Saudi investors eye Tanzanian farmland

Saudi investors eye Tanzanian farmland

Mimi naona waruhusu mkataba lakini si kwa miaka 99. Miaka 99 ni kwa Watanzania na hatuwezi kukodisha mashamba kwa miaka 99. Kila miaka mitano kufanyike review kuona kama masharti ya mkataba yanafuatwa huwezi ku rent mashamba kwa vizazi vijavyo ni lazima tu sign mikataba kwa miaka yetu na si kwa wajukuu.
 
Tatizo ni kwamba hutampata mwekezaji atakayekuwa tayari kuwekeza pesa yake mahali ambapo anajua baada ya miaka 5 kuna uwezekano wa kunyang'anywa. Hata wewe huwezi kukubali. will you?
 
wakati tunapat uhuru, tulikua watu milioni saba tu. miaka 48 baadae tuko kama milioni 50 hivi. sasa tukiwapa waarabu ardhi kubwa kiasi hicho kwa miaka 100, wakati tutakuwa tumeongezeka na kuwa kama milioni 150 hivi, ndio tutakua tumefanya nini. saudi ni janwa naa hawajui kulima, sasa huo utaalamu wameupata wapi wa kulima ngani? hivi sisi tunaweza kupata hata kiwanja tu cha kujenga Uarabuni. Mungu atuweke na ujinga wetu.

macinkus

Good point. This is why family planning cannot be separated from economic policies. UNFPA data zinaonesha kuwa by 2050, tutaongezeka kufikia 80 millions. And this is regardless of the fact that we have already started the demographic transition [declining fertility and mortality rate]. Intuitively kuongezeka kwa idadi ya watu kunaonekana kuwa na madhara kwa ubora wa maisha. But there's no consensus on the causal linkage between population growth and economic development.

On your second point, waarabu ni kweli hawajui kulima na nchi yao ni jangwa lakini wana pesa and probably brains [meaning they know what they want]. So, you should not be surprised to see Monsato or any other giant producing food in Tanzania on behalf of Saudis.
 
Serikali haiwezi ku rent sehemu kubwa hivyo kwa miaka 99 kwani wajukuu wetu hawata kubali hilo. Hivyo miaka ipunguzwe na kuwe na kipindi cha kuangalia huwezi kuhakishia wawekezaji kuchukua shamba kwa miaka 99 kwani sijawahi kuona mkataba wa miaka 99!. Wananchi tuna mikataba ya mika 99 kwasababu ardhi ni ya serikali na sisi ni wazawa lakini si kwa wageni.
 
Wana JF, nafarijika kusoma maoni mbali mbali kuhusu swala la ardhi. Mawazo mengi juu ya swala hili yanatetea hoja kwamba serikali iwe makini katika kuingia mkataba wa kukodisha ardhi, itakuwa vizuri zaidi kama swala hili kuweka wazi (transparent) na kwa maslahi ya uma.

Kuhusu ombi la Saudi kukodi Ardhi Tanzania, mie nina mawazo mawili juu ya swala hili

1. Ningekubaliana na Serikali ya JK kuwapa lease ardhi ya miaka 99 kwa wa-Saudi au Saudi Royal Family (SRY), kama na wao wako tayari kutupa lease ya visima vya mafuta (crude oil) huko kwao Saudi ambayo thamani (economic returns) yake ni sawa na watakayopata SRF kwa kupata ardhi yetu. Tuna wachumi na wanasheria ambao wanaweza kuweka mkataba huu ukaka vizuri kwa manufaa ya nchi mbili. Hoja kuu hapa ni kwamba Saudi wanatatizo la chakula (food security) na sisi tunatatizo la mafuta (crude oil and its products), kwa hivyo basi tufaidi wote.

2. Vile vile Saudi waje lakini wawekeze kwenye food processing & preservation na vyakula wanavyo process wanunue toka kwa wakulima wetu. Hii inawezekana kabisa inajenga hoja ya kufufua mashamba kama yale ya Nafco nk. Wote tunajua msimu wananasi na machungwa mambo yalivyo huko nyumbani, mazoa mengi, bei powa na uharibikaji mkubwa kwa ukosefu wa storage & preservation facilities. Pamoja na hilo kuna wakulima wengi Tanzania ambao wanaweza kuzalisha kwa wingi mazao ya aina nyingine, tatizo kubwa ni soko, processing/preservation and storage. Mfano wa karibu zaidi unapatika kwenye taarifa ya gazeti la Raia Mwema kuhusu maradi wa kilimo cha umwagiliaji Igomelo Mkulima Mbeya amtambia Pinda

Tanzania ina Ardhi ya kutosha, Serikali inawajibu kuhakikisha hili swala la ukodishaji wa ardhi linifanywa kwa maslahi ya umma. Mifano hapo juu ni hatua mojawapo ambapo swala hili laweza kutekelezwa.

Asanteni, tuendelee kuchambua na kuchangia mswala muhimu ya nchi yetu
 
Wana JF, nafarijika kusoma maoni mbali mbali kuhusu swala la ardhi. Mawazo mengi juu ya swala hili yanatetea hoja kwamba serikali iwe makini katika kuingia mkataba wa kukodisha ardhi, itakuwa vizuri zaidi kama swala hili kuweka wazi (transparent) na kwa maslahi ya uma.

