Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Scars haaamini kwenye uwepo wa Mungu lakini anaomba dua na kufanya maombi

Mbona sijaona Mungu kwenye hiyo tafsiri?

Sasa nikikuambia Morality haihusiani na Mungu utakuwa umenielewa
Nimekuuliza nani kaweka morality? Source yake ni nini?
 
Sasa elezea ulikuwa unaomba nini na kwa nani.
Hili swali ulitakiwa kuuliza kule ulipoitoa ile Quote.

Namimi ili nikujibu unatakiwa u-confess kwenye main thread yako kwa kuninukuu vibaya na ukiri kuwa hukuelewa na kuomba moderators wabadilishe title ya uzi
 
Yani watu wanataka tushindwe kutumia maneno yaliyokuwa na maana nyingine kabla ya dini kwasababu saizi yamemilikiwa na dini kimazoea hivyo tukionekana kuyatumia wanaanza kutu accuse kuwa sisi na wao tupo kitu kimoja

Ni sawa na rainbow color kabla ya mashoga kuiweka kwenye nembo yao. Ilikuwa ni rangi nzuri iliyokuwa ikiwakilisha mambo mema tu.

Ila saizi imejenga tafsiri mpya ukionekana umevaa nguo yenye rangi za rainbow watu watasema ni shoga.

Sasa swali la kujiuliza je ni kweli rainbow maana yake ni ushoga au ni mazoea ya watu kutokana na kuona mashoga wanatumia rangi hizo?
Nafikiri wewe unajichanganya tu.Ukweli akili yako inajaribu kumpinga Mungu lakini ndani sana nafsi yako inamkiri ndo maana uliisema uliomba dua.Kiswahili cha kuomba maana yake yupo aombwae.Sasa unaposema ni neno lenye kumtakia mtu matashi mema,naona unajaribu kujitetea. Tafakari chukua hatua.
 
Naona nimekubana mbavu unaanza kukimbia mapema sana. Kama jibu unalo litoe hapa.
 
Kwa mujibu wa chanzo chako ulichoweka kimemtaja nani kama mletaji?
Hapo nimekupa tafsiri halafu nakuuliza nani ameweka ndani ya wanadamu wote hiyo morality? Dunia nzima na kwenye jamii zote kuua ni jambo baya, kwanini? Under whose standards?
 
Nafikiri wewe unajichanganya tu.Ukweli akili yako inajaribu kumpinga Mungu lakini ndani sana nafsi yako inamkiri ndo maana uliisema uliomba dua.Kiswahili cha kuomba maana yake yupo aombwae.Sasa unaposema ni neno lenye kumtakia mtu matashi mema,naona unajaribu kujitetea. Tafakari chukua hatua.
Tatizo lingine la kuwa toxic na udini naloliona ni swala la kila muumini kujifanya amepewa karama ya kuona yale yaliyojificha kwa wengine.

Umeona kama hapo kwenye maelezo yako umetaja neno nafsi.

Namimi nakuambia hilo neno pia nalitumia vizuri katika daily life yangu licha ya kwamba mimi ni Atheist.

Lakini utofauti unakuja kwenye maana.

Neno nafsi kwangu lina maana ya personal emotions au zile feelings ambazo naweza kusema zipo controlled na ubongo lakini katika kuzielezea nikazihusisha na moyo.

Kwa hiyo utagundua kwenye mbadala wa neno nafsi naweza nikatumia neno "moyo" na bado nikafikisha maana ileile niliyoitaka.

Ni tofauti na wewe unayetafsiri nafsi kama kitu ambacho ni immortal kinaishi ndani yako hata siku ukifa chenyewe kitapaa juu kwenda huko mbinguni.

Sitafsiri nafsi kama apparatus ya kiroho ambayo ipo ndani yako kama muongozo.

Sitafsiri nafsi kama device ya kiroho ambayo imewekwa ndani yako kwa ajili ya ku link connection kati ya Mungu na wewe.
 
Hapo nimekupa tafsiri halafu nakuuliza nani ameweka ndani ya wanadamu wote hiyo morality? Dunia nzima na kwenye jamii zote kuua ni jambo baya, kwanini? Under whose standards?
Unajua unakosea hadi kuuliza swali

Nani kaweka ndani ya mwanadamu ndio swali gani?

Nini kinachokufanya ufikiri morality inapaswa kuwekwa na hicho kitu ukichokipa identity ya "nani"?
 
Kwahiyo unaamini simba kumfunga waydad na ila hauamini kuhusu kuwepo muumbaji?
Eeeh naamini tutamfunga Wydad maana yake sina uhakika ndio maana naamini

Wydad namjua tumecheza naye mechi tatu kashinda 2 nimeshinda moja.

