SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

SAUT yafuta degree za Madaktari wa Afya 162 waliohitimu Chuo cha Mt. Francis

Kwenye hii inshu bado kuna vitu hatuvijui.

SAUT wenyewe hawajasema ilikuwaje watu hao wakapewa Shahada bila idhini ya Seneti.

Pia hatujasikia upande wa Pili wa hao waliokuwa Madaktari 162.

Ni Jukumu la Waandishi wa Habari Makini kutufunulia tusiyoyajua.
 
kwa nini waliwapa? tuanzie hapo
Tatizo la kutoa cheti kwa makosa/kimakosa linarekebishika (ni curable) Utaratibu wa kuzingatia katika kufanya Marekebisho ni pamoja na kuretrieve hizo Transcripts. Na hilo SAUT wamelifanya kwa muda mrefu sana lakini bila mafanikio - Madokta wakekaza shingo.

Hatua ya mwisho ndo hiyo ya kuzifuta juu kwa juu wewe unabaki na karatasi lisilo na thamani i.e. halitambuliwi kisheria. Endapo Hawatafikia Muafaka, bado ni hatari kubwa zaidi kwani Waajiri (Serikali au Private Sector) watafuatiliwa kuhusu Ajira kwa Mujibu wa Qualifications. Wewe Utakuwa ni mmojawapo wa waathirka - Huna qualifications za Udaktari. Hapo utakuwa mgeni wa nani???

Lakini kwa nini kote huko?? Si urudishe karatasi la watu halafu mengine mtayajenga? Hakuna lisilowezekana chini ya hili jua. Nyie ni watu wazima -fanyeni mambo yenu ki-Utu uzima. Umeshafanya kazi kwa zaidi ya 6yrs na nina amini unao uzoefu wa kutosha kazini. Hili la karatasi linakushindaje?

Unaogopa nini?
 
Kwenye hii inshu bado kuna vitu hatuvijui.

SAUT wenyewe hawajasema ilikuwaje watu hao wakapewa Shahada bila idhini ya Seneti.

Pia hatujasikia upande wa Pili wa hao waliokuwa Madaktari 162.

Ni Jukumu la Waandishi wa Habari Makini kutufunulia tusiyoyajua.
Waliofutiwa wataingea na wanahabari

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Tatizo la kutoa cheti kwa makosa/kimakosa linarekebishika (ni curable) Utaratibu wa kuzingatia katika kufanya Marekebisho ni pamoja na kuretrieve hizo Transcripts. Na hilo SAUT wamelifanya kwa muda mrefu sana lakini bila mafanikio - Madokta wakekaza shingo. Hatua ya mwisho ndo hiyo ya kuzifuta juu kwa juu ww unabaki na karatasi lisilo na thamani i.e. halitambuliwi kisheria. Endapo Hawatafikia Muafaka, bado ni hatari kubwa zaidi kwani Waajiri (Serikali au Private Sector) watafuatiliwa kuhusu Ajira kwa Mujibu wa Qualifications. Wewe Utakuwa ni mmojawapo wa waathirka - Huna qualifications za Udaktari. Hapo utakuwa mgeni wa nani???
Lakini kwa nini kote huko?? Si urudishe karatasi la watu halafu mengine mtayajenga? Hakuna lisilowezekana chini ya hili jua. Nyie ni watu wazima -fanyeni mambo yenu ki-Utu uzima. Umeshafanya kazi kwa zaidi ya 6yrs na nina amini unao uzoefu wa kutosha kazini. Hili la karatasi linakushindaje?
Unaogopa nini?
Mbona kwa sasa hawahitaji hizo transcript maana tayari wamefuta shahada zao.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Aisee, tutashuhudia mengi sana mpaka mwaka huu uishe
 
Mimi sio mhusika .
Ila nimeishangaa sana hiyo move yao ki ukweli kuna kitu wanaficha,
Si wanaweza kushtakiwa?
 
Chuo kikuu cha St. Augustine kimebatilisha shahada ilizotoa kwa madaktari 162 waliohitimu chuo cha udaktari cha St. Franscis kuanzia mwaka 2015-2019.

St. Augustine imechapisha tangazo kwenye gazeti la Daily news ikitoa notisi kubatilisha shahada za wanafunzi hao 162 ambao inadai wamegoma kurejesha nyaraka ya matokeo(Transcripts) ambazo walipewa bila baraza la senete la chuo kuwa na taarifa na kuziidhinisha.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na mwenyekiti wa seneti ya chuo hicho, balozi Prof Costa Mahalu imesema maamuzi hayo yamefikiwa baada ya mkutano wa senet ilioketi mwezi wa pili.