Kuhusu ombi la Saudi kukodi Ardhi Tanzania, mie nina mawazo mawili juu ya swala hili

1. Ningekubaliana na Serikali ya JK kuwapa lease ardhi ya miaka 99 kwa wa-Saudi au Saudi Royal Family (SRY), kama na wao wako tayari kutupa lease ya visima vya mafuta (crude oil) huko kwao Saudi ambayo thamani (economic returns) yake ni sawa na watakayopata SRF kwa kupata ardhi yetu. Tuna wachumi na wanasheria ambao wanaweza kuweka mkataba huu ukaka vizuri kwa manufaa ya nchi mbili. Hoja kuu hapa ni kwamba Saudi wanatatizo la chakula (food security) na sisi tunatatizo la mafuta (crude oil and its products), kwa hivyo basi tufaidi wote.

2. Vile vile Saudi waje lakini wawekeze kwenye food processing & preservation na vyakula wanavyo process wanunue toka kwa wakulima wetu. Hii inawezekana kabisa inajenga hoja ya kufufua mashamba kama yale ya Nafco nk. Wote tunajua msimu wananasi na machungwa mambo yalivyo huko nyumbani, mazoa mengi, bei powa na uharibikaji mkubwa kwa ukosefu wa storage & preservation facilities. Pamoja na hilo kuna wakulima wengi Tanzania ambao wanaweza kuzalisha kwa wingi mazao ya aina nyingine, tatizo kubwa ni soko, processing/preservation and storage.

1. Assume wewe ni mwakilishi wa Saudi Arabia kwenye mazungumzo, ungekubaliana na point ya 1?

2. Wanachotaka hawa jamaa ni kulima mpunga na ngano. Hawajasema kwamba wana tatizo la mananasi na machungwa. Ni kweli tungependa wawekeze kwenye usindikaji wa chakula, but it's not in their interest to do so. How do you negotiate that?

3. Kitu kingine cha kufahamu ni kuwa hawa jamaa hawalazimishi and we are not a monopoly when it comes to land supply. So, tukiona hakuna maslahi, tunaweza kukataa. Other countries will grab the opportunity and play the cards appropriately.
 
Jasusi,
Mkuu wewe ni Mtanzania una jumba hapo US, sijui umekodishiwa kwa miaka mingapi au umeuziwa kabisaaa!... hivi kweli bongo ingewezekana kwa mtazamo wa JF!

Wanabodi,
Wabongo jamani mimi najua tatizo ni jina SAUDIA kama ingekuwa Marekani msingefikia hapa. Nakumbuka tulikuwa na mjadala kuhusu Marekani kuweka kambi yao TZ watu kibao humu JF walisherekea jambo hilo, akaja Bush kanunua ardhi wala sii muda mrefu nikaliweka hapa watu wakadai ni jambo zuri, leo tunasikia tu SAUDIA imekuwa rafu!..
Haya vyama vyote hupokea misaada toka nchi za nje iwe Ujerarumani, Uingereza, na kadhalika..Kikwete kapewa kotoka Iran na Oman tayari watu wamelidakia wanataka kujua ukweli..hizi double standard zitaisha lini. Kosa ni kosa tu kama kukodiusha ardhi yetu ni kosa basi watu wote waliowekesha nchini na kukodishiwa ardhi within miaka ya Kikwete waondolewe..It;s not about kitu gani wanalima kwani Colombia unajulikana duniani kwa kulima Kahawa na pato lake kubwa (kodi) linatokana na mauzo ya kahawa wakati wamiliki wa kahawa hizo ni mashirika ya Kimarekani.
Huu ndio Ubepari wakuu zangu mlifikiria Ubepari ni kuvuna tuuu!..welcome to the club, tukisema sana tunaitwa wajamaa kumbe nyie ndio Wajamaa sana tu.

What the heck!
 
Mwenzako alibinafsisha kila kitu sasa tumbo joto kila kunapokucha wewe sasa unataka kuuza na ardhi kabisa eti 99yrs wapi hata katika maandiko matakatifu hakuna kitu kama hiki eti ardhi wanakodishiwa watu wa mataifa ya mbali.Mkuu alikuwa ametoka usingizini au halafu watanzania waende wapi? kama wanataka kuja kuwekeza katika kilimo ni jambo la msingi kwani italeta ajira kwa watanzania na chakula lakini sio kuwapa mikataba eti ya miaka 100 na ushee..sasa huyu anataka kutuuza hata na sisi wananchi kwa waarabu. Ubwanyenye na usultani uliisha miaka hiyo msiturudishie ukoloni sijui ndio mamboleo au ni nini. mnashitushwa na trillions hawa watu wanaweza kuwa wasanii tu hakuna lolote.Nyerere amka huko uliko uone watu wako wanavyotaka kuiuza nchi kwa mwarabu sasa sio mhindi tena au mzungu sasa hivi ni mwarabu kwa kwenda mbele
 
Uwekezaji utakaoiondoa Tanzania kwenye umasikini sio wa kimachinga kama wachina wanavyofanya pale kariakoo. Wala sio wa madini ambayo tayari Mkapa na genge lake wameshafunga kwa mikataba isiyofunguka leo wala kesho. Uwekezaji tunaohitaji kwa nguvu zote kwa sasa ni katika kilimo. Cha muhimu baada ya kuumwa na nyoka sasa tuwe makini. Tusianze kuukataa uwekezaji huu kabla ya kujua mkataba unasemaje.

