Seba aliyeandika meseji kwa rafiki yake amtunzie mwanae na anakata roho kwenye ghorofa ya Kariakoo lililoanguka, akutwa amefariki

Rais katoa shilingi milioni 700 kwa timu ya mpira wakati hawa watu bado wamefukiwa na jumba lililoanguka.

How insensitive.
Kwamba kama watu wakuangukiwa na jengo mambo mengine yasiendelee.

Acheni hizo, na uzuri/ubaya hajaanza leo kumwaga pesa huko kwa wachezaji.

Labda kakosea timing tu ila sio kua hajali walioangukiwa na jengo.
 
Kwamba kama watu wakuangukiwa na jengo mambo mengine yasiendelee.

Acheni hizo, na uzuri/ubaya hajaanza leo kumwaga pesa huko kwa wachezaji.

Labda kakosea timing tu ila sio kua hajali walioangukiwa na jengo.
Sasa kukosea timing unaona ni jambo dogo la kusema "labda kakosea timing tu"?

Hapo kuna mengi, lakini nahofia tuna tofauti za kifalsafa.

Ukiondoa timing, kitendo cha rais kugawagawa pesa kila sehemu si sawa.

Kwani hakuna chama cha soka? Hakuna wizara?

Rais hafanyiwi auditing. Hiyo hela hatujui imetoka kwa walipa kodi au ni pesa aliyochukua rushwa kwa Adani.

Hilo nalo ni tatizo tayari.

Unaelewa hilo? Au unafurahia tu rais anatoa pesa?
 
Mkuu kichwani mwako mupo sawa lakini?
Zaidi ya sawa, mnaendeshwa na hisia na siasa uchwara na sio uhalisia.

Ni lini huyo raisi kaanza kutoa mamilioni kwenye mambo ya mpira wa miguu?? Kwani kaanza leo??

Ninyi wananchi sio watoa taarifa, sio wapigania haki zenu, sio washiriki kwenye uchaguzi ila ni mahiri kwenye kukosoa mitandaoni (keyboard worriers).

Vijiweni mnajadili simba na yanga, jukwaani humu mnakuja kummnanga raisi muonekane ni great thinkers. Shame on you
 
Hizo hela hajaanza kutoa juzi wala jana na si yeye tu hata mtangulizi wake ndivyo alivyokua na hiyo tabia haijakoma mpaka leo.

Kwamba akitoa hizo 700M ndio ataokoa watu kariakoo??
Hiyo ni mipango iliyotakiwa kupangwa kabla ya janga na majanga yafananayo na hayo.

Ila hii ya kusema sijui raisi katoa 700M kwa taifa stars huku katosa uokozi sio sawa, maana hata akitoa hizo 700M kwenye uokozi zitaishia kuliwa na wachache tu..

Sijui unaelewa.
 
Mungu alikuwa wapi kuzuia hilo jengo lisiporomoke?

Masikitiko mengi…..Mungu hivi Mungu vile.

Where was his ass in Seba’s hour of need?
Mungu kawapa akili, jinsi ya kuitumia ni maamuzi yenu ila mkimuomba atawasaidia.

Sasa ninyi ni viburi, much know a.k.a kajua yote
 
Sijasema hela kaanza kutoa leo.

Sijasema milioni 700 zitaokoa watu Kariakoo.

Sijasema angetoa milioni 700 Kariakoo.

Kariakoo kuna tatizo lililozidi pesa.

Milioni 700 katika hesabu za nchi ya watu milioni 65 si pesa nyingi hivyo.

Sijasema angetoa milioni 700 kwenye uokozi.

Huelewi point zangu. Ndiyo maana nikasema tuna tofauti z akifalsafa.

Kwanza, it was insensitive kutoa pesa kwenye mpira wakati watu wamefukiwa na ghorofa. Ni kama haku acknowledge kuwa lile ni janga la kitaifa.

Pili, habari nzima ya rais kugawagawa pesa ni kosa. Ndiyo maana naona hoja yako ya "kwani kaanza kutoa leo, kwani kaanza kutoa yeye" kuwa ni mufilisi. Ni hoja ya mtu asiyejua kusoma kwa ufahamu.

Maadam rais hafanyiwi auditing na CAG, rais kutoatoa pesa ni makosa. Pesa za rais hazina transparency. Tutajua vipi hizi ni pesa za walipa kodi na si pesa za rushwa ya Adani? Nimekuuliza hili swali hujajibu.
 
Ni wakati sasa na wapangaji kwenye hayo majengo kuchukua hatua kwa matengenezo wanayo ona yanaweza kuhatarisha uhai wao
Maana mnaona kabisa nguzo zinapigwa nyundo na nyie mpo ndani kimya tuu
Watu washaanza kuhofia juu ya kufanya biashara kwenye ghorofa. Wengine wanangojea mkataba uishe wahame.
 
Majanga kama haya hayana mbabe mkuu, kumbuka tetemeko la uturuki, ghorofa la floors kumi unadhani watafanyaje ili kuharakisha uokozi?
Kwa akili km zako lzm waafrika tutawaliwe Tena , badala ya kuhimiza maboresho kwenye taasisi husika , ww ndo kwanza unawapa hamasa kuwa hakuna namn ya hv walivyoperfom kwenye hili jengo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…