#COVID19 Sayansi inazidi kutokomeza Corona

#COVID19 Sayansi inazidi kutokomeza Corona

Mkuu asante sana kwa ujumbe na ushauri mzuri ulioutoa kwa manufaa ya nchi yetu.

However, waisrael sio ndio waliotengeneza hiyo chanjo mkuu, tuwape credit wahusika nao ni wajeremani (kampuni ya kijeruman- BioNTech) wakishirikiana na kampuni ya kimataifa ya wamarekani - Pfizer.

historia fupi ya hii chanjo iko hivi

Mwezi wa kwanza 2020 hii kampuni ya kijerumani ilianza mchakato wa kutengeneza chanjo hii ikiita 'Project Lightspeed' Projekt Lichtgeschwindigkeit

Walitengeneza ainanyingi sana ya chanjo katika maabara yao ya Mainz. Kati ya hizo nyingi 20 ziliwakilishwa katika taasisi ya kinga ya ujerumani - Paul-Ehrlich-Institute.

Chanjo hii inayotumiwa na waisrael iliaanza kutumika (phase I/II) ujerumani kwa majaribio tarehe 23 mwezi wa 4 2020 ikifatiwa na US tarehe 4 mwezi wa tano 2020

Baada ya kuonyesha mafanikio ndio makampuni yakaanza kujitokeza kutoa pesa kuchangia.

Mwezi wa 6 2020 umoja wa ulaya ulitoa euro milioni 100, mwezi wa 9 2020 serekali ya ujerumani ilitoa euro milioni 375.

Much credit wapewe hawa wajerumani maana ndio waliofanya kazi kubwa sana haya makampuni kama Fosun na Pfizer ni madalali tu
 
Hivi ukubwa wa nchi ya Israel si ni sawa na ukubwa wa mkoa wa Mbeya?
 
Umenikumbusha kauli ya Baba Askofu Bagonza, “Tulipokuwa tuna Chuo Kikuu kimoja UDSM hatukuwa na wajinga wengi lakini sasa tuna vyuo vikuu vingi idadi ya wajinga nchini imeongezeka sana.”
Wewe na bagonza wako wote ni wapumbavu.
 
Ungeelezea hiyo jewish manag protocol ina utaratibu gani ili na wewe uingie katika historia ya kuokoa maisha ya wale watakaitumia wakihusi ama kuthibitisha kuambukizwa. Ingekuwa vyema zaidi ya kumuongelea JPM jambo ambalo haliwezi badilisha chochote
 
Kuna watu sijui wananufaika vipi na upotoshaji wanaofanya!
Unawezaje kesema Corona itaondoka yenyewe? Kwanini siyo magonjwa mengine lakini Corona?
Au Mungu anabagua magonjwa ya kuondoa kuwa hili limekuja kimakosa hivyo litaondoka litake lisitake?

Mwisho labda tujiulize: Hospitali na vituo vya utafiti wa magonjwa nini kazi yake kama Mungu anaweza kuondoa magonjwa haya yakaisha!!!
Naanza kupata picha kuwa watu wengi hutumia akili zao vema utotoni, ndiyo maana ule msemo wa Mungu humsaidia anayejisaidia unaheshimika sana kwa watoto.
 
Waisrael wamekufa 5526.
tangu mwaka Jana .
He Tanzania wanafika waliokufa na Corona hyo idadi?.
KWA MUNGU TUNATEGEMEA.na tutashinda.
Mganga MUNGU tu
Wewe una Mungu zaidi ya yule wa Waisrael taifa teule...!!! Vaa Barakoa, nawa mikono usiwe chanzo cha kifo cha ndugu & rafiki zako
 
Usipende kuchukua mifano ya nje ukaileta hapa kwetu,vita ya ugonjwa huu ni vita ya kichumi pia..kupigana kwa nchi moja kwa namna yake si sababu nchi nyingine iigee upmbanaji wa wengine

kuna watu yamkini mnalipwa ili kueneza taharuki kwenye jamii lakini naamini mtashindwa tu,sasa ni Corona gani ya sasa ichukue viongozi ambao wanatibiwa na kula wanacho taka ila wachukuliwe na Corona na tuachwe walala hoi sokoni,kwenye vijiwe vya kahawa,mashuleni kote huko hakuna mwenye Corona.

Ila akitokea mtu akaniambia kwa sababu za vita vya kiuchumi labda viongozi hawa walikaa mahala kwenye kikao na ajenti wa mzungu akawepo akawapiga sumu ili kisingizio kiwe ni kuleta chanjo hapa ntakukubali.

Libya ilikua ni nchi ya maziwa na asali hawakua na shida yoyote dhidi ya Ghadaffi, lakini kilicho tokea ni dhahiri kabisa raia wale walipewa kitu pasi wao kujua na kuamua kumkataa tu Ghadaffi wakaita na majeshi ya NATO ili eti waje kuwasaidia kumng'oa dikteta,yaani ni sawa na baba nyumbani kwako wanaibuka watoto wako wa kuzaa hawakutaki na wanashirikiana na mama yao wakukate kate ufie mbali.

Corona ni vita fulani tu.
 
Kwa wenzetu Wakristo dunia nzimà, Mungu ni wa Waisrael aliowateua yeye mwenyewe hata Mwanae Mpendwa alizaliwa huko, hao wengine ni miungu tu ikiwa ni pamoja na wa Waitalia, wa Wachina, wa Wasukuma nk. Mungu wa Watanzania anayewalinda wao tu hayupo Mbinguni wala duniani!
Tatizo lako ni uelewa tu basi
 
Inabidi kuifahamu hii The Jewish Covid 19 Management Protocol. Siku zote Tujifunze kwa waliofanikiwa.
 
