Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Sativa225 (Edgar Mwakabela) kijana maarufu kwa kukosoa serikali X apatikana, baada ya kutekwa na ‘watu wasiojulikana’

Wakuu Salama,

Sativa amekuwa akitafutwa toka weekend (Jumapili - 23/6/2024), baada ya ndugu zake kumtafuta bila mafanikio.

Watetezi wa haki za binadamu wamepiga kelele kuhusu hili hata mmojawapo wa viongozi wa ACT Wazalendo Rahma Mwita alizungumza suala hili kwenye kwenye XSpaces jana 26/6/2024 kuwa yupo tayari kujitolea muda wake kuambatana na ndugu wa kijana huyo kwenda kwenye vyombo vya habari na asasi mbalimbali za kiraia kupaza sauti kuhusu kupotea kwa kijana huyu.

Edgar anaishi Mbezi kwa Msuguli na amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.

Kama kelele zisingepigwa huyu ndio ilikuwa ntolee, halafu kuna chawa wanaotetea ujinga kila siku.

Kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera kuhusu kuwapoteza watu soma hapa: Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

Aisee, wakati wa kubadilika ni sasa, mtu akipotea wote tupige kelele, serikali ikienda kushoto wote tupige kelele. Isiwe kazi ya wanaharakati wachache au watetezi wa haki za binadamu, peke yao hawawezi. Tukiungana wote tunakuwa na nguvu.

Tuendeleze hashtag Wakuu, #KataaMachawa #KataaUozo2025, amsha kila utakayeweza kumuasha, tushikamane na kuteteana wakati wote kuleta uwajibikaji nchini.
Wabongo nguvu ya soda.............Tujifunze kwa jirani zetu hapo juu,,,,
 
HALAFU wanatokea watu wanasema anayehusika ni CHAMA FULANI ama ni TAASISI FULANI......! wakati mtu kutwa kuchwa KUTUKANA........
Wewe unaenda kuwatukana watu huko mitusi mikubwa mikubwa mbaya zaidi unawaonyesha mpaka Sura yako unategemea wakufanyie nini wakuvalishe Kitenge?
 
Anko chatu ndio nani mkuu?
Ndio Ankali Chatu huyu hapa unataka na Wewe ukamsalimie? Ushakula Mafunzo ya kupigana nae lakini?
Screenshot_20240627-220013.png
 
Hapo wanapanga kumpelekw police kwanza kabla ya kumfikisha hospitali!
Unbelievable.
Eti ndivyo sheria/taratibu inavyotaka hivyo. Sio kosa la wananchi. Ni kosa la wajinga wanaotunga sheria mbovu kama hiyo.
 
Hospitali zetu unaweza kumfikisha wakakataa kumtibu mpaka awe na PF3

Kuna jamaa yetu alishavamiwa akachomwa na visu tumekimbia police haraka kupitia pf3 hapo tumepanic balaa akatoka askari ile tunamwambia tuandike haraka jamaa linajibu "huyo mbona bado mpya, hata hajapigwa sana, Kuna watu wanaletwa hapa wamechakaa" 😃
Utaratibu huu ni lazima ubadilike.
 
Wakuu Salama,

Sativa amekuwa akitafutwa toka weekend (Jumapili - 23/6/2024), baada ya ndugu zake kumtafuta bila mafanikio.

Watetezi wa haki za binadamu wamepiga kelele kuhusu hili hata mmojawapo wa viongozi wa ACT Wazalendo Rahma Mwita alizungumza suala hili kwenye kwenye XSpaces jana 26/6/2024 kuwa yupo tayari kujitolea muda wake kuambatana na ndugu wa kijana huyo kwenda kwenye vyombo vya habari na asasi mbalimbali za kiraia kupaza sauti kuhusu kupotea kwa kijana huyu.

Edgar anaishi Mbezi kwa Msuguli na amepatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana, hali yake ikiwa si nzuri.

Kama kelele zisingepigwa huyu ndio ilikuwa ntolee, halafu kuna chawa wanaotetea ujinga kila siku.

Kauli ya Mwenyekiti wa UVCCM Kagera kuhusu kuwapoteza watu soma hapa: Mwenyekiti UVCCM Kagera, Faris Buruhan: Tukiwapoteza wanaomtukana Rais Samia mitandaoni, Polisi msiwatafute

Aisee, wakati wa kubadilika ni sasa, mtu akipotea wote tupige kelele, serikali ikienda kushoto wote tupige kelele. Isiwe kazi ya wanaharakati wachache au watetezi wa haki za binadamu, peke yao hawawezi. Tukiungana wote tunakuwa na nguvu.

Tuendeleze hashtag Wakuu, #KataaMachawa #KataaUozo2025, amsha kila utakayeweza kumuasha, tushikamane na kuteteana wakati wote kuleta uwajibikaji nchiniS

Hakunaga Kiongozi asiye katili duniani

Ndio sababu Hapa kwetu akiapishwa anapewa Mkuki 😂😂
Mm sijajua kukosoa kama mtu kakosea hasa kiongozi ni kosa? Ila naamini kukosoa Kwa matusi na maneno ya kejeli ni kosa kubwa!!
Mwamba kapigwa kama ngoma
 
Back
Top Bottom