Ukweli nikwamba mkataba ukiwa mzuri, wenye maslahi kwa pande zote (win-win) basi tutaibuka kwa kasi sana kiuchumi. hapa ndipo maisha ya watanzania wengi yatakapobadilika kwa kasi. Lakini tukirudia yale makosa na ubabe wa Mkapa kwenye IPTL, Madini na ubinafsishaji wa mabenki, na nishati kwa ujumla yatakuwa ni yale yale tu tuliyoyazoea.
 
Jasusi,
Mkuu wewe ni Mtanzania una jumba hapo US, sijui umekodishiwa kwa miaka mingapi au umeuziwa kabisaaa!... hivi kweli bongo ingewezekana kwa mtazamo wa JF!

Wanabodi,
Wabongo jamani mimi najua tatizo ni jina SAUDIA kama ingekuwa Marekani msingefikia hapa. Nakumbuka tulikuwa na mjadala kuhusu Marekani kuweka kambi yao TZ watu kibao humu JF walisherekea jambo hilo, akaja Bush kanunua ardhi wala sii muda mrefu nikaliweka hapa watu wakadai ni jambo zuri, leo tunasikia tu SAUDIA imekuwa rafu!..
Haya vyama vyote hupokea misaada toka nchi za nje iwe Ujerarumani, Uingereza, na kadhalika..Kikwete kapewa kotoka Iran na Oman tayari watu wamelidakia wanataka kujua ukweli..hizi double standard zitaisha lini. Kosa ni kosa tu kama kukodiusha ardhi yetu ni kosa basi watu wote waliowekesha nchini na kukodishiwa ardhi within miaka ya Kikwete waondolewe..It;s not about kitu gani wanalima kwani Colombia unajulikana duniani kwa kulima Kahawa na pato lake kubwa (kodi) linatokana na mauzo ya kahawa wakati wamiliki wa kahawa hizo ni mashirika ya Kimarekani.
Huu ndio Ubepari wakuu zangu mlifikiria Ubepari ni kuvuna tuuu!..welcome to the club, tukisema sana tunaitwa wajamaa kumbe nyie ndio Wajamaa sana tu.

What the heck!
Mkandara,
Tatizo si Saudia (as far as I am concerned). Tatizo kwangu ni ukosefu wa sera katika serikali yetu. Tunajua Saudia kuna soko la mchele na ngano. Tunajua tuna ardhi nzuri na pia tunajua kuwa asilimia 80 ya raia wetu ni wakulima. Tuna shida gani ya kulishika hilo soko la Saudia kwa kuongeza uzalishaji wa mpunga na ngano badala ya kuwaalika Wasaudia waje wajilimie wenyewe kwenye ardhi yetu.? Mimi ningefurahi sana kama Mwungana angerudi na kuwaambia wakulima wetu wa mchele pale Kyela kuwa nimewapatieni soko la uhakika, ongezeni uzalishaji wa mpunga ili tuweze kuuuza mpunga wetu Saudia na kuliongezea taifa kipato. Kwa mtaji huo hata mimi ningefikiria kutafuta shamba Kyela. Huo ndio mtazamo wangu. As far as kuwa na nyumba Marekani, ninahenya na mortgage kwa miaka 25 ijayo. Lakini kuwapatia wageni wowote ardhi ilhali watu wetu wanaendelea kuteseka na umasikini ni uhaini wa hali ya juu kwa upande wa viongozi wetu. Hii si kwa Saudia peke yake, bali hata Holland ambao wanalima maua kule Arusha au Sweden ambayo ilitaka mashamba ya jathropa kabla ya bei ya mafuta kupungua.
 
Jamaa anajionyesha rookie katika diplomacy, yaani aide wa rais anaenda kusema maneno potentially explosive kama hivyo unnecessarily?

Hivi alishindwa kusema tu kwamba ni lazima tuhakikishe kwamba deal linakuwa "mutually beneficial"?

Hivi ma aide wa Yar'Adua wakitoa comment za reja reja kuhusu Tanzania hawa wakuu wataweza kufanya nao deal? Vipi kesho Kikwete akienda Nigeria na January Makamba halafu Wa Nigeria wakimbana kuhusu hii kauli?

Si lazima kusema kila kitu ina a sensational anecdotal way. Yaani kuna watu ukiwapa mistari miwili tu ya kuongea hawakosi kuongea pumba!

Halafu anaongea kuhusu situation ya Nigeria kama wao wana moral authority, bongo kuna resources kibao dhahabu, ardhi, mito, lakini bado watu wanakufa na njaa, what is the difference?

Ndugu, just confess that you have some personal issues with January Makamba. The discussion is about 'LAND LEASING' and not about the example he gave. Instead of blaming, why don't you come up with some intelligent ideas and suggestions on what to do in order to help if you think this decision isn't going to benefit us?
Grow up!
 
sikubaliani kabisa na mpango wa kulease ardhi kwa waarabu siyo kwa sababu ni idea mbaya ila kwa sababu hatuna uongozi intelligent enough kuingia mkataba kama huu.Kama tukiamua kuingia huu mkataba tunaweza kujifunza mengi kutoka kwa Saudi Aramco na mikataba ya mafuta na western companies
 