Mechi ya mwisho alipigiwa mpira mwingi na bao alipata kizari tu na ndio maana wametimua kocha

Kwasababu mpira ni namba basi matumaini yangu ya kumfunga Wydad nayaona ila ipo nafasi pia ya matokeo kuja tofauti.

Sasa Mungu sababu ya kuamini kwanza nitakuuliza katika maelfu ya Miungu, Mungu gani unayetaka mimi nimuamini?

Na kwanini wewe huamini Miungu hiyo mingine?
 
Yani watu wanataka tushindwe kutumia maneno yaliyokuwa na maana nyingine kabla ya dini kwasababu saizi yamemilikiwa na dini kimazoea hivyo tukionekana kuyatumia wanaanza kutu accuse kuwa sisi na wao tupo kitu kimoja

Ni sawa na rainbow color kabla ya mashoga kuiweka kwenye nembo yao. Ilikuwa ni rangi nzuri iliyokuwa ikiwakilisha mambo mema tu.

Ila saizi imejenga tafsiri mpya ukionekana umevaa nguo yenye rangi za rainbow watu watasema ni shoga.

Sasa swali la kujiuliza je ni kweli rainbow maana yake ni ushoga au ni mazoea ya watu kutokana na kuona mashoga wanatumia rangi hizo?
Ila Scars mbna ungetumia evidence ingine bila kuingiza ushoga jaman, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nadhani mkuu wewe umekurupuka. Akisema haamini uwepo wa mungu ungemuuliza anaamini uwepo wa nini?

Pili hapo kwenye hiyo comment yake hajamtaja mungu popote. So kuomba kwake dua ungemuuliza anaomba dua kwa nani na sio kumsingizia kuwa amemuomba mungu.

Pia unatakiwa useme kama dua linaombwa kwa mungu tu au kila mtu anaomba dua anapopaamini. Je anaefanya tambiko kwenye mti au mlima nakufanya dua zake anaomba kwa mungu?
Usiwe mbishi...huyo anayemwomba dua ndo Mungu wake....tayari anaamini kuna kitu chenye uwezo wa kuombwa na kikatoa majibu..
 
So Scars kutumia neno dua maana yake anaamini Mungu?

Maana yake na mimi nitakuwa sahihi kusema hata Wakristo na Waislamu watakuwa wanaabudu Miungu ya kigiriki iwapo tutabaini kuna maneno fulani yamayopingana na dini zenu mkiyatumia?

Kwasababu wamekuwa wakitaja miezi ya mwaka kwa kuiita Januari ambapo kimsingi Januari ni jina la Mungu wa kigiriki aitwaye Janus.

Au niseme mnaabudu miungu ya kirumi kwasababu mmekuwa mkiita mwezi wa tatu "March" wakati hilo ni jina la Mungu wa kivita wa kirumi?

Vipi kuhusiana na siku za wiki Monday, Tuesday, Wednesday, Friday, Thursday, Saturday hadi Sunday ambaye ni Mungu jua?

Hujui kwamba hiyo ni Miungu?

Kwahiyo tunapokuona ukitamka tusemeje sasa? Tuseme unatamka hayo maneno kwasababu unaamini hiyo Miungu?

Au tuseme na nyie mnatuektia kusema mnaamini Mungu na wakati tunawaona mnatumia Dollar ya marekani ambayo ina chata ya kishetani ambayo imeelezwa kwenye vitabu vyenu?

****************************
Kujibu swali lako

Kwa bahati mbaya unaonekana kushindwa kuelewa baadhi ya maneno yana double meaning kwa kuchukua maana ile iliyo kaririwa ambayo imekuwa ikitumika sana kimazoea

Neno dua linaweza kuwa na maana nyingine na kutumika kama "wish" au "hope"

Kumtakia mtu heri ya jambo lolote linaloenda kufanyika mbele hiyo sio dua kwa mtazamo wa kidini ni jambo la kiutu katika morality

Lakini kama upo katika circle ya udini lazima uwe na perception ya tofauti unaweza kusema ni dua

Kwa hiyo hayo ni maswala tu ya utata wa maneno hususani pale inapotokea neno kuwa na maana zaidi ya moja huku maana fulani ndio ikiwa inatumika kimazoea kwenye jambo fulani.
Hapa umeleta ubishi na maelezo mengi ya bure....ujumbe wako ulikuwa moja kwa moja...haya maelezo ni ngonjera tu
 
Back
Top Bottom