Sehemu gani nzuri Kwa Dar es Salaam Ya kutoka na Mpenzi?

Ngoja nijaribu kukuwekea maeneo ambayo yatakuwa ndani ya budget yako na pia nimezingatia utulivu..

1. Terrace Lounge Rooftop (Msasani Mall, karibu na Oysterbay Police)

2. G’eez Hangout - Restaurant & Pizza (Mbezi Beach karibu na kona ya kwenda Shoppers)

3. Trust The Kitchen Restaurant (Noble Center Victoria mataa ya kona ya kwenda Mwananyamala Hospitali, zamani Istana)

4. KingJada Hotels (Morocco mataa,hii bado ni mpya, upande wa restaurant pana upepo mzuri ukikaa outdoors ingawa wana indoor pia)

5. Jacques Salad and restaurant (Mikocheni mtaa wa Chato, barabara mpya ya zege inayounganisha ilipokuwepo AAR zamani na kijiwe maarufu cha msosi Container)

6. Salt Restaurant (Masaki jengo walipo Tembo Nickel )

LIst ni ndefu lakini jaribu hizi kwanza...
 
Nimemuwekea list kwa kuzingatia budget , msosi mzuri na utulivu (sijazingatia music kwa sababu sehemu nyingi zenye chakula huwa hawajali sana muziki, sehemu zenye masanga ndio hujali muziki)..
Nimeona, Utuwekee na sisi ambao hatupendi independent restaurants kama hizo. Tunapenda restaurants za kwenye hotels.. Mfano same hotel kuna different restaurants. Leo unajaribu hii kesho ile.

Hivi Terrace bado panabamba? Sarah anajitahidi sana.
 
Nimeona, Utuwekee na sisi ambao hatupendi independent restaurants kama hizo. Tunapenda restaurants za kwenye hotels.. Mfano same hotel kuna different restaurants. Leo unajaribu hii kesho ile.

Hivi Terrace bado panabamba? Sarah anajitahidi sana.

Hii list nimezingati mandhari tofauti, utaona nimetupia kiota kipya hapo cha Jadda Hotel pale Morocco kwa sababu ya mandhari ya hoteli, au Terrace ambapo kutakuwa na choices za misosi ya kibongo bongo, Jacques kutakuwa na greens, Salt na G'eez misosi ya kitasha n.k

Terrace bado ni choice nzuri kwa sababu pana utulivu, rooftop unapigwa na upepo natural, pana privacy.
 
On my bucket list , Will try king Jada na Salt.

Thank you.
 
Njoo twende nikupele ukale calamari na prowns popcorn
Mbona hata wewe unazo
 
Shukurani mkuu, ngoja nione nitachagua wapi.
 
Nenda hapo slipway au Sin club ya Jeshi lakini hiyo pesa hautoboi.
 
Slipway kungekufaa sana
 
Kama ni mzee wa kufukia sana.
Chimbo hilo hapo nadhani sahivi ni 27k per person kuna nyama za aina zote ispokuwa kitimoto, na mazaga zaga kama yote,

Mchawi njaa tu maana ni kila after dk 2 sahani zinapita, kwahyo timing muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…