Unaweza ukatoa mifano hai ya hiyo michango ya atheism katika jamii?
Mfano hai ni James Randi
James Randi alikuwa ni mtu wa physics na alipenda sana kufanya maonyesho ya magic
James Randi alikuwa ni Atheist na watu walikuwa wanamuita mchawi kwa kile alichokuwa ana perform jukwaani.
Licha ya mara nyingi kuwaambia watu kuwa hakuna uchawi ni trick tu ambazo hamjajua nazifanyaje lakini watu walikuwa wagumu kumuelewa.
Mpaka siku moja alipoletewa taarifa ya mchungaji mmoja aitwaye Peter Popof kuwa ni mtu ambaye amepewa karama ya kujua maisha yako kabla wewe hujamuambia.
James Randi alisema hakuna namna yeyote mtu anaweza kupata taarifa zako kwa kumtajia tu jina lako.
James Randi akaenda kufanya utafiti kwenye hilo kanisa na hiki ndio alichokuja nacho.
Peter Popof alikuwa na foundation yake ambayo ilikuwa inasimamiwa na mkewe na kila muumini lazima apitie hapo kwanza.
Watu hawakuweza kujua kuwa hiyo foundation inamilikiwa na huyo Pastor.
Katika hiyo foundation muumini utajaza fomu za taarifa zako na matatizo yako na mambo mengine ambayo yanakusumbua.
Pastor akiwa ibadani alikuwa anavaa ear piece kufanya mawasiliano na mkewe aliyepo nyumbani.
Kwa hiyo ilipokuwa inatokea muumini kaenda madhabauni basi Pastor alikuwa anamuuliza jina lake.
Muumini akijibu, kule mkewe anasikia kwa hiyo anaanza kutafuta jina hilo kwenye zile taarifa za watu walioandikisha.
Akishapata anaanza kumsomea mahali huyo mtu anaishi, ana familia au hana, matatizo yake aliyonayo na yalianza kumsumbua lini
Ambapo Pastor yale maneno anayosomewa na mkewe yeye anakuwa anayatamka mbele ya maiki na waumini wakisikia.
Na yule muhusika anakuwa surprised kwasababu kweli kilichotajwa ni sahihi.
Sasa James Randi alichokufanya aka intercept zile signal kukata mawasiliano kati ya mke wa Pastor na Pastor mwenyewe.
Kwa hiyo watu walipokuwa wanakuja wakitaja majaina yao, kule kwa mke wake sauti haifiki mawasiliano hakuna. Huku Pastor anasubiriwa atoe ubashiri wake na mambo yanamgomea.