Sehemu gani nzuri ya starehe Mwanza?

Sehemu gani nzuri ya starehe Mwanza?

Mwanza bwana mm sipaelewagi sijajua sababu sio mwenyeji ssna au ni vipi, nikifika hapo nikaulizia boda akasema villa park, nikasema twende aah kufika pale just live band na wanakata mauno yao pale jukwaani ndio la msingi (tofauti na hapo hakuna jipya), nikaambiwa kama unatakaa mziki mzuri toka hapo nje mkabala na villar park kuna club, nikaenda naambiwa elf 2 kuingia, nikalipia hahaha kufika pale mahali bwana bora kigodoro cha Kinyanya Kibiti huko kwanza hapako vzr, hapana mwanga, mvua kidogo ilipita panaloana kila sehemu nikaona jau nikanyanyuka nikatoka zangu nje, boda akasema pale daraja la furahisha pembeni ya rock city mall pana muzik pia na vyakula na pazuri sana nikasema twende, nikafika pale na penyewe kuna kajukwaa tu kadogo na muzik wa nje, na watu mnakaa kwenye viti hapo unaagiza unachokula unahudumiwa japo wahudumu wako slow, anyway nikaona nile ugali sato nikarudi hotel kulala.

Kwa kifupi sijapata kiwanja mwanza kinipe vibe la ukweli.

Labda mtu anambie hapa kipi kiwanja cha vibe mwanza tofaut na hizo nilizoenda
Bro mimi nilikuwa natoka Musoma naenda Mwanza kula bata,lakini nikifika Mwanza nazunguka mjini saa moja tu basi nakosa pa kwenda,narudi lodge.
 
Bro mimi nilikuwa natoka Musoma naenda Mwanza kula bata,lakini nikifika Mwanza nazunguka mjini saa moja tu basi nakosa pa kwenda,narudi lodge.
Huwez amin nilijihisi bored sana mzee, jiji kali vile, milima imepamba jiji ila hakuna kiwanja cha kutikisa mtima tii tiii.

Ngoja nijaribu huko Malaika beach aliposema mdau nione kama kuna kipya
 
Hapo parkjng ya gari kila baada ya saa 1 ni TZS. 1,000.

Ukikaa masaa 5 unalipia 5,000 alafu local beer ni 4,000 na imported beer 6,000.

Si afadhali uende Malaika Beach Hotel
Ya kitalii ile hotel chumba cha kulala tu bei ya mwisho ni 270k nakuendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio utupe majibu hapa Mkuu, mfano hapo jengo la rock city mall mbona niliona parking zimejaa, kila anaezama ni ndinga unaanzAje kusema pa low class, pamoja na yote hayo ni paboooovu, taja hapa kiwanja hot Mwanza! Disco kali, vyakula full, ma Dj hot, na huduma mbali mbali. Otherwise utakuwa umeponda ila huna suluhisho
Viwanja vuruga kwa Mwanza ni Amy J, Diamonds, Las Vegas na Bundesliga. ...Viwanja standards Bonansera, Cask, Tilapia na Elevate
 
Hapo parkjng ya gari kila baada ya saa 1 ni TZS. 1,000.

Ukikaa masaa 5 unalipia 5,000 alafu local beer ni 4,000 na imported beer 6,000.

Si afadhali uende Malaika Beach Hotel
Hizi story Cask beer zote buku nne
 
Ulienda lini hapo?

Kabla ya kuungus wiki 1 bia walipandisha bei
Nilienda kitambo kidogo kabla haijauungua manz wangu aligonga savanna kwa buku nne nne sawa na mm niliyegonga guiness
 
Zamani kidogo shoga yangu alikuwa na graduation tumemaliza wakasema twende gold crest club kule underground si ndo mara ya kwanza naingia club!

Yesuuuu kuna baridi sio kwa Ac ile , kizuri pembeni kulikuwa na sofa safi mimi na shoga yangu hatutumii pombe tukakaa pale

Watu wanacheza mziki balaa watu wanatoka jasho mimi naskia baridi, nikaita mhudumu aniletee chai😂😂😂 akasema huko chini chai hakuna mpaka hotelini juu. Nikajisemea huu upuuzi gani nina hela yangu siwezi pata ninachotaka.
Kumbe club watu wanacheza na watu ambao hawawajui? Kha! Ile mishiko ndo sikupenda yaan zero sistance mmh

Mimi nimejikalia hapo naona vikaka vinakuja vinanishika eti tukacheze nikajisemea mimi sishikwe na mtu simjui😂😂😂 nisije shikwa na litoto lidogo.

