Mkandara,
Tatizo si Saudia (as far as I am concerned). Tatizo kwangu ni ukosefu wa sera katika serikali yetu. Tunajua Saudia kuna soko la mchele na ngano. Tunajua tuna ardhi nzuri na pia tunajua kuwa asilimia 80 ya raia wetu ni wakulima. Tuna shida gani ya kulishika hilo soko la Saudia kwa kuongeza uzalishaji wa mpunga na ngano badala ya kuwaalika Wasaudia waje wajilimie wenyewe kwenye ardhi yetu.? Mimi ningefurahi sana kama Mwungana angerudi na kuwaambia wakulima wetu wa mchele pale Kyela kuwa nimewapatieni soko la uhakika, ongezeni uzalishaji wa mpunga ili tuweze kuuuza mpunga wetu Saudia na kuliongezea taifa kipato. Kwa mtaji huo hata mimi ningefikiria kutafuta shamba Kyela. Huo ndio mtazamo wangu. As far as kuwa na nyumba Marekani, ninahenya na mortgage kwa miaka 25 ijayo. Lakini kuwapatia wageni wowote ardhi ilhali watu wetu wanaendelea kuteseka na umasikini ni uhaini wa hali ya juu kwa upande wa viongozi wetu. Hii si kwa Saudia peke yake, bali hata Holland ambao wanalima maua kule Arusha au Sweden ambayo ilitaka mashamba ya jathropa kabla ya bei ya mafuta kupungua.
Jasusi,
Nakupata vizuri unapozungumzia swala zima la Policy yetu, inatulinda vipi. Lakini mimi kinachonishinda ni kwamba nchi yetu imekuwa iki lease ardhi toka tumeuvamia Ubepari na haikuwa issue. Mwenyewe umesema Wa Holland wanalima maua kule Arusha na hakuna issue iliyo au inayozungumziwa zaidi ya kufurahia mauzo hayo kuongeza GDP ya Taifa, hali sehemu kubwa ya pato la maua hayo inachukuliwa na wageni hao hao..Hayo maua hata kuyala hatuyali acha chakula!
Sasa nachopinga mimi ni zaidi ya Policy ni mwamko wetu sisi ktk ulinzi wa mali yetu kama vile kuna watu wanaoruhusiwa kukodishiwa ardhi kwa sababu ni Wazungu na hakuna mtu anauliza mkataba wao upo vipi?.. Kisheria leasing ya ardhi Tanzania ina maximum ya miaka 99 sote tunafahamu hilo kwa hiyo sidhani kama hili ni tatizo, Wazungu wame lease kwa maswala kama haya miaka 99 na hatuoni ubaya wala kulizungumzia..kwani sii tatizo isipokuwa tunaposikia Waarabu (hasa nchi za Kiislaam) wanapokuja nchini kuwekesha au hata kutoa msaada ni issue kubwa sana.
Hii mentality ndio inanishinda kwa sababu ubaguzi wetu umefikia mahala ambapo inabidi tuanze kujitazama sisi wenyewe.
NDIVYO TULIVYO ni neno linalotokana na ufukara wa hali na Mali, akili ya kushikiwa yaani mawazo yetu yanasukumwa na imani ya mafundisho tuliyopewa na wageni kujenga roho za kikorosho..Dini zimekuwa uwanja wa majungu, chuki na Ushetani amekuwa binadamu mwingne! maana ya dini imeondoka kabisa badala ya watu kumcha Mwenyezi Mungu, dini zimekuwa tofauti baina yetu kama vile wazungu walivyofundishwa kututenga sisi weusi..
Kila issue kubwa inayobebwa na Watanzania ina mikondo miwili, kwanza ni ROHO MBAYA.. Roho mbaya inajenga chuki kwenye vyama, chuki ipo kwenye Makabila, Chuki ipo kwenye Jinsia, Chuki ipo kwenye rangi zetu na zaidi ya yote haya Chuki imeingia hata kwetu sisi binafsi as individuals yaani unaweza mchukia mtu kwa kumtazama tu..Kilichotangulia yote chuki kubwa ipo ktk imani ya DINI..
Utafikiri kama vile Ardhi yetu ni sawa na mtoto wetu wa Kike... Mume atakaye ozwa ni yule tu atakayekubalika na wazazi kwa masharti yanayokidhi roho zetu na sio mahitaji ya binti yetu.
Lakini yote haya yanatokana na kisa kikubwa kuliko yote UTUMWA.. sisi ni watumwa wa mawazo (elimu zetu) kwa hiyo kila kinachozungumzwa na wageni ndicho somo kubwa la maisha yetu..Bado kabisa hatujaondokana na Utumwa wa akili...
Kwa nini nimeirudisha issue hii ni kwa sababu tumewahi kuzungumzia sana wakati Makaburu walipofukuzwa Zimbabwe, walikuwa wakiitupia macho Tanzania... Nakumbuka vizuri mada ile nilisimama peke yangu na baadhi wachache waliokuwa wakitetea. Niakitwa mjamaa na kuwa na chuki nina Wazungu..Mkuu tunavyozungumza tayari wapo makaburu ambao wameingia nchini!
