Sehemu ambazo CAG haruhusiwi kusogelea: ATCL na Wakala wa Barabara - TANROADS. Unajua kwa nini?

Wajinga wanashangilia badala ya kujiuliza kulikoni mambo haya!!!
 
Mbunge ahoji kwanini CAG hajafanya ukaguzi ATCL, Tanroads

Mbunge huyo amehoji akitaka kujua ukaguzi huo uelezwe kwanini haujafanyika ili isije ikawa hela zinapigwa

Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde amemtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kueleza sababu za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutofanya ukaguzi katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na Wakala wa Barabara (Tanroads).

Akizungumza katika mjadala wa bajeti hiyo leo Jumatatu, Aprili 23 bungeni mjini Dodoma, Silinde amesema, “Kuna usiri gani wa kuleta taarifa ya ukaguzi wa ATCL bungeni. Isije kuwa tunapigwa fedha kupitia shirika hili. Tunataka waziri atueleze sababu ni nini?

“Pia ukaguzi wa Tanroads nao hauonekani na kuna taarifa huko mitaani kuna miradi hewa ya barabara iliyogharimu Sh282bilioni, tunataka kujua thamani ya barabara zinazojengwa kupitia ukaguzi wa CAG. Mtueleze kwanini hauletwi hapa bungeni.”

Kwa mfano: Hii Kampuni iliyokula Bilioni 14 bila kujenga hata mita moja pamoja na umuhimu wa barabara ya Makutano, Natta, Mugumu, Loliondo mpaka Mto wa Mbu kwa utalii Serengeti ndio imejenga Chato Airport, unajua kwanini?

View attachment 1245587

ATCL na Tanroads ni makazi ya Malaika mkuu! CAG ni nani hata aweze kusogelea makao matakatifu!
 
Hili donge kwa maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya 5..
 
Profesa Makame Mbarawa ni waziri wa ujenzi? Eti huyu ndiyo akili kubwa ya chadema anayetegemewa ni aibu.
Soma vyema. Hiyo ni sehemu ya mchango wa Mbunge Silinde Bungeni wakati uliopita. Punguza kukurupuka na kuona umepata cha kukosoa. Jibu hoja: kwanini ukaguzi wa CAG haufanyiki ATCL na Tanroads?
 
Mbunge ahoji kwanini CAG hajafanya ukaguzi ATCL, Tanroads

Mbunge huyo amehoji akitaka kujua ukaguzi huo uelezwe kwanini haujafanyika ili isije ikawa hela zinapigwa

Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde amemtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kueleza sababu za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutofanya ukaguzi katika Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na Wakala wa Barabara (Tanroads).

Akizungumza katika mjadala wa bajeti hiyo leo Jumatatu, Aprili 23 bungeni mjini Dodoma, Silinde amesema, “Kuna usiri gani wa kuleta taarifa ya ukaguzi wa ATCL bungeni. Isije kuwa tunapigwa fedha kupitia shirika hili. Tunataka waziri atueleze sababu ni nini?

“Pia ukaguzi wa Tanroads nao hauonekani na kuna taarifa huko mitaani kuna miradi hewa ya barabara iliyogharimu Sh282bilioni, tunataka kujua thamani ya barabara zinazojengwa kupitia ukaguzi wa CAG. Mtueleze kwanini hauletwi hapa bungeni.”

Kwa mfano: Hii Kampuni iliyokula Bilioni 14 bila kujenga hata mita moja pamoja na umuhimu wa barabara ya Makutano, Natta, Mugumu, Loliondo mpaka Mto wa Mbu kwa utalii Serengeti ndio imejenga Chato Airport, unajua kwanini?

View attachment 1245587
Ni wi, wizi wizi tuu
 
Back
Top Bottom