Security alert kwa Serikali yetu: Tuwe makini sana na Marekani, kuna kitu kinapangwa halafu wajifanye walionya kabla. Je, wanapanga kutu-Libya?

Watu wanajitoa uelewa.

Kama wanao to begin with.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajitahidi kama jina lako lilivyo,muhula nduo umeisha, sasa hivi no uteuzi tunaanza kampeni sasa
 
Mitanzania mijinga sana yaani hata kujifunza kwa waloharibiwa nchi zao kwa hila ka hizi(Libya) .. Endeleeni kushadadia tuu ujinga mkidhani marekani anajali hii nchi..
Nyie ngojeni tuuu si mnajifanya wajingA

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona nchi yetu imekewishaharibiwa tayari na Dikteta Uchwara? Nini kimebaki Tanzania baada ya miaka 4 ya JPM? Umaskini inaongezeka, uhuru tulioutaka toka kwa mkoloni umeondewa, manyanyaso kutoka kwa kikundi kidogo ndiyo yametawala.
Mkoloni wa Chato ni mbaya kuliko Mkoloni wa London.
 
Natamani hao Usalama wa Taifa ndio wawe wa kwanza kukamatwa na kuning'inizwa kichwa chini miguu juu ili watie akili
 
Makamu wa Rais ni Muislamu na Waziri Mkuu ni Muislamu lakini hawa ni mapoyoyo tu wala hawashiriki kwenye maamuzi mikubwa ya nchi. Maamuzi makubwa ya nchi ni 'One Man Show' sana sana anaweza shiriki Makonda au Palamagamba.

Kusema Serikali haina mfumo Kristu kwa sababu ya hawa Majaliwa na Samia ni changia la macho.
 
Nakazia kwa zege la madaraja yanayokatiza baharini.
 

Hiyo ndiyo habari kubwa. Kama Mkapa anasema hayo basi ujue yuko pissed off kuliko hata huyo Yusuf Makamba na Absulrahman Kinana. Magufuli mwisho Octoba 2020, akilazimisha tu atadhalilishwa kama Laurent Bagbo wa Ivory Coast mwaka 2012
 

Kwasababu ya chaguzi 2015 hasa Zanzibar na uchaguzi wa serikali za mitaa . Game nzima wamezijua sio wenyewe tu bali upinzani. Zitto mfano kitu kimoja alichowaambia wadhamini ni kwamba kukitokea mauaji wasiingizwe huko maana yake serikali pekee ndiyo itaonekana imesababisha fujo. Vilevile serikali ikikataa tume huru ambayo ubalozi wa US wameandika barua maana yake US wanaweza kufanya lolote na kibaya zaidi 50% hawata support serikali kama uchaguzi hautakuwa wa haki. Hata kama 40% kama ya 2015 hatutakuwa na umoja wa kitaifa ndani hivyo hatutaweza kupigana na vikwazo. Hakuna nchi iliyoshinda vikwazo hata Russia ni mafuta tu uchumi una sua sua sana. Uzoefu wa kimataifa ni tatizo hapa na usikivu wa serikali wasitumie historia wakati huu haiwezekani. Yaani sasa hata wazazi wetu kuja kusalimia US na sheria mpya hii haiwezekani! tumeshaanza kupata shida kwasababu ya sera zetu
 
Kwa uandishi wa Pascal Mayalla , the line between satire and reality isn’t so clear. Expect puzzlement.

Jitahidini mumuelewe
 
Yawezekana hoja ni muhimu lakini ilivyoandikwa, ni vigumu kuamini imeandikwa na yule Mayala wa zamani.
 
Tuache upuuzi wa kusingizia mataifa ya kigeni kama chanzo cha matatizo yetu.

Cha msingi tuzungatia haki za binadamu, uhuru wa maoni ya watu, demokrasia ya kweli, n.k. Mengine yote ni upuuzi.

Ukiamua kujitumbukiza kwenye Ziwa ili ufe, hatuwezi kuyalaumu maji.
 
Tanzania haina umuhimu kivile kwa Marekani mpaka Marekani ianze kufikiria suala la ‘regime change’.

Mnajipa umuhimu ambao hamna mbele ya Marekani:
Wewe ni mgeni kwa sera na mikakati ya Marekani? Au unajitoa ufahamau kwa vile ni mnufafaika wa mfumo kandamizi wa Jiwe. Kama Marekani inaweza ikaitangazia dunia kuwa imezuia Paul Makonda na mke wake wasiende Marekani, Je kati ya Tanzania na Makonda nani ni sensitive kuliko mwenzie?

Hebu shirikisha ubongo unapochangia hoja kuliko kuviacha vidole vitembee kwenye keyboard.
 

Sijaelewa ulichokiandika!

Jaribu tena.
 
Nitajie hao Waislamu 2 Majaliwa na Samia nini wamewahi kufanya au ku-influence? Hao ni danganya toto tu, kukubwa wanachofanya ni kuhudhuria mkutano ya nje ya Tanzania ambayo yeye haendi. Kimsingi Makonda na Kabudi wana nguvu ya maamuzi kuliko Waziri Mkuu na Makamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…