Umebaki unalalamika tu Kuwa Mungu hayupo ,Mungu hayupo
Na wewe umebaki kusema Mungu yupo! Mungu yupo!
Ila mpaka sasa umeshindwa kuthibitisha uwepo wake.
Unaruka ruka tu.
Ok ngoja nikujuze kuhusu hoja zako, japo unarudi kule kule kila mara
1. “Ulijuaje Mungu yupo kabla ya kujua ni wa kiroho?”
Hoja ya "kujuaje Mungu yupo kabla ya kusema ni wa kiroho" inahitaji kueleweka ndani ya muktadha wa dhana za ontolojia (nature of being) na epistemolojia (how we know).
Hiyo dhana ya "ontolojia" ni ya nani?
Imetoka kwa nani? Kwa utafiti upi na uthibitisho upi?
Ni nani aliileta hiyo dhana ya ontolojia?
Na huyo aliye ielezea dhana ya "ontolojia" alikuwa na uthibitisho upi wa kuwepo Mungu?
Au alifosi tu kuna Mungu bila uthibitisho na akawapachikia na kuwa andikia hii dhana yake uchwara ya "ontolojia" bila uthibitisho?
Jibu: Dhihirisho la uwepo wa Mungu linatokana na tafakuri juu ya mambo yasiyoelezeka kirahisi kupitia asili ya ulimwengu. Wanafilosofia kama Thomas Aquinas walijenga hoja za kimantiki, kama ile ya "Kila kitu chenye mwanzo lazima kiwe na sababu ya kuwepo."
Unathibitisha vipi ulimwengu una mwanzo?
Huyo Thomas Aquinas, Alijuaje na alitoa uthibitisho upi kwamba ulimwengu una mwanzo?
Ulimwengu Hauna chanzo na Hauhitaji kuwa na chanzo.
Kama ni lazima ulimwengu uwe na mwanzo, Hata huyo Mungu lazima awe na mwanzo.
Huwezi kufosi kwamba Mungu hana chanzo, Halafu unaanza kulazimisha ulimwengu uwe na chanzo.
Una elewa hilo?
Hii inamaanisha kwamba lazima kuwe na chanzo cha mwisho kisicho na mwanzo (uncaused cause), ambacho ni Mungu.
Sio Mungu, Kwa sababu bado hujui kama yupo na umeshindwa kuthibitisha uwepo wake.
Ulimwengu upo na una thibitishika upo na wala hauna chanzo chochote kile chenye ukweli kilicho thibitika kiliuumba ulimwengu.
Hicho chanzo hakipo na wala hakuna uthibitisho wowote ule wa chanzo kilicho umba ulimwengu.
Hivyo,
Ulimwengu hauna chanzo.
Tafakuri hii haimlazimishi Mungu awe wa kiroho moja kwa moja, bali inahitimisha uwepo wa chanzo kisicho cha asili.
Kwa nini unalazimisha na kuhitimisha kuna chanzo kisicho cha asili, ilihali hukijui na wala huwezi kuthibitisha kama kipo?
Huoni kwamba unafosi mawazo yako ya kiimani, yasiyo na uthibitisho wowote ule?
Hali ya kuwa Mungu ni wa kiroho hujengwa kutokana na dhana kwamba chanzo hicho hakiwezi kuwa cha kimwili kwa kuwa kipo nje ya muda na nafasi.
Bado hujathibitisha uwepo wa hicho chanzo ukiitacho Mungu.
Unafosi fosi tu kiwepo, ilhali hata hujui kipoje.
Ndio maana kuna dhana nyingi uchwara kama hizo za " ontolojia" zisizo na uthibitisho wowote ule.
2. “Thibitisha kwanza, ulijuaje Mungu yupo?”
Hoja hii inahitaji mjadala wa kina kuhusu ushahidi wa uwepo wa Mungu.
Jibu: Mungu anaweza kueleweka kupitia ishara za ulimwengu (evidence of design) na hoja za kifalsafa kama vile:
Hapa unafanya Logical non sequitur.
Ulimwengu
Haumuhitaji huyo Mungu ili uwepo, Ni nyie tu mnahangaika na kujaribu kufosi ulimwengu uwe umeumbwa na huyo Mungu wenu wa kufikirika na kusadikika.
