Mwanza bwana mm sipaelewagi sijajua sababu sio mwenyeji ssna au ni vipi, nikifika hapo nikaulizia boda akasema villa park, nikasema twende aah kufika pale just live band na wanakata mauno yao pale jukwaani ndio la msingi (tofauti na hapo hakuna jipya), nikaambiwa kama unatakaa mziki mzuri toka hapo nje mkabala na villar park kuna club, nikaenda naambiwa elf 2 kuingia, nikalipia hahaha kufika pale mahali bwana bora kigodoro cha Kinyanya Kibiti huko kwanza hapako vzr, hapana mwanga, mvua kidogo ilipita panaloana kila sehemu nikaona jau nikanyanyuka nikatoka zangu nje, boda akasema pale daraja la furahisha pembeni ya rock city mall pana muzik pia na vyakula na pazuri sana nikasema twende, nikafika pale na penyewe kuna kajukwaa tu kadogo na muzik wa nje, na watu mnakaa kwenye viti hapo unaagiza unachokula unahudumiwa japo wahudumu wako slow, anyway nikaona nile ugali sato nikarudi hotel kulala.
Kwa kifupi sijapata kiwanja mwanza kinipe vibe la ukweli.
Labda mtu anambie hapa kipi kiwanja cha vibe mwanza tofaut na hizo nilizoenda