili kuonesha ni maandamano ya amani mwisho imetafsiriwa ni uhalifu na kupelekea vijana wengi kuanza kupigwa risasi za moto, hii inaonyesha hakukuwa na mikakati mizuri

Nimeona clip bodaboda akitoa onyo kwa wenzake kuwa fanyeni maandamano ila msiharibu miundombinu lakini mtandaoni sativa anahamasisha vijana waende mpaka ikulu wakachome moto ili hali yeye yupo kwake kazi yake kutoa maelekezo, mbona hakutoa maelekezo ya raia kujilinda na kuepuka vifo na ulemavu? Matokeo yake leo hii wamewaumiza wazazi vijana wamekatishwa ndoto zao kisa watu wachache

Ifike mahali watu tujitafakari, leo inalaumiwa serikali lakini pia hawa watu wanaharakati uchwara hawapaswi kutetewa huwezi andaa mission then unashindwa kuwapa watu mbinu za kujilinda sio sawa kabisa
 
Mungu Fariji waliopoteza Ndugu, Mungu fariji Watanzania.

Hili limeniumiza sana....

Kwa kweli!

Wanabezwa sana na siku zote marehemu hana haki wala hana wa kumsemea, washaitwa wahalifu, wageni toka nchi jirani, chadema, na kila jina baya, wanaweza kujitetea mchangani? Hawawezi, tuliobaki ndio tunaweza kuwasemea tujaribu ICC ndio inawaweza watawala wa kiafrika sisi watatumwaga mavi na damu tu!
 
Ungejikita kwenye mapochopocho tu na kupelekewa moto. Mada hizi nzito nzito huziwezi. Waandamanaji ni maroboti yanayomsikiliza huyo Sativa bila kufikiri? Unajua kuwa vijana hawa wengi wao ni graduates wa vyuo?

Kwa nini watu wameandamana? Kwa nini walikuwa/wana hasira? Nini kifanyike? Bila kugusia haya maswali; na kuelekeza lawama kwa Sativa ni uandunje wa fikra.

Lete mada za mapishi please! 🚮
 
Ungejikita kwenye mapochopocho tu na kupelekewa moto. Mada hizi nzito nzito huziwezi. Waandamanaji ni maroboti yanayomsikiliza huyo Sativa bila kufikiri?

Kwa nini watu wameandamana? Kwa nini walikuwa/wana hasira? Nini kifanyike? Bila kugusia haya maswali; na kuelekeza lawama kwa Sativa ni uandunje wa fikra.

Lete mada za mapishi please! 🚮
Bro jikite kwenye mada achana na matusi hayakusaidi ila hapa tunajaribu kuchambua kila mtu kwa mtazamo wake na maono yake na jinsi gani alivyo lichukulia hili jambo
 
Mwanzo maandamano yalikuwa yana enda vizuri watu haku fanya uharibu lakni sativa aliotoa maelekezo kuwa waanze kuchoma vituo vya mwendoksi kisha wakaandika tena mtandaoni watu watembelee vituo vya mafuta na kuchoma, kila mda kwenye account yake alikuwa akitoa taarifa za kuharibu miundombinu na biashara za watu binafsi

Haikutakiwa kuwa ivyo bali yeye ange waambia waandamaji wasiguse mali za watu wal za serikali bali wabaki barabarani ili kuonyesha ni maandamano ya amani mwisho ime tafsiriwa ni uharifu na kupelekea vijana wengi kuanza kupigwa risasi za moto hii ina onyesha hakukuwa na mikakati mizuri

Nimeona clip bodaboda akitoa onyo kwa wenzake kuwa fanyeni maandamano ila msiharibu miundombinu lakin mtandaoni sativa ana hamasisha vijana waende mpaka ikulu wakachome moto ili hali yeye yupo kwake kazi yake kutoa maelekezo mbona hakutoa maelekezo ya raia kujilinda na kuepuka vifo na ulemavu? Matokeo yake leo hii wame waumiza wazazi vijana wamekatishwa ndoto zao kisa watu wachache

Ifike mahali watu tujitafakari leo ina laumiwa serikali lakini pia hawa watu wanaharakati uchwara hawapaswi kutetewa huwezi andaa mission then una shindwa kuwapa watu mbinu za kujilinda sio sawa kabisa
Yote hayo hayahalalishi mamluki wa Samia kupita kwenye makazi ya watu na kuwafyatulia watu risasi. Watu ambao hata walikuwa hawaandamani.
 
Yote hayo hayahalalishi mamluki wa Samia kupita kwenye makazi ya watu na kuwafyatulia watu risasi. Watu ambao hata walikuwa hawaandamani.

*** Samia.
Ni kweli ujakosea lakini tukifwata historia ya nyuma kuna mambo mengi yalisha fanyika sana ya ovyo ambayo yana tugharimu mpaka sasaivi kama nchi mbona kizazi chenu hamku chukua hatua ya maandamano mpaka leo mna zeeka why kizazi iki mnataka kukihujumu?

Haya yanayo endelea sasaivi ni matunda ya yale ninyi wazee wtu mli yapanda misingi mizuri hamkuifanya mwanzo
 
Hakuna mass protests isiyokuwa na kuchoma au destructions. #M029 haifikii hata kidogo walichofanya gen z wa Nepal. Wale walichoma bunge, mahakama, tv stations, radio stations, five star hotels, nyumba za mawaziri, police stations na magari yao. Lakini idadi ya vifo inakadiriwa kuwa 72. Hawakuwauwa kwa kukodi genge la wahuni.
 
Ni kweli ujakosea lakini tukifwata historia ya nyuma kuna mambo mengi yalisha fanyika sana ya ovyo ambayo yana tugharimu mpaka sasaivi kama nchi mbona kizazi chenu hamku chukua hatua ya maandamano mpaka leo mna zeeka why kizazi iki mnataka kukihujumu?

Haya yanayo endelea sasaivi ni matunda ya yale ninyi wazee wtu mli yapanda misingi mizuri hamkuifanya mwanzo
Hata sijaelewa ulichokiandika! Ni ngumu kufanya mjadala na watu wenye uwezo mdogo wa kuelewa na kujieleza.
 
Back
Top Bottom