Nikasema tatizo kubwa la wananchi wa Zimbabwe sio kwamba hawana Ujuzi wa kulima zabibu, mahindi na vyakula vinginevyo kwa sababu ndio asili yao, hawa ni Wabantu na Mzungu Kaburu kawekesha kwenye kilimo kwa sababu mbili kubwa Ardhi (location) na manpower!..Kwa hiyo Wazimbabwe ni asili yao Kulima, lakini hawana elimu wala asili ya Biashara ambayo Mtaji (Capitalism) unatakiwa kuweza kukuza kilimo hicho hicho kuweza kukutajirisha zaidi.
Kwa hiyo utakuta kwamba wananchi wa Zimbabwe wameshindwa kulima kwa sababu serikali yao bado inafikiria Kijamaa au wamevamia Ubebari bila kufahamu kwamba Mtaji ndio siri kubwa ya maendeleo ktk Biashara yoyote..Serikali ya Mugabe alishindwa kuwatajirisha wananchi, na sisi kama utakumbuka tulichukua mashamba ya mkoloni tukashindwa kuyaendeleza kwa sababu hatukuwa na mfumo bora (Capitalism)unaolingana na uwekeshaji ule..Hivyo utekelezaji wa sera nzima ya kilimo ilikufa..
Kwa hiyo leo hii serikali yetu inapozidi kushindwa kuwatajirisha wananchi wake kwa fikra kwamba mtaji sio swlaa la serikali.. Serikali ikupe ardhi kisha tena ikupe na mtaji?..Uliona wapi haya ndio mawazo ya kina Mugabe na nchi zote za kiafrika ambazo Ubepari kwetu ni mfumo tunaousoma ktk vitabu.. Hivyo urahisi kwao ni kuwapa wageni ambao wana mfumo tayari unaweza kuwatajirisha kwa mikopo toka benki zao.. Leo hii benki zinaposhindwa kutajirisha wananchi serikali zao zimesukuma fedha ndani kuzipa nguvu benki hizo... Mzunguko wa Ukopeshaji ukifa, Ubepari pia utakufa - hivyo siri ya Ubepari ni mikopo!
Nina hakika hao waarabu wanakuja wekesha, hawalimi wao lini mwarabu akakubali kukunja kanzu lake akaingia shamabani kulima Mpunga au ngano! Mkuu wangu msifanye mchezo na kazi hizi hata kidogo..Hata mashamba makubwa ya huku Canada na US kuna wakulima huagizwa kutoka visiwa vya Carribean huja fanya kazi kwa contract ya msimu..Ukitazama maisha yao na jinsi wanavyokuwa treated huwezi kuamini kwamba nchi hizi zinazojisifia zinaweza kuwadharirisha binadamu wengine kiasi hicho. Nenda Saudia kwenyewe tazama maisha ya Wahindi na WaPhillipino ambao wanafanya kazi kwa waarabu utalia mkuu wangu..
Pamoja na yote haya nachojaribu kusema mimi tusiwe wabaguzi, issue kubwa kwetu ni sababu gani serikali imeshindwa kuwatajirisha wananchi ktk Kilimo?.. Serikali imeshindwa kununu Matrekta na zana muhimu za kilimo ktk mfumo mzuri kama huu wa Ubepari badala yake tunaagiza wageni kufanya kazi ambayo asilimia 90 ya kazi za uzalishaji zinafanywa na wananchi hao hao walionyimwa mtaji..Soko la Arabuni lipo siku zote haikuhitaji Kikwete kwenda Saudia kufahamu hilo.. Uki surf ktk Google na kutafuta soko la kitu chochote utaweza kupata mashirika yanayohusika na uagizaji wa mali hizo.. Hata ukienda India mzalishaji mkubwa wa mchele wa Basmati (Pishori) unaoitwa Tilda ni Mhindi ambaye nyuma yake kuna Mwarabu..
Kwa hiyo wenzetu uwekezaji ktk Kilimo unakuwa na masharti magumu kama ni lazima Mwananchi/Wananchi awe na hisa zaidi ya 50 ili mwekezaji apatiwe kibali cha kuwekeza nchini. Unafanya hivyo sio kwa sababu unawazuia Wawekeshaji isipokuwa lengo zima la uwekeshaji sio kuona ardhi imelimwa isipokuwa ardhi hiyo inakuwa na manufaa kwa mwananchi...
Serikali inatakiwa kuwatajirisha wananchi wake ktk Kilimo na kama soko linazidi kuwa kubwa kuliko uwezo wa mwananchi huyo ndipo yeye anaweza kuuza hisa zake kwa waarabu, wazungu au watu wa makabila.. hivyo msukumo wa kujipanua unatokana na soko la kile unachozalishwa na sii uwezo wa mtaji wa mwarabu, mzungu au Mhindi....