Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Nikikuambia shambani kwangu mi nina panda

Hapo nitakuwa nimemaanisha nini?

Utakuwa umepata tafsiri gani?

Nitakuwa nimepanda mmea yani "planting"?

Au nimepanda mti kwa kuukwea juu yake yani "climbing"?

Au nina miliki mnyama huyu aitwae panda?

View attachment 2843510

Hapo utaenda na jibu gani? Na lina takiwa moja
Jibu swali, ulikuwa unamuomba nani katika maombi yako?
 
Kwenye ulimwengu wenu wa utupu kupasuka kila kitu kinatokea kwa bahati nasibu, hakuna morality. Ukoshataja morality maana yake unamtaja aliyeiweka, ambaye ni Mungu.
Morality haihusiki na Mungu

Ingekuwa inahusika na Mungu basi tusingeona maandiko kwenye biblia yanayoonesha Mungu akiuwa watoto kwa lengo la kumkomoa Farao.

Morality unaijua?
 
Ni sawa na rainbow color kabla ya mashoga kuiweka kwenye nembo yao. Ilikuwa ni rangi nzuri iliyokuwa ikiwakilisha mambo mema tu.
KAbisa mkuu

hata mimi binafsi nimekuwa nikiwashangaa watu waachao kutumia hii alama ya rainbow katika matumizi ambayo walikuwa wakiyatumia kabla ya ushoga eti kisa mashoga wanatumia.

Kuacha kutumia alama hii ambayo Katika asili tumeikuta ikitanda katika anga alafu kiurahisi tunakubali kwamba ni alama ya mashoga aisee inakuwa sisi ni wajinga.
 
Kisicho kuwepo Hakihitaji uthibitisho wa kutokuwepo kwake, Kwa vile hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika.
Kanuni hii haiwezi kuapply katika mjadala wa Mungu,kwa sababu Wanaomthibitisha Mungu wanamthibitisha kupitia matukio ama vitu ambavyo tunaviona na kuvikiri.

Hivyo wanaomthibitisha Mungu wao humthibitisha kwa yale mambo yaliyothibiti.

Kwa mantiki hiyo wanaokanusha uwepo Wa Mungu mbele ya wakubaliji uwepo wa Mungu basi hawa wakanushaji nao wanayo dhima ya kuthibitisha kutokuwepo kwake.

Hivyo kanuni hiyo haiwezi kuapply katika mjadala huu.

Ndio maana yule bwana mkubwa

Stephen Hawking's

Aliandika kitabu chake akakiita

There's 'No Possibility' of God in Our Universe.

Humo kaweka uthibitisho (kwa mjjibubwa yeye) wa kuthibitisha kwamba hakuna Mungu.

Hivyo hata wanaopinga Mungu hayupo nao wanatakiwa wathibitishe kwa hoja mbalimbali kama alivyofanya bwana stephen.
 
Morality haihusiki na Mungu

Ingekuwa inahusika na Mungu basi tusingeona maandiko kwenye biblia yanayoonesha Mungu akiuwa watoto kwa lengo la kumkomoa Farao.

Morality unaijua?
Kuua ni kinyume na morality ipi? Imewekwa na nani?
 
KAbisa mkuu

hata mimi binafsi nimekuwa nikiwashangaa watu waachao kutumia hii alama ya rainbow katika matumizi ambayo walikuwa wakiyatumia kabla ya ushoga eti kisa mashoga wanatumia.

Kuacha kutumia alama hii ambayo Katika asili tumeikuta ikitanda katika anga alafu kiurahisi tunakubali kwamba ni alama ya mashoga aisee inakuwa sisi ni wajinga.
Ni ujinga wa watu tu wa kuvipa tafsiri ya ubaya vile vitu vizuri vinavyofanywa na wabaya.

Kwasababu vibaka wengi wanavaa majeans na kunyoa panki basi tayari hiyo imeshapewa tafsiri mpya kuwa mtu yeyote mwenye panki kimaadili anaonekana kama kibaka.

Sasa siku vibaka wataanza kukaba wakiwa wamevaa suti afu wamenyoa para. Sa sijui tutaanza kuhalamisha uvaaji wa suti na kunyoa vipara kwasababu ni style ya vibaka wengi?
 
Kisicho kuwepo Hakihitaji uthibitisho wa kutokuwepo kwake, Kwa vile hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika.

Mungu huyo hayupo kwa namna yoyote ile zaidi ya mawazo ya kufikirika tu, Imaginations just an illusion.
Unaweza kuthibitisha uwepo wa electron? Hivi unajua kwamba umeme hakuna mtu amewahi kuuona? Unachoona ni effects za uwepo wa umeme. Ukiweka taa utaona mwanga na kusema umeme upo japo hauuoni.

Basi hata Mungu tunamuona kupitia matendo yake makuu hasa katika uumbaji wa ulimwengu na vyote vilivyo ndani yake.
 
Unaelewa morality ni nini mpaka uhitaji majibu ya kujua iliwekwa na nani?
Kwa mujibu wa dictionary, morality is principles concerning the distinction between right and wrong or good and bad behaviour.

Sasa hizo principles zimewekwa na nani?
 
Haujajibu ndio maana nimekwambia ujibu kwamba ulikuwa unafanya maombi yako kwa nani?
Sasa kama sijajibu kwanini ujiwekee majibu ya kuhusisha na maswala ya Mungu?

Statement yenye tafsiri zaidi ya maana moja unaanzaje kulazimisha kwa kujichagulia aina fulani ya maana kuwa ndio kusudio langu kwasababu tu ya interest zako?
 
Kwa mujibu wa dictionary, morality is principles concerning the distinction between right and wrong or good and bad behaviour.

Sasa hizo principles zimewekwa na nani?
Mbona sijaona Mungu kwenye hiyo tafsiri?

Sasa nikikuambia Morality haihusiani na Mungu utakuwa umenielewa
 
Sasa kama sijajibu kwanini ujiwekee majibu ya kuhusisha na maswala ya Mungu?

Statement yenye tafsiri zaidi ya maana moja unaanzaje kulazimisha kwa kujichagulia aina fulani ya maana kuwa ndio kusudio langu kwasababu tu ya interest zako?
Sasa elezea ulikuwa unaomba nini na kwa nani.
 
Back
Top Bottom