Sayansi ya uumbaji ndani ya Qur'an/Koran: Sehemu ya 01

Unapochanganya sayansi na dini yako unakosea sana
 
Unapochanganya sayansi na dini yako unakosea sana
unajua hata ukiita mtu asiyejua kusoma na kuandika au kichaa au mtoto mdogo ukampa kalamu na karatasi ukamwambia aandike hilo karatasi mpaka lijae na wino....Yeye atachoronga choronga tu lakini baada ya hiyo michorongo ukiamua kutafuta herufi zilizojitokeza hutakosa..Lazima michorongo mingine itafanana na C,g,p,d,b,l,e nk. nk.
Ukilazimisha zaidi unaweza kupata hata maneno yaliyojitengeneza.

Kutafuta Miujiza kwenye quran ni sawa na kutafuta hizo herufi

kutafuta fact za kihistoria kwenye Quran ni sawa na kutafuta maneno kwenye michorongo

Kutafuta Sayansi kwenye Quran ndiyo kabisaa ni sawa na kutafuta sentesi zenye maana kwenye hiyo michorongo.
 
Ngoja tukukamate unafikiri watu ni mazuzu! Hiyo hadithi ipo kwenye mlango gani? Tupatie jina la scholar ambaye ni mufassiruun na kufafanua kama wewe ulivyofafanua hapo juu!
 
Mkisikia habari za Quran roho zenu huwa zinawakeleketa sana

Aya za sayansi zipo nyingi sana katika Quran ukizitaka zitakuja kama mvua maana aliyeumba ulimwengu ndio huyohuyo aliyeileta Quran

Chukua na hi nakupa kama zawadi

Quran 21:33.
Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga vinaogelea.
 
Sahih bukhari 4:421
Ngoja tukukamate unafikiri watu ni mazuzu! Hiyo hadithi ipo kwenye mlango gani? Tupatie jina la scholar ambaye ni mufassiruun na kufafanua kama wewe ulivyofafanua hapo juu!
View attachment 1673510View attachment 1673511Hapa unaambiwa jua likizama linaendaga kujificha under the throne ambayo ina miguu na inabebwa na malaika...likifika uko linasujudu linaomba ruhusa ya kuchomoza tena kesho...Mawazo ya hivi yaliwezekana kwasabab watu waliamini dunia ni flat lakini kama ni sphere inamaana hailizami kwenda sehem maana kuna sehem tu duniani bado linaonekana hata likizama huko meccaView attachment 1673513View attachment 1673512View attachment 1673514
 
NASIKIA HIKI KITABU KILISHUSHWA??
Hata Injili ya ilishushwa,Alishushiwa Yesu

Unatakiwa uwe mswahiili wa kufahamu kiswahili ndio utafahamu imekusudiwa nini inaposemwa kuwa vitabu vya Mungu vimeshuswa..

Injili(sikusudii biblia) na Kuran mfumo wake ni mmoja

Yesu alihubiri maneno yake kwa watu wake,kile alichohubiri ndio INJILI

Muhammad alihubiri maneno yake kwa watu wake,yale aliyohubiri ndio QURAN..

Hayo waliyohubiri,walishushiwa na Mungu kwa njia za Malaika..

Malaika Jibril/Gabriel walipewa jumbe na Mungu wazifikishe kwa Mitume ili zifikishwe kwa Binadamu..

Hiyo ndio maana ya KUSHUSHWA usifikirie kuwa kitabu kizima kimeanguka kutoka mbinguni..
 
Hayo ndio yaliyoandikwa kwenye Quran suatil Nisai sura ya 4 aya ya 412,..(4:412)

Sasa hayo mambo ya Jua yametokea wapi??
 
injili ya Issa iko wapi?
 
Kila hadith ina munasabah yake! Usifikiri kila hadith unakoti tu ili kuinasibisha kwenye mazingira unayoyaona wewe!
Basi poa nishakutajia hadith ni bukhari na mufassirun ni Ibn kathir.
Kuna lingine?
 
Babu mbona unaleta maelezo mengi?

Vitabu vya Uislam vinafahamika na wanazuoni wao wanafahamika ambao ni warathatul anbiyaai. Wamejikita kwenye fani mbalimbali za dini!

Ukienda kwenye fiqh ina watu wake na wanafahamika, Muhaddith wapo na wanafahamika, Ahlul mantwiq wapo na wanafahamika, mufassiruun wapo wanafahamika!

Umekoti aya kutoka suratul Yaseen, ukafungamanisha na hadith kuonyesha zinashabiana. Swali nililokuuliza ni mufassiruun yupi aliyeelezea hiyo aya kama wewe ulivyoielezea mbele ya umma wa Jf?

Tutajie jina la huyo mufassiruun, jina la kitabu na kurasa. Ni swala jepesi tu! Ukija usije na ngonjera njoo na jawabu!
 
Basi poa nishakutajia hadith ni bukhari na mufassirun ni Ibn kathir.
Kuna lingine?
Babu hivi unazijua hadithi?
Bukhari katika mlango upi wa hadithi? Na hadithi nambari ngapi?

Ngoja niiangalie tafseer ya Ibn katheer kwenye hiyo aya! Nitarudi hapa hapa!
 
Nitaje marangapi?Kusoma huwezi hata picha nilizoweka huoni?
 
Babu hivi unazijua hadithi?
Bukhari katika mlango upi wa hadithi? Na hadithi nambari ngapi?

Ngoja niiangalie tafseer ya Ibn katheer kwenye hiyo aya! Nitarudi hapa hapa!
babu naona umeamua kunipotezea muda.
Nishasema Huko juu ni bukhari 4:421
Sasa kukusaidia zaidi ni book 54 toleo la 4 hadith namba 421
 

Haujakosea ndugu, Upo sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…