Sebuleni kunakaa TV na makochi pekee hivyo vingine vyote ni uchafu

Usitupangie wengine tukilala tunaona utajiri wetu woteπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜ƒ
 
Hata hii picha uliyotupia bado ina makorokoro mengi na haina nafasi. Cha muhimu kila mtu aishi kulingana na kipato chake. Kuna walioiga kupanga nyumba nzima wameishia kuwa watumwa wa wenye nyumba.
 
Hata hapo kwenye picha mbona kumejaa vitu vingi. Kwa mfano mbali na makochi na Tv ninaona hivi vitu pia kwenye hiyo picha;
1. Maua
2. Makabati
3. Mavyungu ya urembo
4. Mavioo
5. Friji
6. Majagi ya umeme
7. Mataa taa ya urembo
8. Mito ya urembo
9. Mazuria
10. Stendi/meza ya kioo.
 
Pia yawe rafiki kwa mgegedo kuna muda watoto hua likizo kwabibi na bint wa kazi

Wakezetu wanaweza kunjiwa hapohapo na asante ikatolewa tena tokamoyoni sio ya

Kubumba
 
Sawa mkuu ila hayo maisha Kwa sie tunaojitafuta ni ngumu kidgo
Apa na comment huku nimekaa ghetto kwangu juu ya java la maji ya kunywa
 
Sebuleni kwangu ndo parking ya bodaboda yangu
 
Mbona hapo sioni kabati la vyombo, friji, redio home sieta wala visturi?
Sebule gani hiyo?
 
Maisha hayafanani kati ya mtu na mtu.
Ni utofauti wa kipato
 
Wengine wanatia aibu, vyumba vyao ni kama karakana, wamejaza vitu mpaka inachukiza
 
pambana yamkini utatimiza ndoto yako mkuu
 
Kuwa na kwako upafanye hivyo na sio kutupangia sisi.
 
Duniani tunapita tu, sasa kuna haja Gani hata ya kuwa na hiyo sebule njiani?
 
Nilisikia kwamba watu wengi bongo tunalala na kuishi stoo
 
Basi hakuna namna zaidi ya kuikataa CCM na vyama vyote vya upinzani, Tanzania inahitaji vijana wa 90s kuikomboa kutokaa kwa mkoloni mweusi
 
Usikariri.

Wengine hawana makocha wana mazulia na mito.
Wengine wana kila kitu sehemu moja.

Muhimu kwenye sebule ni mpangilio tuu.
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…