Mara nikamuona mhudumu mtu mzima, kumbe meneja, nikamuuliza siweza pata maziwa akaniambia unataka sehem tulivu nikasema ndio. Akanielekeza kule juu, manina nafika huko nilkuta watu wa maana nikajisemea huku ndo dunia ilipo.
Kutupia jicho namuona waziri fulani wakati ule alikuwa mbunge, na vijana wake nikajisemea kumbe huku ndo wakubwa wanakaa. Sehemu ile nzuri kama unataka utulivu panafaa.
Nilienjoy ile sehemu. Nikaletewa nilivyotaka siku ikaisha.

Sema kitu nilichoona club ile ni sehem ya kutoa stress, watu kule wana raha sana.

Ambao hatutumii pombe kuna kitu tunakikosa, yaan kuna starehe tunaikosa.
 
Huwez amin nilijihisi bored sana mzee, jiji kali vile, milima imepamba jiji ila hakuna kiwanja cha kutikisa mtima tii tiii.

Ngoja nijaribu huko Malaika beach aliposema mdau nione kama kuna kipya
Malaika nilienda club elevate hakukuwa na vibe,watu wachache sana,juzi kati pia nilienda lakini nilikuta live band,pia watu hawakuwa wengi lakini nikiri nilienda mapema sana...ila hapo malaika jipange,bei za kitalii sana mkuu.
 
Zamani kidogo shoga yangu alikuwa na graduation tumemaliza wakasema twende gold crest club kule underground si ndo mara ya kwanza naingia club!

Yesuuuu kuna baridi sio kwa Ac ile , kizuri pembeni kulikuwa na sofa safi mimi na shoga yangu hatutumii pombe tukakaa pale

Watu wanacheza mziki balaa watu wanatoka jasho mimi naskia baridi, nikaita mhudumu aniletee chai😂😂😂 akasema huko chini chai hakuna mpaka hotelini juu. Nikajisemea huu upuuzi gani nina hela yangu siwezi pata ninachotaka.
Kumbe club watu wanacheza na watu ambao hawawajui? Kha! Ile mishiko ndo sikupenda yaan zero sistance mmh

Mimi nimejikalia hapo naona vikaka vinakuja vinanishika eti tukacheze nikajisemea mimi sishikwe na mtu simjui😂😂😂 nisije shikwa na litoto lidogo.

Mara nikamuona mhudumu mtu mzima, kumbe meneja, nikamuuliza siweza pata maziwa akaniambia unataka sehem tulivu nikasema ndio. Akanielekeza kule juu, manina nafika huko nilkuta watu wa maana nikajisemea huku ndo dunia ilipo.
Kutupia jicho namuona waziri fulani wakati ule alikuwa mbunge, na vijana wake nikajisemea kumbe huku ndo wakubwa wanakaa. Sehemu ile nzuri kama unataka utulivu panafaa.
Nilienjoy ile sehemu. Nikaletewa nilivyotaka siku ikaisha.

Sema kitu nilichoona club ile ni sehem ya kutoa stress, watu kule wana raha sana.

Ambao hatutumii pombe kuna kitu tunakikosa, yaan kuna starehe tunaikosa.
Aaash,joy ya club dada nikucheza na mtu usiyemjua...ukiwa na vibe huwezi hisi baridi kabisa,kuna wakati watu wanakuwa wengi AC inaelemewa...Watu tunatofautiana matakwa,mimi ungenipeleka hapo kwenye kahawa ningekununia.
 
Mmh mtu humjui akushike vile nilivyoona? Hiyo sikuipenda.
Ila wakiweka miziki ya kubanjuka basi watu wanaruka haswa.

Sasa wakati nataka kuanza kutoka hoteli za maana najua nikitoka na 50000 siwezi imaliza yaana kila ijumaa lazima nitaanza kutoka.nimechoka kukaa ndani, ni mimi kazini home, no nataka kuanza kujipa raha kubaki ndani kama kufuri hapana.

Tena sasa hivi ndo wakati mwafaka ila sio club ni sehemu tulivu za starehe. Naenda saa mbili saa5 narudi.
 
Back
Top Bottom