Saudi Arabia has announced end of dollar dominance in global oil trade. The dominoes are beginning to fall on the US evil empire

juzi umesahau Urusi au hupo vijiwe vya kahawa
Unaongelea nini hapa ?, Nashindwa kukuelewa....

Angalia mambo kwenye business point of view; Mwarabu ana faida gani ya kukataa Pesa za nchi nyingine na kulazimisha itumike Dollar ? Je inafanya mafuta yake yauzike zaidi sokoni ?

Mwenye faida ni nani ?, Na aliweza vipi kufanikisha / kulazimisha hilo litokee ? , Na je bado anao uwezo wa kuendelea kulazimisha hivyo ?....

Mambo ni Dynamic na jambo moja linaweza kupelekea jambo lingine pia Dedollarization sio concept mpya imekuwa ikifikiriwa kwa muda mrefu and the economic power shift from west to east inaweza ikafanikisha jambo hilo;

Anyway my own two cents......, kuwa na One leading Superpower is not Safe for the World...
 
Hicho kitu ni kigumu sana kutokea.itakua WWIII
Niambie kwa nini iwe WWIII.Kutumia Dollar kama Petro Dollar ilikuwa by design,so it can be removed by design,wala hakuna lazima kutumia Petro Dollar.Ni kweli Wamarekani watakasirika,we know, lakini kama nchi zingine zote zitaungana,there is nothing America can do,they will have to sit down and watch the Empire crumble.

Tunajua walimuua Gadafi alipofanya jambo kama hili,sasa tusubiri tuone kama watamuua MBS.

 
Kama mtu hujui uchumi utaishia kusema hii ndoto ya mchana. Kwa wasiojua biashara kubwa duniani inafanyika kwa malipo ya dola over 38% sawa na almost 90trillion dollar. Sasa kati ya hizo transaction 55% ni mauzo ya mafuta peke yake. Na wauzaji wakubwa wa mafuta duniani Russia na Saudia tayari wanaacha kutumia dollar kama pesa ya malipo.

Lapili ili ununue mafuta lazima uwe na dollar ili ufanye malipo kutoka kwa wauzaji. Hivyo unaponunua dollar maana yake US lazima ahakikishe zipo za kutosha kwenye mzunguko zikipungua anaongeza.

Tatu unapoacha kununua mafuta kwa fedha uliyokuwa unatumia awali(dollar) zile unazoacha kuzitumia zinarudi kwa mwemyewe(US). Pesa hizi hazirudi kama sadaka bali kupitia mauzo namanunuzi mbalimbali sasa zitakuwa nyingi kwemye mzunguko kulko mahitaji. Matokeo

Thamani ya hela husika inashuka(dollar inapoteza thamani). Kisha inapelekea kupanda kwa gharama inflation.

Kwa nini saudia ni hatari? Kwa sababu kiwango cha dollar anachotumia kufanya biashara ni kikubwa sana kusababisha madhara makubwa marekani na dunia kwa ujumla.
 
Mpango wa BRICS ni kwamba kila nchi ifanye biashara tokana na sarafu yake,,,,.......na sarafu wanataka zisapotiwe na resource fulani aidha dhahabu au madini mengine, ndo maana kwa sasa kuna nchi zinakusanya sana dhahabu.....ukienda kununua bidhaa nje,tuseme ndo hayo mafuta ukaambiwa ulipe kwa pesa yako...watapima thamani ya pesa yako tokana na soko la dhahabu lilivyo (mf....gram5 ya dhahabu ni sawa na tsh2), dollar ni mfumo wa kuprint tu makaratasi ila nyuma yake hayana kitu chochote cha kubeba thamani yake na ni sarafu ya kinyonyaji sana
 
Mabeberu wanaojidai werevu zaidi ya Mrusi na walio upande wake.🤔
 
Kuna watu (wagonjwa akili) huu mjadala watauamishia kwenye dini.


😂😂😂
Mtu yeyote akifanya hivyo atakuwa kakosea sana.Hakuna issue ya dini hapa.Wanauza mafuta yao popote,watauza nchi za Kiislamu na Kikristo, ila Dollar ya Marekani haitatumika as "the only" Currency in oil transantions.Una Yuan lete,una Ruble lete,una South African Rand lete,una Indian Rupee lete,bora tu iwe convertible na backed by a commodity like Gold or Silver,isiwe Fiat Currency kama ilivyo US $ kwa sasa.
 
Mafuta yatahitajika sio kwa magari tena kwani electric cars zimeanza kujaa
Hadi zije kua common sio leo,,,,tena zile full electric bado kabisa kuna gari chache sana ambazo ni full electric na nyingi ni ndogo hazina nguvu, kwa sasa wengi wanatumia hybrid inakua inatumia mafuta na umeme,,,,,.....gari za mafuta hadi zije kuondoka kabisa sijui kama wengine tutakua hai hasa kwa huku africa wazee wa used cars
 
Natural news sijawahi hata kuisikia [emoji1] [emoji1787]
Utaisikia wapi,ninyi mmezoea main stream media kama BBC,Aljazeera,CNN,CGTN,SkyNews etc.,ambapo mnalishwa mataka taka or fake news.Natural News is an independent news source,ambapo mabeberu hawana mkono wao,so you get the real news about them.Mainstream Media reports what they:the NWO Cabal, wants you to hear.
 
Sio kweli mkuu
Vans zimejaa sana za electric na magari madogo yanaongezeka kila siku
Naziona 100% electric vans kuanzia kampuni ya Amazon ndio wameyanunua haswa na hata Royal mail
Hizi zimejaa sana na takwimu za [emoji636] pekee zipo 660,000 barabarani kwa sasa
Kwa Afrika tunafuata mkumbo tu bado sana
Kama Tanzania nzima ni magari 700,000 ya kawaida na wenzetu ya umeme tu zaidi ya laki 6 sasa na ndio kwanza yanafyatuliwa kila kukicha
Don't get me wrong bro
Gari za mafuta itachukua miaka kupotea ila zitabaki nchi masikini tu kwa wingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…