Sehemu gani nzuri ya starehe Mwanza?

Sasa mtu anayekujua anakubambiaje kiasi hiko kama sio mpenzi wako? Mimi nimefika chuo welcome first year,demu kaniomba nikambanbie nikakataa,ila siku hizi? Nipo tayari kutoa hela kwa ajili ya kubambia tu..Ndio fanya mpango uwe unatoka,kama una maisha ya home-kazini-home ni maisha yanayoleta upweke sana sometimes.Kama upo Mwanza Malaika nadhan patakufaa sana,hizo chai unazotaka zipo,ice cream pia.Then unaweza kwenda Cinema kama unapenda.
 
Ingia club elevate, hutojutia
Tatizo la mwanza haina choice pana za viwanja vikali vikali.

Ukiwa mwanza una wigo mdogo mno wa kuchagua viwanja vya maana.
hayazidi machaguo manne ya viwanja vikali.

Athari yake ni kwamba; ukiboreka na pub A, B, C, na D hakuna choice E, nk

Hata hiyo villa park nayo imefunguliwa tena juzi tu..lakn kuna wakt ililazimika kufungwa kwa sabab ya cris ya wateja.

Chaguo la site ya jembe ni jembe halipo tena.

Afterall mwanza haina wanywaji..
sijasema haina wadau wenye hela, N0.
Nachomaanisha mwanza haina watu spendful.

Watu ambao wana character za 'kutumia' wapo kahama na geita isipokuwa wanaponzwa na udogo wa miji yao.

Nje ya wikend, mwanza Ukienda pub nyingi saa 4 utakuta meza kibao zipo vacant.
 
Hii tabia ya meza kuwa reserved niliiona Bambalaga Dodoma, siku moja niko pale nakula vyangu pole pole mara mhudumu anatundika mezani kwangu bango table reserved, nikamwabia sitataka usumbufu maana nimekuta meza tupu haya ya reserved sitak kuja sumbuliwa, akanambia haina shida boss nikaona lile bango pale mezani limepotea.
 
Ulitakiwa umlambe na kofi juu huyo
 
Kweli mkuu ila haya mambo ni mazoea, sasa hivi ka uwezo ninako naweza enda sehemu yoyote ila najikuta ijumaa jioni niko busy kuandaa kazi za j3 eti najikuta nimechoka naenda nyumbani.

No no this xmass kama sitosafiri sehemu zote za maana nitafika.wenda na mazuri yote nikakutana nayo huko huko.
 
Jitahidi mama,wanasema ukiwa unatafuta maisha usisahau kuishi...vunja mfupa angali meno bado yapo.Lakini huna marafiki wakuzoeshe night life? Haya mambo yanaenda sana ukiwa na influence.
 
Jiji ni moja tu Daslam
 
Alikupeleka middle class unapomfata mwambie kabisa unataka level ip isitoshe huyo sio mwenyeji kakpeleka hit za zamani

tutajie basi hit za kisasa, me karibia kila weekend nipo pale, hata mimi sielewi elewi, mpaka nawaambiaga masela wangu tusiwe tunalala tuwe tunaamsha, mbelembele...
 

Atakwambia pale roundabout kwenye ile hotel chini....au Delmonte juu ghorofani...
 
Sehemu za starehe utegemea unachopenda. Kuna watu wanapenda sehemu tulivu, kuna watu wanapenda vurugu na amshaamsha. Hapo villa navyojua mimi kuna sehemu karibu tatu. Kuna sehemu ya music live, pili kuna sehemu mziki umetulia kwa juu. Kule wanakaa weye fedha yao. Na tatu kuna club huko vibe la nguvu. Yote haya ni ndani humo humo Villa. Kama hakujabadilika ndo villa ilivyo.
Ila Mwanza maeneo mengi ya kuvinjali ni yaliyo tulivu huku ukipata hewa mwanana toka ziwa victoria.
Mwanza hawana club za kujazana na makelele, imepitwa na wakati. Maeneo ya kujirusha ni mengi ila watu wanaustaarabu wao. Vibe zinatofautiana! watu wanakula life kinamna huku fedha inateketea.
Wengi uenda Kijereshi campsite maeneo ya Seregenti kula maisha. Mambo ya kujazana club mwanza naona hawana sana. Wanaoenda starehe zinazoongeza afya ya mwili. Si unaenda starehe unarudi nyang'anyang'a.
 
Mkuu embu tutafutane bhana tubadilishane mawazo,usiwe MTU wa ndani ndani kama utumbo
 
Vp hakuna alimaindi flag hiyo sehemu ya juu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