SAYANSI NA TEKNOLOJIA KATIKA MATOKEO HASI KATIKA VYOMBO VYA USAFIRI NA MATUMIZI YA SIMU KWA VIJANA WA KARNE HII PAMOJA NA LUGHA YETU.
Sayansi na teknojia imekuwa msaada mkubwa katika karne hii ya 21,kumekuwa na mavumbuzi mengi na ya kisasa,Sayansi na teknolojia imezalisha na kuwaibua wataalamu wengi katika janja hizo,na vitu vingi,mitaala mbalimbali ya elimu imebadilika kulingana na uhitaji wa Sayansi na Teknolojia,Vitivo mbalimbali pia vimeimarishwa,Sayansi imekuwa kipaumbele si tu kwa familia zetu,bali hata kwa Taifa zima.
Kulingana na ubora wa Sayansi na Teknolojia,lakini pia kuna matokeo hasi kwa jamii yetu,kwa mfano kwa sasa vyombo vingi vya usafiri vimeunganisha teknolojia ya Sayansi na Teknolojia kupitia runinga (Televisheni) kwa lengo la kuwaliwaza abiria wawapo katika safari,sio jambo baya hata kidogo,ila ubaya unakuja pale ambapo teknolojia hiyo inapogeuka kubomoa maadili na kelelezo cha MWAFRIKA.
Ndani ya magari yapo mambo yanayoendelea ambayo hayakemewi ni muhimu waangalizi na wamiliki wa vyombo hivyo pamoja na Serikali ifahamu hili na kuingilia ili kurekebisha mapema kabla sumu hii haijakomaa: Kwanini Sayansi na Teknolojia imekuwa na matokeo hasi katika vyombo vya usafiri.
1.Madereva kuonyesha muziki au filamu mbalimbali ambazo hazina maadili:
Miziki kama ya kuonyesha sehemu za mwili,mfano kitovu,mapaja au nguo za ndani ni kinyume na maadili na haifundishi katika jamii yetu,Sayansi haitakiwi kuwa kisu cha kutuchinjia kizazi chetu,kwani ndani ya usafiri kuna rika tofauti tofauti,ni lazima mamlaka zenye kusimamia vyombo hivi,kutoa elimu kwa watenda kazi wao,kusudi ya kulinda mila na tamaduni za Mwafrika.
Sambamba na hilo zipo video ambazo wakati mwingine zilishafungiwa na BARAZA LA SANAA LA TAIFA, lakini katika vyombo hivi tunakuta zikionyeshwa.
Wakati mwingine mambo haya ndiyo yamekuwa na vichocheo vya watu kuanguka katika tamaduni ngeni,ambazo ndiyo zimekuwa chanzo cha kuingiza tamaduni za kigeni katika Nchi zetu za KIAFRIKA.
Vijana wetu tuwafundishe maadili mema kupitia Sayansi na Teknolojia,Wasanii pia wafundishwe namna ya kuyakuza maadili na siyo kuyabomoa kupitia kazi wanazozifanya.
2.Sayansi na Teknolojia cha kuleta tamaduni ngeni:
Kwa mfano kwa sasa kuna watu wanavaa au kunyoa nywele vibaya kulingana na “ROLE MODEL”(Mtu anayevutiwa naye) vijana wengi wamekuwa ni waathirika katika hili huko mitaani,kupitia kuona kile walichoangalia ,kumekuwa na ongezeko la mmomonyoko na mwingiliano wa tamaduni mpya kwetu.Ni muhimu kuchambua yale mazuri katika yale yanayoletwa kupitia SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
3.Sayansi na Teknolojia katika mustakabali wa lugha yetu:
Kutokana na kukuwa kwa Sayansi na Teknolojia kumekuwepo na mwingiliano wa lugha,na wakati mwingine watu wamekuwa wakijiona kutokuzungumza labda lugha yetu ya kizawa ndiyo usomi Zaidi,na wakati mwingine wanamuziki wa Magharibi na uimbaji wao ambao wakati mwingine,umekuwa na lugha isiyo ya sitara,ndiyo umekuwa ukichukua nafasi katika jamii.
Ni ulimbukeni kutaka kuikuza na kuzungumza lugha au utamaduni wa mtu mwingine .
(b)MATUMIZI YA SIMU KWA VIJANA:
Katika nyakati hizi tulizokuwa nazo matumizi ya simu yamekuwa na umuhimu mkubwa sana katika kurahisisha mawasiliano,kulingana na Sayansi na Teknolojia ,Simu pia inachangia mambo mbalimbali kwa vijana na hili ni muhimu kulifanyia kazi kusudi tuokoe nguvu kazi ya vijana wetu wa sasa na wa baadaye.
(a) Matumizi ya simu yamewafanya vijana wakose bidii katika kufanya kazi kwa wakati kwa sababu matumizi ya muda wao mwingi,yanakula,muda kulingana na muda wao mwingi kutumia huko katika teknolojia ya mawasiliano
(b) Pia uvujaji wa taarifa za siri makazini kupitia simu hasa simu hizi za kisasa maarufu kwa jina la “SIMU JANJA” Umekuwa pia ni kero na kukosa uaminifu katika Taasisi mbalimbali za maendeleo,kwani tunaona hata katika miongozo mbalimbali katika Taasisi binafsi na zile za Serikali,suala la “USIRI” likitiliwa mkazo ili kulinda haki ya mwajiriwa na aliye mwajiri.Wakati mwingine ni vizuri kuwaajibisha wale wanaofanya hivi ili kulinda uwaaminifu wa Taasisi mbalimbali kwa manufaa ya wale wanaoongoza na wanaoongozwa.
(C) Kuna mrundikano wa mambo mabaya hasa katika kundi hili la vijana kupitia Teknolojia matumizi ya kutazama mambo machafu na maovu,hasa yale yasiyokuwa ya kimaadili kwetu,yamewavuta vijana sana,na wakati mwingine kusababisha masuala ya ubakaji,ulawiti,ushoga na usagaji.
Ndani ya Teknolojia ndani yake kuna tovuti na kurasa mbalimbali ambazo hazina maadili,wakati mwingine zimekuwa zikiwavutia vijana katika kufanya yale mabaya ambayo ni kinyume na utamaduni wetu,Kundi hili la vijana ni muhimu kulikimbilia mapema kabla halijapata madhara.
HITIMISHO:
Wadau mbalimbali wanaweza kutoa elimu juu ya matumizi mbalimbali katika masuala ya Sayansi na Teknolojia katika suala chanya na hasi,vyombo mbalimbali vya habari vinaweza pia kuandika Makala mbalimbali ambazo zinaweza kuwa na mchango mkubwa katika makundi kadhaa katika jamii yetu,tukifanya hivyo matumizi ya Sayansi na Teknolojia yatatusogeza katika hatua bora ya kuwa na watu ambao tutalisogeza Taifa letu na Familia zetu mahali ambapo Mungu amekusudia Maisha yetu kufika.
Mitaala mbalimbali iliyopo au inayoendelea kutayarishwa iwe inayoweza kuwaandaa watu kuwa bora na Wazalendo kwa kile kilichopo katika Taifa kupitia Sayansi na Teknolojia.
Upvote
2