Sauti ya wengi sio sauti ya Mungu. Huu msemo ni kuchanganya dini na siasa

Sauti ya wengi sio sauti ya Mungu. Huu msemo ni kuchanganya dini na siasa

kuna msemo wa kirumi Vox Populi Vox dei ( Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu).

Huu msemo ni sahihi kisiasa sio kidini au kiimani. Wanasiasa walitumia huu msemo kujihalalishia mambo yao hata kinyume cha Mungu na wengine ilikula kwao. Sasa ni aibu kwa kauli hii kusikika kwa watu wa dini. Ibaki kutumika katika mimbari ya kisiasa sio dinini.

Ushahidi
Nebukadneza Sauti ya wengi ilimjaza na akajiona mungu. Mungu alimpa adhabu ya kuishi porini na wanyama miaka saba hadi kiburi kiliposhuka.

Sauti ya wengi ndio ilimkataa Samweli aloyetumwa na Mungu, na kutaka waisrael watawaliwe kama mataifa mengine kisiasa.

Sauti ya Wengi ingekuwa ya Mungu, basi Nuhu na familia yake ndio wangekufa kwa mafuriko huku wengi wakiokolewa na safina.

Sauti ya wengi ya kumsifu Herode ilimsabajishia apigwe na chango akafia kwenye mimbari za kisiasa huku waliomsifu wamemkimbia.

Wengi waliwahi kusema afunguliwe jambazi Baraba na asurubiwe Yesu Yusuph aliyewafufulia watoto wao na kuwatoa mapepo yaliyowatesa.

Sauti ya wengi ni sauti ya hao wengi sio lazima iwe sauti ya Mungu. Linaweza kuwa kundi la wengi waliopotoshwa au wenye maslahi jifichi kwa kumpakazia Mungu kuwa sauti zao ni sauti yake.

Ni hayo tu waungwana.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki afrika kusini mwa jangwa la sahara.
Uko sawa ndugu, hawa Roman wameonyesha kupingana kabisa na Biblia, Wajifunue wazi tuwaone rangi zao halisi wasitumie mwamvuli wa dini.
 
Ukubali usikubali, haiwezi kubadilisha chochote. Tamko limeshatolewa, na ukweli umeliweka huru Kanisa la Mungu.
 
SAUTI YA WENGI KIGEZO CHA KUWA SAUTI YA MUNGU, HASA KATIKA SIASA

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Imezuka kasumba moja ya ajabuajabu ambayo sio Sahihi, yaani sio kweli. Yakwamba Sauti ya Wengi ndio Sauti ya Mungu. Yaani Watu wengi wakiamua Jambo Fulani basi uamuzi wao ndio uamuzi wa Mungu, na wakisema Jambo Fulani basi Mungu Kasema. Huo ni Uongo mkubwa. Ni upotoshaji unaofanywa kimakusudi.

Sauti ya Mungu haipimwi na wingi wa midomo ya Watu. Kuna vipimo vinavyoonyesha Sauti Hii NI Sauti ya Mungu. Vipimo au vigezo ni kama ifuatavyo;

1. HAKI

Sauti ya Mungu lazima izingatie Haki. Bila kujali yupo au hayupo atakayeisema au kuitenda.
Hata awepo mtu ambaye atasema lakini akapingwa na watu elfu moja na moja bado. Hao Watu elfu moja na moja Sauti zao haziwezi kuwa Sauti ya Mungu ikiwa ni Sauti isiyo ya Haki.

2. UKWELI
Ukweli hauna demokrasia kwamba wengi wape. Ukweli ni ukweli hata atakayeusema awe ni mtu mmoja au asiwepo. Sauti ya Mungu lazima iwe ni Kweli. Mtu yeyote anayesema ukweli ujue hiyo ni Sauti ya Mungu.
Ukweli hauna ubinafsi, ukweli ni sehemu ya Haki na upendo.

3. UPENDO
Sauti ya Mungu ni Sauti yenye upendo. Kujali wengine. Kuwapenda wengine kama unavyojipenda. Sauti ya Wengi haimaanishi ndio Sauti ya Mungu. Watu wengi ni wabinafsi, wengi husema mambo Kwa kuvutia kwao. Ni nadra Sana Kwa Watu kutokuwa na ubinafsi.
Kwa nature ya binadamu wengi Sauti zao haziwezi kuwa Sauti za Mungu.

4. AKILI NA MAARIFA
Sauti ya Mungu ni lazima iwe na Akili na maarifa ndani yake. Haiwezi kuwa ya Watu wengi Kwa sababu wote tunakiri kuwa ni wachache ndio wanamcha Mungu. Kwa sababu kumcha Bwana Mungu aliyekuumba ndio chanzo cha maarifa/ Akili. Sauti ya Mungu inakaa katika midomo ya watu waadilifu, wacha Mungu, Watu wenye upeo Mkubwa wa KUFIKIRI Kwa sababu huwezi kuwa na Akili na maarifa kama humtii na kumcha Yule aliyekuumba ambaye ndiye mwenye maarifa yote.

Sauti ya Wengi haiwezi kuwa Sauti ya Mungu Kwa sababu;
1. Binadamu wengi sio waadilifu
2. Watu wengi ni wabinafsi. Hufanya kila Jambo Kwa kujiangalia wao wenyewe bila kujali nafasi za Wengine.
3. Watu wengi hupenda kuwa Bora kuliko wengine. Kiburi.
4. Watu wengi hawapendi Mafanikio ya wengine. Ni wachache wanaopenda Mafanikio ya wengine.
5. Watu wengi ni Wanafiki. Sio wakweli. Huweza Kuunga mkono kishabiki au Kwa sababu aliyesema ni ndugu au mzazi au kabila lake au dini yake licha ya kujua kuwa Jambo Hilo sio sahihi.

Vipo visa ambavyo vinaonyesha kuwa sauti ya Wengi sio Sauti ya Mungu Kwa sababu mawazo ya Mungu na macho ya Mungu sio kama ya wanadamu. Mifano michache hasa ya kisiasa;

1. Mungu alimchagua Daudi kuwa Mfalme lakini Watu wengi hawakufikiri kuwa Daudi angeweza kuwa Mfalme. Kuanzia Baba na Ndugu zake mpaka Nabii Samweli mwenyewe alishangaa kuona Daudi amechaguliwa na Mungu. Mungu akasema, yeye haangalii mwonekano wa MTU kama wanadamu wengi wanavyofanya Bali hutazama Nafsi ya mtu(mioyo ya Watu).

2. Joshua na Kalebu Dhidi ya Wapelelezi Kumi
Wakati Sauti ya Wapelelezi kumi Kati ya kumi na Mbili waliotumwa kuipeleleza Yeriko, wakisema nchi Ile ya ahadi haifai na wakatoa sababu zao ambazo nyingi ni za msingi. Lakini Wapelelezi Wawili ambao ni Joshua na Kalebu wao wakasema nchi Ile ni nzuri na inafaa. Na Ile ndio ilikuwa Sauti ya Mungu.
Ilikuwa ni Sauti ya Mungu Kwa sababu kuu moja, nayo ni kutii agizo la Mungu waliloambiwa kuwa watoke Misri utumwani kisha waende Canaan. Kumtii Mungu ni chanzo cha maarifa/Akili. Na hicho ni kigezo cha Sauti ya Mungu. Mungu akiagiza Jambo Fulani anachotaka NI utii wako.

3. Sauti ya waisrael wengi waliamua kukataa kuongozwa na Mungu, yaani serikali Yao walitaka iongozwe na wafalme binadamu kama yalivyo mataifa mengine yanayowazunguka. Ile haikuwa Sauti ya Mungu. Matokeo yake tunayajua.

Sauti ya Watu wengi ndio iliyoharibu mifumo ya Haki za makundi ya Watu kama vile Watoto na Wanawake na kuwafanya wawe watumwa na vibaraka ndani ya Jamii. Sauti ya Watu wengi ndio iliyopendekeza Mila na desturi potofu kama vile ukeketaji, biashara ya kuuza Wanawake ambayo huitwa Mahari, na mifumo mibaya ambayo mpaka sasa hivi inaitesa jamii yetu.

Sauti ya Watu wengi ndio imehalalisha na kufanya viongozi wa dini na watawala kuabudiwa na kuonekana ni miungu Watu hata wakiwa wanakosea Jambo ambalo sio Sahihi.

Sauti ya Watu wengi ndio inapelekea Watu kununuliwa kwenye Siasa na kisha tunapata viongozi wa hovyo.
Sauti ya Watu wengi ndio chanzo cha unafiki na propaganda ya kuzuga Watu kuwa wanakubali au kukataa Jambo Fulani Kwa Kutumia Watu mashuhuri ambao wanawafuasi wengi.

Sauti ya Mungu haiangalii umashuhuri wa mtu au Watu Kwa sababu Kwa Mungu hakuna mtu mashuhuri zaidi ya Yule ambaye anamcha na kumuabudu yeye pekee.

Mungu alimuahidi Ibrahim kuwa Maarufu (kukuza jina lake, jina la Ibrahim) Kwa sababu ya utiifu wake. Mtu maarufu ni Yule anayemcha Mungu bila kujali Watu wengi wanamuonaje au wanasemaje.

Sauti ya Mungu haingalii heshima ya wanadamu wengi ambao wengi huheshimu watawala Kwa hofu(unafiki) na huwaheshimu matajiri kinafiki. Wakati Watu hao ni Maharamia, mafisadi na waovu. Watu waliomdharau Mungu Kwa kufanya maasi. Mungu mwenyewe anasema kuwa, Kwa kuwa umemdharau basi naye atakudharau. Sasa Watu wengi huwashangalia Watu waliodharauliwa na Mungu Muumbaji.

Nataka kusema, wingi wa Watu sio hoja. Hoja ni Haki, Upendo, Akili na Ukweli. Hizo ndio hoja.
Bila kujali atakayesema ni Nani, kama hoja hizo zitazingatiwa basi hiyo ni Sauti ya Mungu.

Na sio kisa MTU amevaa joho madhabahuji akiongea basi ndio iwe Sauti ya Mungu. Au mtu anatembea na ving'ora akisema ndio iwe Sauti ya Mungu. Haipo hivyo. Mungu hayupo kwenye ving'ora au mavazi ya kifalme au kikuhani. Wala hayupo katika wingi wa Watu. Mungu yupi katika kila mwenye HAKI, upendo, ukweli na Akili/maarifa.

Acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
kuna msemo wa kirumi Vox Populi Vox dei ( Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu).

Huu msemo ni sahihi kisiasa sio kidini au kiimani. Wanasiasa walitumia huu msemo kujihalalishia mambo yao hata kinyume cha Mungu na wengine ilikula kwao. Sasa ni aibu kwa kauli hii kusikika kwa watu wa dini. Ibaki kutumika katika mimbari ya kisiasa sio dinini.

Ushahidi
Nebukadneza Sauti ya wengi ilimjaza na akajiona mungu. Mungu alimpa adhabu ya kuishi porini na wanyama miaka saba hadi kiburi kiliposhuka.

Sauti ya wengi ndio ilimkataa Samweli aloyetumwa na Mungu, na kutaka waisrael watawaliwe kama mataifa mengine kisiasa.

Sauti ya Wengi ingekuwa ya Mungu, basi Nuhu na familia yake ndio wangekufa kwa mafuriko huku wengi wakiokolewa na safina.

Sauti ya wengi ya kumsifu Herode ilimsabajishia apigwe na chango akafia kwenye mimbari za kisiasa huku waliomsifu wamemkimbia.

Wengi waliwahi kusema afunguliwe jambazi Baraba na asurubiwe Yesu Yusuph aliyewafufulia watoto wao na kuwatoa mapepo yaliyowatesa.

Sauti ya wengi ni sauti ya hao wengi sio lazima iwe sauti ya Mungu. Linaweza kuwa kundi la wengi waliopotoshwa au wenye maslahi jifichi kwa kumpakazia Mungu kuwa sauti zao ni sauti yake.

Ni hayo tu waungwana.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki afrika kusini mwa jangwa la sahara.

Unaumia Ukiwa Wapi dogo!
Huwezi Ukamuwekea Mipaka Aliyekuumba!; Yeye ni Muasisi wa Mema Yoote Unayo Yaona na Usiyo Yaona!
 
Attachments

  • VID-20230910-WA0169.mp4
    30.8 MB
Back
Top Bottom