===

Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) kimewafutia shahada Madaktari 162 waliohitimu Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha St Francis (SFUCHAS) kuanzia mwaka 2015-2019.

Notisi kwa Umma iliyochapishwa katika Gazeti la Daily mnamo Jumatatu (27 Machi, 2023), ilisema wahitimu 162 walikataa kimakusudi kurudisha nakala za masomo, 'Transcript' walizopewa bila ufahamu na uidhinishaji wa seneti ya chuo kikuu licha ya kukumbushwa kwa muda mrefu.

Taarifa hiyo iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa seneti ya SAUT Balozi Prof. Costa Mahalu inaeleza uamuzi wa kuondoa shahada hiyo umekuja baada ya kikao cha Seneti cha Chuo Kikuu kilichofanyika Februari mwaka huu.

"SAUT kupitia Seneti ya Chuo Kikuu katika Seneti yake ya 54 isiyo ya kawaida, mkutano uliofanyika tarehe 25 Februari 2023 katika chuo kikuu cha SAUT na kwa mujibu wa Kifungu cha 47(1) & (2) cha Sheria ya Vyuo Vikuu, Sheria Na. 7 ya 2005 ikisomwa pamoja na Vifungu. 6(3)(ii), 7,8 na Kanuni ya 29 (1) ya Mkataba wa SAUT GN. HAPANA. 580 ya 2020 ilifuta shahada walizopewa wahitimu 162 wa Madaktari wa Udaktari wa SFUCHAS kuanzia 2015 -2019,” inasomeka taarifa hiyo.

Source: Daily News
Kwanini walipewa bila baraza la seneti kuidhinisha na kwanini wanaadhibiwa kwa makosa na uzembe wa watu wengine?
 
tukiacha kila mtu afanye anavyofikiria kichwani mwake mambo hayataenda.taratibu ziko wazi fuata kuepuka usumbufu na kama unadhani degree ni kile tu kilichopo kichwani kazi kwako kama utatumia kichwa kuomba kazi.
Suala ni kuomba kazi, kutengeneza pesa na sio huduma husika kwa jamii inayomuhitaji daktari, Ila wakigoma kwamba maslahi ni madogo inabadilika kuwa udaktari ni wito.
 
Kwa hiyo muda wote huo wameendelea kutumia transcript zisizoidhinishwa? Kama wametunukiwa shahada bila kukamilisha vigezo muhimu, hilo ni kosa la nani?
 
Mbona kwa sasa hawahitaji hizo transcript maana tayari wamefuta shahada zao.

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Dah! Hapo sijui itakuwaje tena wakiingia hatua ya kuwafuatilia Waajiri wao (makazini kwao) kupitia kwa Chama cha Madaktari Tanzania. Iko hatari ya kuwadidimiza madokta 162. Inasikitisha.
 
Msichokijua ni kwamba degree ni mali ya chuo. Vikao vyenye mamlaka vinaweza kukuvua degree yakona ukabaki na elimu ya form six tu
Cheti cha degree ni mali ya Chuo. Elimu uliyoipata sio mali ya chuo. Kwa shahada hizi zisizohitaji sana kutoa cheti ili ufanye kazi, vyeti unasahau vilipo au vinavyofanana.
 
Madaktari warudishe Transcript zikaidhinishwe wanaogopa nini kama ni halisi ? Waache longolongo.
 
Mimi sio mhusika .
Ila nimeishangaa sana hiyo move yao ki ukweli kuna kitu wanaficha ,
Si wanaweza kushtakiwa ?
Ndio kabisa. Inasikitisha sana sana. Yaani unaweza kufananisha na Mpishi(SAUT) anayeleta chakula mezani ambacho hakijaiva eti watu (watu Wagonjwa/waTz n.k.) wale ili wapate afya na nguvu za kulitumikia Taifa hili. Huo ni Uhujumu wa Afya na Mustakabali wa Uhai wa wananchi - Uhalifu dhidi ya Usalama wa Uhai wa Binadamu. Unamwidhinishaje (Unamkingia kifua)daktari fake aajiriwe ili akatoe Huduma kwa wananchi???

Halafu unapoona siri inafichuka unaanza kudai Transcripts ulizoidhinisha (SAUT) ukiwa na akili timamu na bila kushinikizwa(Vijana madokta) wanasita kuvirudisha na chap-chap unafuta Shahada/vyeti vyao. Kwa nini Usiwajibike au Uwajibishwe wewe(SAUT)?? Lakini nilishauri kama watu wazima, kaeni myajenge. Mbona nyumba mnayojenga ni moja ya nini kugombania fito?
 
Back
Top Bottom