Mkandara,
Tatizo si Saudia (as far as I am concerned). Tatizo kwangu ni ukosefu wa sera katika serikali yetu. Tunajua Saudia kuna soko la mchele na ngano. Tunajua tuna ardhi nzuri na pia tunajua kuwa asilimia 80 ya raia wetu ni wakulima. Tuna shida gani ya kulishika hilo soko la Saudia kwa kuongeza uzalishaji wa mpunga na ngano badala ya kuwaalika Wasaudia waje wajilimie wenyewe kwenye ardhi yetu.? Mimi ningefurahi sana kama Mwungana angerudi na kuwaambia wakulima wetu wa mchele pale Kyela kuwa nimewapatieni soko la uhakika, ongezeni uzalishaji wa mpunga ili tuweze kuuuza mpunga wetu Saudia na kuliongezea taifa kipato. Kwa mtaji huo hata mimi ningefikiria kutafuta shamba Kyela. Huo ndio mtazamo wangu. As far as kuwa na nyumba Marekani, ninahenya na mortgage kwa miaka 25 ijayo. Lakini kuwapatia wageni wowote ardhi ilhali watu wetu wanaendelea kuteseka na umasikini ni uhaini wa hali ya juu kwa upande wa viongozi wetu. Hii si kwa Saudia peke yake, bali hata Holland ambao wanalima maua kule Arusha au Sweden ambayo ilitaka mashamba ya jathropa kabla ya bei ya mafuta kupungua.

Soko la ndani wameshaliweza? If you cannot feed yourself, how can you feed others?
 
mara nyingi mikataba mikubwa miaka 20 - 25 na katika huu muda wawaekezaji wanakuwa washapata faida kibao
hii mikataba pia tunaishindwa....

mikataba ya ardhi ipo ya miaka 33, 66 na 99
kwa nini JK anataka kutoa wa miaka 99 wakati wa miaka 33 ni enough kwa saudia kurudisha hela yao
99 years is too much, nchi gani inasign mikataba ya miaka 99
JK tuonyeshe basi unaakili kidogo angalau mkataba uwe wa miaka 33....
mimi kijana sina familia kwa hiyo inamaanisha mungu akinijalia familia huu mkataba utakuwa kwa ajili ya watoto, wajukuu. vitukuu ndio vitaweza kuuwangalia upya du......
 
wanaojua maswala ya ardhi kwa kina, je mnajua hali ya umiliki ikoje kwa sasa katika hayo mafungu matatu ya ardhi? wenyeji vs wageni? na yatumikaje? Ardhi ya jumla imebaki kiasi gani, ama ndio wameanza kufuata za vijiji! Kwenye hifadhi kukoje? umiliki wake je! - well sio umiliki- haki ya matumizi-- ndio huohuo umiliki-- miaka 99.

Kinachotokea ni kuwa kwavile hakuna mtu mwenye ownership ya land ila individuals or groups wana bundles of rights depending on the position then kwa upande wa ardhi ya vijiji wanakijiji ni propriators that means they are second from state and they have all remaining four bundles of rights of propriatorship, management, user and access and for that case wanauwezo wa ku transfer hizo rights and not a right to sell, through leasing to investors kwa makubaliano either compansation or what. Hii ina procedure zake na sheria na policy inaelezea. kibaya kinachotokea wachache wenye uchu wana wadanganya wanakijiji ambao analysis yao ni ndogo na hivyo wanakijiji wana sign makubaliano hayo bila kujua the long term effects ila baadae wanakuja ku realize they made a mistake or some times few elites in the village wana enda against bado kwakua nguvu yao ni ndogo na mambo ya kuogopa ku fall victim wananyamaza. Ambacho hatujui ni kuwa information flow inakuwa kubwa sasa na demand to land is growing due to population growth and increase in marginal value for land baadae itakapo fika sasa walio na ardhi niwachache na wengi hawana access ndo struggle zitaanza kama nchi za Kenya na kwingineko. Ofcourse kwa sheria rais anaweza ku tengua hayo maamuzi kama kuna justifiable reasons and following proceedures tatizo nikuwa wale occupants watahitaji compansation sasa kwa umasikini wetu na trend yetu ya maendeleo uwezo huo tutakuwa nao? ukizingatia hao wawekezaji watafanya ujanja wa kuweka heavy investiments kama irrigation schems ili kulinda right yao ya occupancy na siyo kusaidia wakulima wetu huku wakiuza mazao at the high price ambapo sisi automatically tutakuwa excluded kutokana na kuwa tuko income poor so justification nyingine ya kuuza kwenye world market kutokana na sera ya free market. Any way hii siyo indepth economic analysis lakini even at that the conclusion will be within the marginal error.

So any move of leasing the land ni muhimu kufikiria mara mbili nakuwa na tahadhari za kutosha. Inawezekana wakubwa wanafikiria kufanya hivyo kwa dhamira njema lakini je wamezingatia ushauri wa wataalam? Na kama ndivyo kwanini isiwekwe publicly in a simple way kwa watu wote waone prons and cons and what are the safety nets created for the victims? Ili wachague kwa hiari yao huku wakijua outcomes?
 
Mkandara,
Tatizo si Saudia (as far as I am concerned). Tatizo kwangu ni ukosefu wa sera katika serikali yetu. Tunajua Saudia kuna soko la mchele na ngano. Tunajua tuna ardhi nzuri na pia tunajua kuwa asilimia 80 ya raia wetu ni wakulima. Tuna shida gani ya kulishika hilo soko la Saudia kwa kuongeza uzalishaji wa mpunga na ngano badala ya kuwaalika Wasaudia waje wajilimie wenyewe kwenye ardhi yetu.? Mimi ningefurahi sana kama Mwungana angerudi na kuwaambia wakulima wetu wa mchele pale Kyela kuwa nimewapatieni soko la uhakika, ongezeni uzalishaji wa mpunga ili tuweze kuuuza mpunga wetu Saudia na kuliongezea taifa kipato. Kwa mtaji huo hata mimi ningefikiria kutafuta shamba Kyela. Huo ndio mtazamo wangu. As far as kuwa na nyumba Marekani, ninahenya na mortgage kwa miaka 25 ijayo. Lakini kuwapatia wageni wowote ardhi ilhali watu wetu wanaendelea kuteseka na umasikini ni uhaini wa hali ya juu kwa upande wa viongozi wetu. Hii si kwa Saudia peke yake, bali hata Holland ambao wanalima maua kule Arusha au Sweden ambayo ilitaka mashamba ya jathropa kabla ya bei ya mafuta kupungua.