Una unganisha vitu viwili tofauti visivyo na uhusiano wowote ule kuunda hitimisho potofu.
Unatumia vitu ambavyo tayari vipo kwenye existence kutaka kufosi kwamba ndio viliumbwa na huyo Mungu wako wa kufikirika.
Fine-tuning: Ulimwengu unaonekana kuwa umewekwa kwa ustadi mkubwa ili kuleta uhai. Sababu ya hali hii haielezeki kwa bahati tu. Hata atheists kama Fred Hoyle alikiri kwamba "design seems to have been fine-tuned."
Una thibitisha vipi kwamba ulimwengu uliwekwa?
Je kama haukuwekwa?
Utajuaje?
Kwa nini unahitimisha moja kwa moja kwamba, Ulimwengu uliwekwa?
Na bado hujui, huna uhakika na wala huwezi kuthibitisha hicho kilicho uweka Ulimwengu?
Moral Law (Sheria ya Maadili): Binadamu wana maadili ya asili ambayo hayawezi kuelezewa na mchakato wa kibaolojia tu. Kama sheria zipo, lazima kuwe na Sheria Kuu (Moral Law Giver).
Huu ulazima wa kwamba lazima awepo " Moral law giver" umetoka wapi na uliwekwa na nani?
Huyo aliyeuweka, Alijuaje na alito uthibitisho upi kwamba kuna, Moral law giver?
Hoja ya Ontolojia: Uwepo wa dhana ya Mungu unashawishi kuwepo kwa Mungu. Wazo la kuwa na Mungu Mkamilifu halingetokea bila chanzo kamili.
Bado hata hiyo hoja ya "ontolojia" inaeleza tu, Mungu ni " dhana" .
Kwamba bado hakuna uhakika, ushahidi wala uthibitisho wa uwepo wa Mungu huyo kwenye uhalisia.
Mungu huyo anabaki "dhana" ya kufikirika tu, imaginations just an illusion.
Hata hiyo ontolojia, Ni uthibitisho wa kwamba Mungu hayupo katika uhalisia. Ni dhana tu ya kufikirika.
Hivyo Mungu hayupo katika uhalisia bali katika dhana ya kufikirika na kusadikika tu.
Uzoefu wa Kiroho: Milioni ya watu duniani wamepata uzoefu wa kiroho. Hata wanasayansi wa akili wanakubali kuwa uzoefu wa aina hii ni halisi kwa wahusika. Ingawa unaweza kusemwa kuwa hallucination, huwezi kupuuza ushuhuda mkubwa kiasi hiki.
Kukubali unaweza kukubali hata uongo, Lakini haitamaanisha kwamba hicho kinacho kubaliwa ni ukweli kwa vile kimekubaliwa na wengi.
Watu wengi pia wanaweza kuukubali uongo.
Hivyo "uzoefu wa kiroho" wa mamilioni ya watu duniani
Hauthibitishi na wala
Haudhihirishi kwamba kuna Mungu.
Bado inabakia ni imani na mitazamo yao tu isiyokuwa na uthibitisho wowote ule wala ukweli wowote ule.
3. “Unathibitisha vipi kwamba ulimwengu ulisababishwa na huyo Mungu?”
Hoja ya sababu kuu inabainisha kwamba kila kitu kilicho na mwanzo lazima kiwe na chanzo.
Ulimwengu hauna chanzo.
Ni ninyi tu mnafosi ulimwengu uwe na chanzo mkiitacho Mungu.
Lakini hamuwezi kuthibitisha uwepo wa chanzo hicho mkiitacho Mungu, Hivyo ulimwengu unabaki bila chanzo.
Mpaka pale mtakapoleta uthibitisho kwamba, Mungu huyo ndio chanzo cha ulimwengu. Na ithibitike hivyo pasi shaka.
Unless otherwise...👇
Kama kila kitu kilicho na mwanzo lazima kiwe na mwanzo, Hata huyo Mungu lazima awe na chanzo.
Na kama si lazima kila kitu kina mwanzo, Hata Ulimwengu hauna chanzo na Hauhitaji kuwa na chanzo.
