GE2025 Sativa na Nuruvan wamehujumu maandamano na kuonekana ni uhalifu

GE2025 Sativa na Nuruvan wamehujumu maandamano na kuonekana ni uhalifu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ungejikita kwenye mapochopocho tu na kupelekewa moto. Mada hizi nzito nzito huziwezi. Waandamanaji ni maroboti yanayomsikiliza huyo Sativa bila kufikiri? Unajua kuwa vijana hawa wengi wao ni graduates wa vyuo?

Kwa nini watu wameandamana? Kwa nini walikuwa/wana hasira? Nini kifanyike? Bila kugusia haya maswali; na kuelekeza lawama kwa Sativa ni uandunje wa fikra.

Lete mada za mapishi please! 🚮
Ndo hicho nilichomuuliza huyo dada juu hapo
 
Usiangalie nani kasababisha maandamano
Angalia hao waandamanaji walikuwa wanaandamana kwa ajiri ya Nini.
Unataka kusema waandamanaji wamefanya hivyo coz ya maria sarungi?
Hapana sijapinga kile walicho kuwa wanadai kabisa ni haki yao kikatiba
 
Ni kweli ujakosea lakini tukifwata historia ya nyuma kuna mambo mengi yalisha fanyika sana ya ovyo ambayo yana tugharimu mpaka sasaivi kama nchi mbona kizazi chenu hamku chukua hatua ya maandamano mpaka leo mna zeeka why kizazi iki mnataka kukihujumu?

Haya yanayo endelea sasaivi ni matunda ya yale ninyi wazee wtu mli yapanda misingi mizuri hamkuifanya mwanzo
Ningeona hii comment yako mwanzon basi nisingehangaika na wewe.
 
maandamano ya amani afu unachoma miundo mbinu ambayo inasidia wengine kwa kigezo tukose wewe aah ujinga tusiupe nafasi

kila mchuma janga hula na wa kwao

jaribu la kupindua serikali ni uhaini na uhaini adhabu yake ni kifo

tulee watoto kwenye maadili na upendo hawa chadema na activists wote walihusika kuhamasisha watafutwe wawekwe mbele ya sheria hawawezi chichea
 
Ungejikita kwenye mapochopocho tu na kupelekewa moto. Mada hizi nzito nzito huziwezi. Waandamanaji ni maroboti yanayomsikiliza huyo Sativa bila kufikiri? Unajua kuwa vijana hawa wengi wao ni graduates wa vyuo?

Kwa nini watu wameandamana? Kwa nini walikuwa/wana hasira? Nini kifanyike? Bila kugusia haya maswali; na kuelekeza lawama kwa Sativa ni uandunje wa fikra.

Lete mada za mapishi please! 🚮
Kupelekewa moto 🧐😳😳😳 unataka kusema kijana amekuwa juisi ya mua ANAKAMULIWA!!?? 😌😔😔
Kama ni kweli huruma, kama si kweli umeongea kwa jazba, tengua kauli mkuu
 
Mwanzo maandamano yalikuwa yanaenda vizuri watu hawakufanya uharibu lakni sativa alitoa maelekezo kuwa waanze kuchoma vituo vya mwendoksi kisha wakaandika tena mtandaoni watu watembelee vituo vya mafuta na kuchoma, kila muda kwenye account yake alikuwa akitoa taarifa za kuharibu miundombinu na biashara za watu binafsi

Haikutakiwa kuwa hivyo bali yeye angewaambia waandamaji wasiguse mali za watu wala za serikali bali wabaki barabarani ili kuonesha ni maandamano ya amani mwisho imetafsiriwa ni uhalifu na kupelekea vijana wengi kuanza kupigwa risasi za moto, hii inaonyesha hakukuwa na mikakati mizuri

Nimeona clip bodaboda akitoa onyo kwa wenzake kuwa fanyeni maandamano ila msiharibu miundombinu lakini mtandaoni sativa anahamasisha vijana waende mpaka ikulu wakachome moto ili hali yeye yupo kwake kazi yake kutoa maelekezo, mbona hakutoa maelekezo ya raia kujilinda na kuepuka vifo na ulemavu? Matokeo yake leo hii wamewaumiza wazazi vijana wamekatishwa ndoto zao kisa watu wachache

Ifike mahali watu tujitafakari, leo inalaumiwa serikali lakini pia hawa watu wanaharakati uchwara hawapaswi kutetewa huwezi andaa mission then unashindwa kuwapa watu mbinu za kujilinda sio sawa kabisa
Mapema tu kwenye saa5 huko Dar alilipotiwa mtu kufariki ...zikaripotiwa risas za moto zimeanza kutumika.
Watu kuona vile ndo wakaanza kuchoma vile ....lakini kuchoma mwendokasi ni kodi zao hata ikulu ni zao waandamanaji police ilikuwa inawauma nini?

Kuchoma mali za mafisadi ni jambo linalokubalika hata mbele za Mungu ni sahihi...sheli nyngi zimechomwa Jwtz wakiwa wanaona
 
Hakuna mass protests isiyokuwa na kuchoma au destructions. #M029 haifikii hata kidogo walichofanya gen z wa Nepal. Wale walichoma bunge, mahakama, tv stations, radio stations, five star hotels, nyumba za mawaziri, police stations na magari yao. Lakini idadi ya vifo inakadiriwa kuwa 72. Hawakuwauwa kwa kukodi genge la wahuni.
Reasoning yako ni ya kipumbavu sana. Kumbuka hapa sio Nepal. Ukifanya ujinga utajibiwa kadiri ya ujinga wako. Huwezi kuchoma mali za watu ukachekewa. Mtu mwenye nia ya kutumia kidumu cha petrol kuleta madhara anastahili risasi ya moto kwa sababu ni gaidi. Humu JF kuna Lord Denning alikuwa akihamasisha vijana wafanye uharibifu na mauaji je kuna faida aliyopata?
 
Back
Top Bottom