Jasusi,
Nakupata vizuri unapozungumzia swala zima la Policy yetu, inatulinda vipi. Lakini mimi kinachonishinda ni kwamba nchi yetu imekuwa iki lease ardhi toka tumeuvamia Ubepari na haikuwa issue. Mwenyewe umesema Wa Holland wanalima maua kule Arusha na hakuna issue iliyo au inayozungumziwa zaidi ya kufurahia mauzo hayo kuongeza GDP ya Taifa, hali sehemu kubwa ya pato la maua hayo inachukuliwa na wageni hao hao..Hayo maua hata kuyala hatuyali acha chakula!

Sasa nachopinga mimi ni zaidi ya Policy ni mwamko wetu sisi ktk ulinzi wa mali yetu kama vile kuna watu wanaoruhusiwa kukodishiwa ardhi kwa sababu ni Wazungu na hakuna mtu anauliza mkataba wao upo vipi?.. Kisheria leasing ya ardhi Tanzania ina maximum ya miaka 99 sote tunafahamu hilo kwa hiyo sidhani kama hili ni tatizo, Wazungu wame lease kwa maswala kama haya miaka 99 na hatuoni ubaya wala kulizungumzia..kwani sii tatizo isipokuwa tunaposikia Waarabu (hasa nchi za Kiislaam) wanapokuja nchini kuwekesha au hata kutoa msaada ni issue kubwa sana.
Hii mentality ndio inanishinda kwa sababu ubaguzi wetu umefikia mahala ambapo inabidi tuanze kujitazama sisi wenyewe.

NDIVYO TULIVYO ni neno linalotokana na ufukara wa hali na Mali, akili ya kushikiwa yaani mawazo yetu yanasukumwa na imani ya mafundisho tuliyopewa na wageni kujenga roho za kikorosho..Dini zimekuwa uwanja wa majungu, chuki na Ushetani amekuwa binadamu mwingne! maana ya dini imeondoka kabisa badala ya watu kumcha Mwenyezi Mungu, dini zimekuwa tofauti baina yetu kama vile wazungu walivyofundishwa kututenga sisi weusi..

Kila issue kubwa inayobebwa na Watanzania ina mikondo miwili, kwanza ni ROHO MBAYA.. Roho mbaya inajenga chuki kwenye vyama, chuki ipo kwenye Makabila, Chuki ipo kwenye Jinsia, Chuki ipo kwenye rangi zetu na zaidi ya yote haya Chuki imeingia hata kwetu sisi binafsi as individuals yaani unaweza mchukia mtu kwa kumtazama tu..Kilichotangulia yote chuki kubwa ipo ktk imani ya DINI..
Utafikiri kama vile Ardhi yetu ni sawa na mtoto wetu wa Kike... Mume atakaye ozwa ni yule tu atakayekubalika na wazazi kwa masharti yanayokidhi roho zetu na sio mahitaji ya binti yetu.
Lakini yote haya yanatokana na kisa kikubwa kuliko yote UTUMWA.. sisi ni watumwa wa mawazo (elimu zetu) kwa hiyo kila kinachozungumzwa na wageni ndicho somo kubwa la maisha yetu..Bado kabisa hatujaondokana na Utumwa wa akili...

Kwa nini nimeirudisha issue hii ni kwa sababu tumewahi kuzungumzia sana wakati Makaburu walipofukuzwa Zimbabwe, walikuwa wakiitupia macho Tanzania... Nakumbuka vizuri mada ile nilisimama peke yangu na baadhi wachache waliokuwa wakitetea. Niakitwa mjamaa na kuwa na chuki nina Wazungu..Mkuu tunavyozungumza tayari wapo makaburu ambao wameingia nchini!

Nikasema tatizo kubwa la wananchi wa Zimbabwe sio kwamba hawana Ujuzi wa kulima zabibu, mahindi na vyakula vinginevyo kwa sababu ndio asili yao, hawa ni Wabantu na Mzungu Kaburu kawekesha kwenye kilimo kwa sababu mbili kubwa Ardhi (location) na manpower!..Kwa hiyo Wazimbabwe ni asili yao Kulima, lakini hawana elimu wala asili ya Biashara ambayo Mtaji (Capitalism) unatakiwa kuweza kukuza kilimo hicho hicho kuweza kukutajirisha zaidi.

Kwa hiyo utakuta kwamba wananchi wa Zimbabwe wameshindwa kulima kwa sababu serikali yao bado inafikiria Kijamaa au wamevamia Ubebari bila kufahamu kwamba Mtaji ndio siri kubwa ya maendeleo ktk Biashara yoyote..Serikali ya Mugabe alishindwa kuwatajirisha wananchi, na sisi kama utakumbuka tulichukua mashamba ya mkoloni tukashindwa kuyaendeleza kwa sababu hatukuwa na mfumo bora (Capitalism)unaolingana na uwekeshaji ule..Hivyo utekelezaji wa sera nzima ya kilimo ilikufa..
Kwa hiyo leo hii serikali yetu inapozidi kushindwa kuwatajirisha wananchi wake kwa fikra kwamba mtaji sio swlaa la serikali.. Serikali ikupe ardhi kisha tena ikupe na mtaji?..Uliona wapi haya ndio mawazo ya kina Mugabe na nchi zote za kiafrika ambazo Ubepari kwetu ni mfumo tunaousoma ktk vitabu.. Hivyo urahisi kwao ni kuwapa wageni ambao wana mfumo tayari unaweza kuwatajirisha kwa mikopo toka benki zao.. Leo hii benki zinaposhindwa kutajirisha wananchi serikali zao zimesukuma fedha ndani kuzipa nguvu benki hizo... Mzunguko wa Ukopeshaji ukifa, Ubepari pia utakufa - hivyo siri ya Ubepari ni mikopo!

Nina hakika hao waarabu wanakuja wekesha, hawalimi wao lini mwarabu akakubali kukunja kanzu lake akaingia shamabani kulima Mpunga au ngano! Mkuu wangu msifanye mchezo na kazi hizi hata kidogo..Hata mashamba makubwa ya huku Canada na US kuna wakulima huagizwa kutoka visiwa vya Carribean huja fanya kazi kwa contract ya msimu..Ukitazama maisha yao na jinsi wanavyokuwa treated huwezi kuamini kwamba nchi hizi zinazojisifia zinaweza kuwadharirisha binadamu wengine kiasi hicho. Nenda Saudia kwenyewe tazama maisha ya Wahindi na WaPhillipino ambao wanafanya kazi kwa waarabu utalia mkuu wangu..

Pamoja na yote haya nachojaribu kusema mimi tusiwe wabaguzi, issue kubwa kwetu ni sababu gani serikali imeshindwa kuwatajirisha wananchi ktk Kilimo?.. Serikali imeshindwa kununu Matrekta na zana muhimu za kilimo ktk mfumo mzuri kama huu wa Ubepari badala yake tunaagiza wageni kufanya kazi ambayo asilimia 90 ya kazi za uzalishaji zinafanywa na wananchi hao hao walionyimwa mtaji..Soko la Arabuni lipo siku zote haikuhitaji Kikwete kwenda Saudia kufahamu hilo.. Uki surf ktk Google na kutafuta soko la kitu chochote utaweza kupata mashirika yanayohusika na uagizaji wa mali hizo.. Hata ukienda India mzalishaji mkubwa wa mchele wa Basmati (Pishori) unaoitwa Tilda ni Mhindi ambaye nyuma yake kuna Mwarabu..

Kwa hiyo wenzetu uwekezaji ktk Kilimo unakuwa na masharti magumu kama ni lazima Mwananchi/Wananchi awe na hisa zaidi ya 50 ili mwekezaji apatiwe kibali cha kuwekeza nchini. Unafanya hivyo sio kwa sababu unawazuia Wawekeshaji isipokuwa lengo zima la uwekeshaji sio kuona ardhi imelimwa isipokuwa ardhi hiyo inakuwa na manufaa kwa mwananchi...
Serikali inatakiwa kuwatajirisha wananchi wake ktk Kilimo na kama soko linazidi kuwa kubwa kuliko uwezo wa mwananchi huyo ndipo yeye anaweza kuuza hisa zake kwa waarabu, wazungu au watu wa makabila.. hivyo msukumo wa kujipanua unatokana na soko la kile unachozalishwa na sii uwezo wa mtaji wa mwarabu, mzungu au Mhindi....
 
Mkandara,
Kwa bahati mbaya sikuwepo enzi mnazungumzia suala la Kaburu na ardhi Afrika. Nakumbuka Mwinyi alipokwenda Afrika kusini kuaga mwaka 1985 aliwakaribisha Makaburu waje Tanzania. Tatizo la viongozi wetu ni kufikiria kuwa sisi hatuwezi. Wageni tu ndio wanaoweza. Nimesoma ripoti moja ya mkulima huko Mbeya ambaye sasa hivi anatengeneza shillingi millioni 100 kwa mwaka kwa kulima mchele, vitunguu, nyanya., nk na anasema kuna wakulima kama 200 katika kundi lake wenye kipato hicho. Na hawa waliwezeshwa kwa kupewa simple education na mhisani mmoja. Kwa hiyo uwezo wa kuwakwamua wakulima wetu upo. Sasa tungetumia mfano huo katika majimbo mengine hali ya maisha yetu ingebadilika sana na vijana hawatakuwa na sababu tena ya kukimbilia mijini kwa sababu kuna hela ya kutosha huko mashambani.
Tuwe waangalifu na ardhi yetu isije ikawa yale yale yaliyotokea katika ardhi ya madini.
Huo ndio mtizamo wangu.
 
Mkuu mwanakijiji,maneno matupu ndani ya jf hayavunji mufupa.

Wazo:
Toa t'shirt nyingine za jf zenye ujumbe USIUZE ARDHI YETU KWA SAUDIA-JK,zisambazwe home kama kawa ktk maduka mbalimbali,naam itasaidia na mkwere ataona haya.
 