Jibu: Ulimwengu unaonyesha kuwa ulianza kuwepo (Big Bang theory). Kama ulianza, lazima kuwe na chanzo chake. Chanzo hiki hakiwezi kuwa cha asili kwa sababu chanzo cha asili kingekuwa ndani ya ulimwengu wenyewe, na hivyo kuhitaji chanzo kingine. Mungu ndiye chanzo hicho kisicho cha kimwili, kisicho cha wakati, na kisicho na mwanzo.
Huyo Mungu kabla ya kuwa
"chanzo cha kila kitu" alikuwa wapi?
Huko alikokuwa kulitoka wapi?
Kama hakuwa mahali popote pale, Basi pia hayupo popote pale.
Huyo Mungu mmemtunga vichwani mwenu tu, Na ana exist kwenye mawazo yenu kufikirika tu.
4. “Kama Energy imeweza kuwepo bila kuwa created, kwa nini ulazimishe kuna Mungu?”
Jibu: Hoja ya nishati kama chanzo cha kila kitu inapingwa na ukweli kwamba nishati haiwezi kujieleza yenyewe au kuamua kitu kwa hiari. Nishati haina akili, lakini ulimwengu unaonyesha ushahidi wa akili kubwa iliyojipanga. Hii inatupeleka kwa chanzo chenye uwezo wa kuumba kwa hiari, ambacho ni Mungu.
Hata huyo Mungu wenu hawezi kujieleza mwenyewe, Ndio maana wewe unahangaika kumwelezea.
Hata huyo Mungu wenu hana Akili, ndio maana hawezi na kashindwa kujidhihirisha mwenyewe.
Huyo Mungu hayupo, Ni wewe tu unafosi awepo na unahangaika kumwelezea.
5. “Unathibitisha vipi kwamba Mungu angejidhihirisha waziwazi, kila mtu angeamini bila hiari?”
Jibu: Mungu ameacha dalili wazi za uwepo wake (design, moral law, and spiritual experiences), lakini amehifadhi uhuru wa mwanadamu wa kuchagua. Imani si suala la kulazimishwa; ni uamuzi wa hiari. Kama Mungu angejidhihirisha waziwazi kwa kiwango cha kumlazimisha kila mtu kuamini, uhuru wa hiari ungeondolewa, na mahusiano ya kiroho hayangekuwa ya kweli.
6. “Kwa nini unahitimisha moja kwa moja kusema kuna Muumba?”
Jibu: Hoja ya muumba inatokana na asili ya ulimwengu. Kama kila kitu chenye mwanzo kina chanzo, basi ulimwengu lazima uwe na chanzo
Hata huyo Mungu lazima awe na chanzo.
Na kama si lazima kila kitu kilichopo kina chanzo, Ulimwengu pia hauna na hauhitaji uwe na chanzo.
. Uchunguzi wa kina hauoneshi chanzo kingine chochote chenye sifa zinazolingana na Mungu wa kiroho: asiye na mwanzo, wa milele, na mwenye uwezo wote.
7. “Dhana za Mungu ni za uongo ambazo zimerithishwa vizazi kwa vizazi.”
Jibu: Hoja kwamba Mungu ni dhana ya kubuni hupuuzilia mbali ushuhuda wa kihistoria, kijamii, na kiroho. Historia inaonyesha kwamba wazo la Mungu linatokea kwa watu wa kila tamaduni, hata zile ambazo hazijawahi kuwasiliana. Hii inaonyesha kuwa dhana ya Mungu si matokeo ya kurithishana tu, bali ni sehemu ya uelewa wa kina wa mwanadamu.
8. “Einstein na Newton kukiri uwepo wa Mungu hakuthibitishi kwamba yupo.”
Jibu: Einstein na Newton hawakuthibitisha uwepo wa Mungu moja kwa moja, lakini walikubali kwamba kuna akili ya juu kutokana na uzuri na utaratibu wa ulimwengu. Ingawa ushuhuda wao hauhitimishi mjadala, unatoa msingi mzuri wa kuelewa kwamba wazo la Mungu halipingani na akili za juu zaidi.
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
Ulimwengu HAUNA CHANZO.
Ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo.