Quraan ni pana sijui niseme inahitaji elimu kubwa kidogo kufumbua mafumbo hayo, si kukurupuka wala kuisoma kwa mihemko
Yawezekana mimi na wewe hatujajua tafsiri ya hiyo aya, katika karne ya 6 quraan imeongea vitu ambavyo kwa kipindi hiko vilikuwa no vituko kuamini, mathalani hii ya jua kujongea nani angeamini, mpaka miaka ya karibuni wanasayansi ndio wamekuja kuproove hilo, koraan imezungumzia bahari 2 maji yake kutokukutana, hebu karne ya 6, watu wa jangwani umwambie allah kajaalie maji ya bahari 2 hayakutani, si anakuona hayawani, quraan imezungumzia orbit, quraan imezungumzia mpaka milima kuwa vizingiti, (kazi ya milima, mijongeo ya milima vitu ambavyo kipindi hicho ni kituko, imegusia time relativity ambayo mpaka sasa bado kuna utata kwa baadhi ya watu, quraan hiyo imezungumzia origin ya ulimwengu, asili ya chuma, imezungumzia black holes, hivyo quraan sio ya kubeza.. Bado imezungumzia skin as pain receptors.
Mtume s.a.w alitufundisha tusipulize chakula, siku moja nikaona clip ya mwanasayansi anaonesha kinywaji(maji) yanavyobadilika ukiyapuliza
Ningekuwa na uwezo kauli zote za katika quraan ningezifanyia research nikaprove.
Hata hii unayosema jua kuzama topeni, usikute kuna elimu kubwa ndani yake chief.
Uislam ni dini(njia, mfumo wa maisha) inayo muelekeza mja katika kuliendea kila jambo, mathalani mwanadamu kuanzia anapoamka mpaka anarudi kitandani usiku basi uislam umecover kote huko, elimu zetu ndogo, wengine hatujasoma kabisa tunabaki kwenye ubishani wa kimehemko badala ya kusoma zaidi.
Hiyo jua kuzama topeni mie sina elimu nalo, huenda lina maana nzito kidogo, alah pia kazungumzia usiku na mchana, huenda tope ndio usiku uliolengwa ila siwezi tolea ufafanuzi kwa kuwa sina elimu nalo, jitahidi uwafate wajuzi zaidi au lah, sayansi itakuja kuthibitisha hili miaka ijayo sababu naamink quraan iko sahihi.