Sawa tumefika mbinguni. Je! tutakuwa tunaongea lugha Gani?

Sababu wewe umekata kupinga Kila kitu hivo ni ngumu
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwapo, asingeweza kupingika.

Ukiona inawezekana kufanyika mjadala kuhusu Mungu huyu kuwapo, ujue huo mjadala nao ni uthibitisho kwamba huyo Mungu hayupo.

Unaelewa hilo?
 
mie nadhani ukienda kwanza huko mbinguni kupitia kaburi, utajua tu namna ya kuongea na utakao kutana nao huko huko huko mbinguni. Ishi vizuri tu kwenye ulimwengu huu, na hazina yako njema utaikuta mbinguni 🐒
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwapo, asingeweza kupingika.

Ukiona inawezekana kufanyika mjadala kuhusu Mungu huyu kuwapo, ujue huo mjadala nao ni uthibitisho kwamba huyo Mungu hayupo.

Unaelewa hilo?
Unaweza kujikuta unakosa raha za peponi kizembe sana
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, angekuwapo, asingeweza kupingika.

Ukiona inawezekana kufanyika mjadala kuhusu Mungu huyu kuwapo, ujue huo mjadala nao ni uthibitisho kwamba huyo Mungu hayupo.

Unaelewa hilo?
NaChojua ndo nikuambiacho Mungu yupo mkuu
 
Kuongea kunaanza kaburini kwanza...
Unakutana na hamsha hamsa mpaka utajua kuingea lugha zote
ni kama ukienda china kule ndani ndani kabisaa vijijini, hawajui lugha nyingine zaidi ya kichina. ukiskia kiu na njaa ya haki lazima utajua tu namna ya kuwasilina nao ili upate maji na chakula, na matokeo yake utajikuta ni sehemu ya jamii ile 🐒
 
Mbinguni sio kama china mkuu
 
Tuta speak in tongue’s lkn tutakuwa tunaelewana
 
Hicho ni unachoamini. Hujakithibitisha bado, hivyo, hakijawa unachojua.

Naona hujui hata tofauti ya kujua na kuamini.

Thibitisha Mungu yupo.
Unanichanganya mkuu. Lengo lako hasa Nini niache kumuabudu Mungu wa mbinguni?
 
Unanichanganya mkuu. Lengo lako hasa Nini niache kumuabudu Mungu wa mbinguni?
Lengo langu ni kichambua mambo kupata ukweli.

Mpaka sasa habari za Mungu kuwapo ni za kiimani tu, hazina uthibitisho.

Imani hata uongo unaamini tu.

Ukweli mpaka uthibitishwe ndiyo unajulikana.

Thibitisha Mungu yupo, mbingu ipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…