Sauli ni mfano wa wamiliki wa mabasi waliofilisiwa na madereva fake

Sauli ni mfano wa wamiliki wa mabasi waliofilisiwa na madereva fake

Nadhani Abood ndio the GOAT wa mabasi yote nchini,miaka takribani 40,ascandinavia kavuma maika michache sana haizidi 20

Abood na shabiby wabunge hao weka pembeni au subiri mitano yao ikiisha.

Scandinavia ikitamba ilihusishwa na kina chumaye ikilamba wese bure BP.

Wako wapi fresh ya shamba, dar express, moretco, kauma, kaudo, uda.

Kwamba ni wajinga wenye mabasi yaliyovuma na leo hawapo?
 
Naona afadhali ya Malori

Nafuu ipo lakini yale yale.

Fika Moro uone, pale malori yakitoka nchi jirani matairi mapya hutolewa yakapachikwa vipara.

Bado spare huuzwa, zikabadilishwa, tingo akaendesha, yakachukua mizigo isiyokuwa accounted, wese likapigwa nyoka, nk.

Kwa ufupi mtanzania au mswahili usimpe investment akakuletee hela, labda uendeshe mwenyewe.
 
Mtanzania gani utampa investment ya mamilioni akakutafutie pesa kama wanavyoita wao?

Ukweli mchungu hakuna mwenye bus au Lori atatoboa.

Hata latra hilo wanajua.

Wote unaowaona ni just a matter of time.
Comment ya kibabe sana
 
Unaweza kuwa sahihi mkuu, ila tu kwa taarifa yako Marehemu Sauli alikuwa kishaagiza unit 6 za yutong. Sema mipango ya Mungu si ya mwanadamu. Aendelee kupumzika alipojiandalia.
Kwa mwendo wa madereva wake hizo yuton ni miezi SITA tuuu zingekufa!? Zote
 
Nafuu ipo lakini yale yale.

Fika Moro uone, pale malori yakitoka nchi jirani matairi mapya hutolewa yakapachikwa vipara.

Bado spare huuzwa, zikabadilishwa, tingo akaendesha, yakachukua mizigo isiyokuwa accounted, wese likapigwa nyoka, nk.

Kwa ufupi mtanzania au mswahili usimpe investment akakuletee hela, labda uendeshe mwenyewe.
Mbona lori za Blue coast zipo na kampuni inazidi kukua kila siku na mmiliki ni mswahili?
 
Mbona lori za Blue coast zipo na kampuni inazidi kukua kila siku na mmiliki ni mswahili?

Wapi ulipoona nimeandika tatizo mmiliki ni mswahili ndugu?

Nimekuwa wazi tatizo ni waswahili wanaokabidhiwa magari hayo Ili wakalete pesa.

Nimekuwa wazi angalia % ya zilizopo dhidi ya zilizokufa.

Katika chache zilizopo nyingi zake ni za wana siasa au wenye nazo Wana biashara zingine.

Kama konda na dereva wanatokomea na mapato yao kama wanavyoona inafaa, polisi nao na viatu vyao, bado latra na zao lukuki.

Wenye malori ziibiwe tokea tairi, spare hadi biashara ya mizigo bubu.

Kampuni ipi yako wewe ya namna hii itadumu ndugu?
 
Back
Top Bottom