Jasusi,
Nakupata vizuri unapozungumzia swala zima la Policy yetu, inatulinda vipi. Lakini mimi kinachonishinda ni kwamba nchi yetu imekuwa iki lease ardhi toka tumeuvamia Ubepari na haikuwa issue. Mwenyewe umesema Wa Holland wanalima maua kule Arusha na hakuna issue iliyo au inayozungumziwa zaidi ya kufurahia mauzo hayo kuongeza GDP ya Taifa, hali sehemu kubwa ya pato la maua hayo inachukuliwa na wageni hao hao..Hayo maua hata kuyala hatuyali acha chakula!

Sasa nachopinga mimi ni zaidi ya Policy ni mwamko wetu sisi ktk ulinzi wa mali yetu kama vile kuna watu wanaoruhusiwa kukodishiwa ardhi kwa sababu ni Wazungu na hakuna mtu anauliza mkataba wao upo vipi?.. Kisheria leasing ya ardhi Tanzania ina maximum ya miaka 99 sote tunafahamu hilo kwa hiyo sidhani kama hili ni tatizo, Wazungu wame lease kwa maswala kama haya miaka 99 na hatuoni ubaya wala kulizungumzia..kwani sii tatizo isipokuwa tunaposikia Waarabu (hasa nchi za Kiislaam) wanapokuja nchini kuwekesha au hata kutoa msaada ni issue kubwa sana.
Hii mentality ndio inanishinda kwa sababu ubaguzi wetu umefikia mahala ambapo inabidi tuanze kujitazama sisi wenyewe.

NDIVYO TULIVYO ni neno linalotokana na ufukara wa hali na Mali, akili ya kushikiwa yaani mawazo yetu yanasukumwa na imani ya mafundisho tuliyopewa na wageni kujenga roho za kikorosho..Dini zimekuwa uwanja wa majungu, chuki na Ushetani amekuwa binadamu mwingne! maana ya dini imeondoka kabisa badala ya watu kumcha Mwenyezi Mungu, dini zimekuwa tofauti baina yetu kama vile wazungu walivyofundishwa kututenga sisi weusi..

Kila issue kubwa inayobebwa na Watanzania ina mikondo miwili, kwanza ni ROHO MBAYA.. Roho mbaya inajenga chuki kwenye vyama, chuki ipo kwenye Makabila, Chuki ipo kwenye Jinsia, Chuki ipo kwenye rangi zetu na zaidi ya yote haya Chuki imeingia hata kwetu sisi binafsi as individuals yaani unaweza mchukia mtu kwa kumtazama tu..Kilichotangulia yote chuki kubwa ipo ktk imani ya DINI..
Utafikiri kama vile Ardhi yetu ni sawa na mtoto wetu wa Kike... Mume atakaye ozwa ni yule tu atakayekubalika na wazazi kwa masharti yanayokidhi roho zetu na sio mahitaji ya binti yetu.
Lakini yote haya yanatokana na kisa kikubwa kuliko yote UTUMWA.. sisi ni watumwa wa mawazo (elimu zetu) kwa hiyo kila kinachozungumzwa na wageni ndicho somo kubwa la maisha yetu..Bado kabisa hatujaondokana na Utumwa wa akili...

Kwa nini nimeirudisha issue hii ni kwa sababu tumewahi kuzungumzia sana wakati Makaburu walipofukuzwa Zimbabwe, walikuwa wakiitupia macho Tanzania... Nakumbuka vizuri mada ile nilisimama peke yangu na baadhi wachache waliokuwa wakitetea. Niakitwa mjamaa na kuwa na chuki nina Wazungu..Mkuu tunavyozungumza tayari wapo makaburu ambao wameingia nchini!

Nikasema tatizo kubwa la wananchi wa Zimbabwe sio kwamba hawana Ujuzi wa kulima zabibu, mahindi na vyakula vinginevyo kwa sababu ndio asili yao, hawa ni Wabantu na Mzungu Kaburu kawekesha kwenye kilimo kwa sababu mbili kubwa Ardhi (location) na manpower!..Kwa hiyo Wazimbabwe ni asili yao Kulima, lakini hawana elimu wala asili ya Biashara ambayo Mtaji (Capitalism) unatakiwa kuweza kukuza kilimo hicho hicho kuweza kukutajirisha zaidi.

Kwa hiyo utakuta kwamba wananchi wa Zimbabwe wameshindwa kulima kwa sababu serikali yao bado inafikiria Kijamaa au wamevamia Ubebari bila kufahamu kwamba Mtaji ndio siri kubwa ya maendeleo ktk Biashara yoyote..Serikali ya Mugabe alishindwa kuwatajirisha wananchi, na sisi kama utakumbuka tulichukua mashamba ya mkoloni tukashindwa kuyaendeleza kwa sababu hatukuwa na mfumo bora (Capitalism)unaolingana na uwekeshaji ule..Hivyo utekelezaji wa sera nzima ya kilimo ilikufa..
Kwa hiyo leo hii serikali yetu inapozidi kushindwa kuwatajirisha wananchi wake kwa fikra kwamba mtaji sio swlaa la serikali.. Serikali ikupe ardhi kisha tena ikupe na mtaji?..Uliona wapi haya ndio mawazo ya kina Mugabe na nchi zote za kiafrika ambazo Ubepari kwetu ni mfumo tunaousoma ktk vitabu.. Hivyo urahisi kwao ni kuwapa wageni ambao wana mfumo tayari unaweza kuwatajirisha kwa mikopo toka benki zao.. Leo hii benki zinaposhindwa kutajirisha wananchi serikali zao zimesukuma fedha ndani kuzipa nguvu benki hizo... Mzunguko wa Ukopeshaji ukifa, Ubepari pia utakufa - hivyo siri ya Ubepari ni mikopo!

