Sebastian Haller, mchezaji wa Ivory Coast akipokelewa klabuni kwake baada ya kushinda AFCON

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Sebastian Haller, mshambuliaji wa Ivory Coast aliyefunga magoli muhimu katika mechi za mwishoni zilizoipa Ivory Coast ubingwa wa AFCON 2023 amerudi kwenye klabu yake ya Borussia Dortmund na kupokelewa kwa staili hii.

Mchezaji wa AFCON wa nchi yako amepokelewaje aliporudi klabuni kwake?

Nikinukuhu maneno kuntu ya Erythrocyte "Mungu wabariki Wazungu"
 
Huwa wanapokelewa hivyo waliochukua ubingwa au kuwa second na third runner we mtu katoka round one apokelewe na maua
Anyway hapo Cha ajabu ni aliyeshinda ubingwa kaisharudi kazini waliotolewa huko mbali hata hapajulikani hadi Leo hawajaanza kazi na wamerudi juzi
Not serious
 
Wachezaji wetu sasa utasikia klabu ikitoa taarifa.

"Fulani na fulani waliokuwa kwenye timu zao za taifa WAMEJIUNGA NA WENZAO KAMBINI"

😂
 
Sebastian Haller, mshambuliaji wa Ivory Coast aliyefunga magoli muhimu katika mechi za mwishoni zilizoipa Ivory Coast ubingwa wa AFCON 2023 amerudi kwenye klabu yake ya Borussia Dortmund na kupokelewa kwa staili hii.

View attachment 2905403
Mchezaji wa AFCON wa nchi yako amepokelewaje aliporudi klabuni kwake?

Hivi ni member gani yule wa JF alikuwa kwenye post zake anamalizia kwa "Mungu wabariki Wazungu?"
Dortmund ya kibabe
 
Alistahili afanyiwe mapokezi mazuri,kwanza alipambana na kuishinda Cancer,akarudi Uwanjani na kuifungia Timu ya Taifa magoli muhimu kwenye Nusu Fainali na Fainali,hakika alistahili mapokezi mazuri
 
Sebastian Haller, mshambuliaji wa Ivory Coast aliyefunga magoli muhimu katika mechi za mwishoni zilizoipa Ivory Coast ubingwa wa AFCON 2023 amerudi kwenye klabu yake ya Borussia Dortmund na kupokelewa kwa staili hii.

View attachment 2905403
Mchezaji wa AFCON wa nchi yako amepokelewaje aliporudi klabuni kwake?

Nikinukuhu maneno kuntu ya Erythrocyte "Mungu wabariki Wazungu"
Hapo ''Majini'' hamna.
 
Back
Top Bottom