Hebu tuseme tumepia waTanzania wote milioni 60, ikagundulika milioni moja wanamaambukizi ya Covid, hapo tumejua ukubwa wa tatizo imetusaidia nini? Hao wanaopima huko na kujifungia ndani, wanawapa raia wao pesa. Marekani mtu mmoja anapewa dola 1200 kwa wakubwa(zaidi ya milion 2 na laki 7) na dola 600 watoto(zaidi ya sh milion 1 na laki 3) bure ili kujikimu kipindi hiki cha corona.

Sisi hata elfu 10 kwa nusu ya watanzania hatuwezi kutoa yanini tulete taharuki ? Tatizo kubwa kwetu ni umasikini, jambo ambalo inabidi liwe kipaumbele.

Japokua Magufuli hakubali kua sisi ni masikini lakini huo ndo ukweli, sisi ni masikini na hili ni tatizo kubwa kuliko Corona. Mnamnanga sasa hivi mbona mlikua kimya kipindi cha kampeni?
1.
US House gives $500 million to Israel, only $600 per ...

12/23/2020 · US House gives $500 million to Israel, only $600 per person in covid relief 23 Dec 2020 The omnibus bill required 12 votes to approve defence …


2.
Third stimulus check: When could you get a $1,400 check ...
2/7/2021 · In the first stimulus payments in April 2020, which directed $1,200 to eligible adults as well as $500 per child, it typically took two weeks to several months for …
 
Israel yenye watu milioni 9 ilikuwa na maambukizi karibu milion 1 na vifo elfu 5 kama ulivyosema.


Bado hoja yangu iko palepale, kwamba pamoja na ustarabu wote wakujifungia ndani na kuvaa mibarakoa bado covid 19 imewatandika vilivyo.

Hitimisho: hakuna njia yeyote iliyoonesha matunda ya kupunguza corona zaidi ya kuijiondokea yenyewe naturally. Naungana na rais, tusitishane.
Sikupatii picha siku ukikumbwa na kovidi 19 utakavyotumua macho kama malimao, unadhani kuambiana ukweli ni kutishana?
 
Israel yenye watu milioni 9 ilikuwa na maambukizi karibu milion 1 na vifo elfu 5 kama ulivyosema.


Bado hoja yangu iko palepale, kwamba pamoja na ustarabu wote wakujifungia ndani na kuvaa mibarakoa bado covid 19 imewatandika vilivyo.

Hitimisho: hakuna njia yeyote iliyoonesha matunda ya kupunguza corona zaidi ya kuijiondokea yenyewe naturally. Naungana na rais, tusitishane.
Akili za kihuni hizi
 
We unaonekana hujui kuhusu virusi kabisa. Hivi Mungu anaweza kuwa na majibu yanayoexpire kweli yani kipindi kile atusaidie leo atuache duu. Ukifuata sayansi utajua kwann sahiv tumepigwa kuliko mara ya kwanza achana na imani Mfu..
Science ina require experiment and proof. sio uswahili.
utavijuaje virusi bila science?
Kama science ingekuwa fake..Mungu angeamua kuifutilia mbali isingekuwepo.
Ameruhusu iwepo ili tutumie kusolve mambo mbali mbali.

Yes kuna imani.. imani bila matendo ni mfu.
hata siku moja Mungu hakupi jibu la direct bila kuonyesha jitihada.

Huwezi omba Mungu akupe majibu ya mtihani wakati hukusoma.
 
Ilipungua dunia nzima lakini Tanzania pia ilichukuwa hatua kama kufunga shule na kampeni za mask na kunawa mikono lakini tulionywa itakuja second wave badala ya kujiandaa na second wave tukaanza kiburi, ingekuwa hawakujuwa kuwa wave ya kwanza itapungua wasingesema kuna second wave haiwezi kuja ya pili bila kuisha ya kwanza haya mambo yalitabiriwa na wataalamu sasa hata second wave tungewahi kuchukuwa tahadhari na sisemi lockdown tungefanya kama mwanzo tu ingepunguza kiasi. wenzetu wakawa busy kutafuta chanjo sababu wanajuwa huu sio mwisho sisi tukasema corona imekimbia Mungu anatupenda hatukujiandaa na second wave ndio unayoona leo haya tumekana mpaka tumeanza kuelewa.
Hizo hatua unazosema kama kufunga mashule,uzingatiaji wa kuvaa mask na kunawa mikono ulidumu kwa muda gani kiasi cha kusema ilisaidia kupunguza maambukizi? Mapema sana sisi tulifungua shughuli zote na kuacha kuzingatia kunawa mikono na kuvaa mask hilo la Corona kupungua lilitukuta sisi tushafanya ile party ya kuiaga corona muda mrefu tu.
 
Ungeelezea hiyo jewish manag protocol ina utaratibu gani ili na wewe uingie katika historia ya kuokoa maisha ya wale watakaitumia wakihusi ama kuthibitisha kuambukizwa... Ingekuwa vyema zaidi ya kumuongelea JPM jambo ambalo haliwezi badilisha chochote
Marekani imegawa hela za bure kwa wayahudi

US House gives $500 million to Israel, only $600 per ...

12/23/2020 · US House gives $500 million to Israel, only $600 per person in covid relief 23 Dec 2020 The omnibus bill required 12 votes to approve defence …
 
Back
Top Bottom