Nina hakika hao waarabu wanakuja wekesha, hawalimi wao lini mwarabu akakubali kukunja kanzu lake akaingia shamabani kulima Mpunga au ngano! Mkuu wangu msifanye mchezo na kazi hizi hata kidogo..Hata mashamba makubwa ya huku Canada na US kuna wakulima huagizwa kutoka visiwa vya Carribean huja fanya kazi kwa contract ya msimu..Ukitazama maisha yao na jinsi wanavyokuwa treated huwezi kuamini kwamba nchi hizi zinazojisifia zinaweza kuwadharirisha binadamu wengine kiasi hicho. Nenda Saudia kwenyewe tazama maisha ya Wahindi na WaPhillipino ambao wanafanya kazi kwa waarabu utalia mkuu wangu..

Pamoja na yote haya nachojaribu kusema mimi tusiwe wabaguzi, issue kubwa kwetu ni sababu gani serikali imeshindwa kuwatajirisha wananchi ktk Kilimo?.. Serikali imeshindwa kununu Matrekta na zana muhimu za kilimo ktk mfumo mzuri kama huu wa Ubepari badala yake tunaagiza wageni kufanya kazi ambayo asilimia 90 ya kazi za uzalishaji zinafanywa na wananchi hao hao walionyimwa mtaji..Soko la Arabuni lipo siku zote haikuhitaji Kikwete kwenda Saudia kufahamu hilo.. Uki surf ktk Google na kutafuta soko la kitu chochote utaweza kupata mashirika yanayohusika na uagizaji wa mali hizo.. Hata ukienda India mzalishaji mkubwa wa mchele wa Basmati (Pishori) unaoitwa Tilda ni Mhindi ambaye nyuma yake kuna Mwarabu..

Kwa hiyo wenzetu uwekezaji ktk Kilimo unakuwa na masharti magumu kama ni lazima Mwananchi/Wananchi awe na hisa zaidi ya 50 ili mwekezaji apatiwe kibali cha kuwekeza nchini. Unafanya hivyo sio kwa sababu unawazuia Wawekeshaji isipokuwa lengo zima la uwekeshaji sio kuona ardhi imelimwa isipokuwa ardhi hiyo inakuwa na manufaa kwa mwananchi...
Serikali inatakiwa kuwatajirisha wananchi wake ktk Kilimo na kama soko linazidi kuwa kubwa kuliko uwezo wa mwananchi huyo ndipo yeye anaweza kuuza hisa zake kwa waarabu, wazungu au watu wa makabila.. hivyo msukumo wa kujipanua unatokana na soko la kile unachozalisha na sii uwezo wa mwarabu, mzungu au Mhindi....

Mkandara:

Watanzania wengi sisi washamba. Na kuna watu wanadiriki kusema kuwa watu weusi ni kama Crabs. Crabs ukiwaweka kwenye kapu, kila crab anayejaribu ku-escape anavutwa chini na crab mwingine na matokeo yake hakuna anayetoka.

Tukirudi kwenye kuna data ambazo watanzania wengi hawana. Mojawapo ni kuwa nchi nyingi za West hazina saving. Unapomchukua investor kutoka West ni lazima akakope benki kwanza na baadaye aje kuweka kwetu.

Kipindi hicho-hicho kuna nchi kama Saudi Arabia, China, UAE na India zimeweza kuweka kwa kiasi kikubwa kuweka reserve ya pesa za kutosha na wanatafuta wapi pa kuziweka.

mSaudi atakapokuja kuwekeza ataleta mtaji na wataalamu watatoka pande zote za dunia.

Chukua mtaji wa Dubai World Port. Emirates wame-invest money lakini wafanyakazi wengi ni kutoka Marekani, India na sehemu zingine.
 
Hawa watu kwa vyovyote watafanya "mechanized agriculture". Uwekezaji utagharimu pesa nyingi. Hivyo, bei ya mazao watakayoyazalisha itapangwa in such a way to guarantee return (well above the average cost). Kwa kuwa gharama za kuzalisha ni kubwa, bei lazima itakuwa kubwa. Je, watanzania wataiweza bei ya hawa jamaa?

Pili, hawa jamaa wanachotaka ni ardhi ya kuzalisha chakula kwa ajili yao. Hilo ndilo hitaji lao na si vinginevyo. Jukumu letu [wenye ardhi] ni kuangalia ni namna tutanufaika na huu mpango i.e. cost-benefit analysis. Tukiona faida ni kubwa kuliko hasara, then tunaukubali mpango. Otherwise, tunakataa. This is how it should work. Tukifanya mahesabu yetu vizuri, I am sure we stand to benefit. Remember, they have oil! They have money! All we need is a good economist to calculate compensation.

Surely there is no benefit out of this deal leasing the land for 99 years man. Jeuri ya nchi yoyote ile duniani ni kujihakikishia chakula cha kutosha nchini. Kama wanapewa machamba basi sharti soko liwe Tanzania. Kuhusu bei wala usiwe na wasiwasi watashindana na soko lililopo so hakutakuwa na bei za ajabu tena naforecast bei zitashuka zaidi ya hapo tulipo. Hatahivyo naungana na mdau mmoja hapo juu kuwakodisha mashamba for 99 years sio feasible. Pili kunatakiwa kuwe na monitoring ya nini watalima na nini hawataruhusiwa kulima mfano Jatropha trees inayotumika kuzalisha biofuel kwa kuwa inaexhaust udongo.
 
Back
Top Bottom