SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Utendaji wao upo kwenye mashaka au basi tu ni ukaidi wao ndio unapelekea kukomoana ?

Kama ni ukaidi pekee naona waendelee kufanya shughuli ndogo ndogo kama kutumbua majipu kama ni weledi / utendaji pia upo kwenye mashaka basi popote pale walipo wanyanganywe hata hio stethography na hizo scrubs haraka sana
 
Ndugu Hakuna injunction kwenye rulling and judgment. Injunction ni kuomba kuweka zuio kwa Jambo lililoamuriwa na chombo ambacho sio Cha mahakama, ili mahakama isikilize shauri Hilo. Refer kesi ya akina mdee.
Injunction inafanyika pale ambapo jambo linaendelea na bado halijatolewa maamuzi, means linatakiwa lizuiwe ili lisije kuathiri haki ya mtu hapo baadae baada ya maamuzi/judgement...linaweza fanywa au kuombwa ktk mahakama yoyote kutokana tu na Jambo lako linahusu nini, au hata ktk tribunal/mabaraza.

Concern yako Sasa: Vyombo ambavyo si mahakama Kama taasisi let say vyuo, vyama vya siasa, makanisa na agencies mbalimbali huwa zinafanya maamuzi kupitia kwa board au committee zao walizojiwekea,...Sasa ikitokea wamefanya maamuzi ambayo yameathiri haki ya mtu, mtu huyo ataenda mahakama kuu kwa ajili ya JUDICIAL REVIEW, kwenye judicial review hiyo ambayo inafanyika high court mtu anaweza akaomba order ya Mandamus, certiorari, injunction, prohibition n.k
 
Kuharibiana tu maisha, wazee wana roho mbaya sana...
Transcript ikiwa haijasainiwa hupewi hao walipewa kimakosa wameambiwa warudishe zisainiwe wakagoma kurudisha ni kosa, kwa hio kufutiwa ni haki yao maana ni watovu wa nidhamu
 
Mimi nilisomea huo Udokta? Usiniboe!
Uspanic Mkuu Thread Iko wazi ni St Francis ni kampasi nafikiri hii itakuwa ya Ifakara kama Niko sawa.Ila Sauti Wana vyuo vingi Vya Udaktari kikiwemo Bugando.Niko tayari kurekebishwa.
 
Administrative law hiyo! Hiyo seneti iliwaita wote hao 162 kwa notisi kwa ajili ya defence? Pamoja au mmoja mmoja,... principle za natural justice zimefuatwa? Kama vile Rule against bias, Audi alteram paterm, Nemo judex in causa sua? Au wameamka tu wakawafuatia huko huko...yasije yakatokea Kama ya SHABIBU MRUMA dhidi ya chuo cha Mzumbe, au Simon Manyaki dhidi ya IFM kesi zote hapa maamuzi ya board au committee yalipigwa chini... Evidence ya wito au notisi kwamba rudisha transcript iliwasilishwaje kwa wahusika na je kila mtu aliipata kwa wanafunzi 2015-2019. Any let us wait
 
Kuna kitu kimetokea kati ya 2015 -2019.

SAUT wawe wazi tu lakini si kuzungurusha maisha ya watu.
 
Transcript ikiwa haijasainiwa hupewi hao walipewa kimakosa wameambiwa warudishe zisainiwe wakagoma kurudisha ni kosa, kwa hio kufutiwa ni haki yao maana ni watovu wa nidhamu
kwa hiyo na kichwani kumefutwa,sio madaktari tena?
 
Sasa unafutaje ujuzi wao,kama mtu amekuwa anapractise udokta kwa muda wote huo,ukifuta degree yake,ujuzi wake unapotea?
Hizi ni siasa tu,ni njia ya kulazimisha malipo,ni Sawa na kuzuia cheti mpaka mtu amalizie ada
 
Nadhani Kuna kitu SAUT wanaficha. Inawezekana IT wao alisaidia baadhi ya watu kwa Siri bila kujulikana.
Ndio ilikuwa kawaida ya IT wa pale ingawa waliokuwa wanafanya hivyo walifutwa kazi. Mdogo wangu katoka Dip hapo mwaka 2021, probably walikuwa wanafanya hivyo 2020 kurudi nyuma na ukitazama hiki chuo kimewafutia hao wa 2019. Seneti nzima sio wapumbavu wakae vikao miezi na miezi watoe maamuzi ya kiwendawazimu.

Pande zote mbili zina makosa
 
Hao wasiotaka kurudisha transcript hawajagoma tu bila sababu. Na hao seneti hawajafuta vyeti vyao bila sababu, maprof wazima hawawezi kaa vikao nenda rudi wakafuta vyeti. Wakati huo daktari anayejiamini hawezi kaa miaka mitatu anaombwa arudishe transcript akagoma wakati mtu yeyote aliyechukua cheti cha chuo anatakiwa ajue hiyo ni mali ya chuo.

Lazima kuna kitu hakitajwi hapa kwenye taarifa. Hicho kitu ni cha kuchafua jina la chuo na sifa za hao madaktari. Na pande zote wanajua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…