Sehemu nyingi za starehe Bongo ni za kawaida

Sehemu nyingi za starehe Bongo ni za kawaida

Sina tatizo na muonekano wa hizo sehemu ila kuhusu ma Dj nakuunga mkono, hawana exposure ya music, wanafungulia sauti kubwa, kelele tu, miziki nin ile ile tu ujinga mtupu.
Hakuna kitu nachukia kama makelele,mtu unajipigia beer yako DJ anafumua mziki utafikiri sijui mko Stadium kwenye concert ya mapipa band, wanaharibu sana starehe za watu
 
Let's say mimi ni DJ alafu anakuja DJ mwingine ananiomba External yangu kwenda kufanyia kazi sehemu utegemee atapiga nyimbo gani? Mostly ata search zile anazozijua tu kichwani mwake na zinazopatikana kwenye drive ndo ana load na kupiga.... Au anakuja ku copy mzigo wote kwangu ye hana hata nyimbo zake za tofauti utegemee nyimbo atakazo kua anapiga zina utofauti? Jibu ni uzembe wa DJ mwenyewe kutokua mbunifu na mwenye kujituma na si meneja mimi navyoona mbaya zaidi unakuta meneja nae kijana hajui nyimbo...

Sema mimi siwapagi kabisa hata External yangu hawa vijana ku copy muziki wengi wao wazembe kujituma na nina muziki ambao hata wengine hawana na huwa nikipiga kwa media/radio mpaka meneja ananiuliza "hizo nyimbo siku tegemea kama unazo na huenda ni wewe pekee ndo umewahi piga hizi nyimbo hapa radio toka ma DJ wengine wapite" so imagine meneja anakwambia hivo lazmia uongeze juhudi katika kazi na kua mbunifu zaidi wa kipekee..

Nashukuru Mungu mimi hii ni passion yangu kabisa na nilienda chuo/DJ Academy kuisomea kuongeza maarifa zaidi mbali na kua na taaluma nyingine niliyosomea, so huwa naifanya kwa kuifurahia na napenda muziki hasa wa zamani na napenda ma DJs wa zamani waliotutangulia kwa hii fani...
Safi sana mkuu. MaDJ wengi wa bongo itakua ndo michezo yao kupeana nyimbo na wanakua wamemaliza hawajiongezi. Unaweza zunguka bongo nzima usikute DJ anapiga Afro -house music wakati ni nyimbo tamu mno na lazma ushake ukiskia. Ni mara moja tu nimewahi sikia sehemu pub moja kule Goba wanapiga Afro house music tena napo walikua wamedownload playlist ya Black coffee ambayo naijua aliifanya kwenye concert Tomorrowland Belgium ila nilienjoy na nikawaona wajanja sana 😆😆
 
Na vingine kiasi ila kwangu burudani kubwa sehem kama hizo huwa ni DJ mixing/playlist,huwa nikikuta DJ mkali naweza nisichomoke. Kuna siku ilikua week day pale wavuvi camp mida ya jioni tu DJ mkongwe Peter Moe alikua anapiga flash back zilikua tam sana,badae akamuachia dogo mmoja hivi basi yule dogo akaja na code zake za kitaa DJ Peter Moe akamfuata akamnong'eza kitu dogo akarudi kwenye track. Asikwambie mtu DJ Peter Moe anajua sana japo umri umekimbia
DJ Peter Moe, DJ JD (John Dilinga), DJ PQ na wengine wachache Hawa jamaa wakongwe toka enzi za kutumia masanturi wanajua nini maana ya kuburudisha mtu au watu wanataka nini kwenye kiwanja cha burudani toka clubs kongwe za enzi hizo wao ndo walianza nazo so wana uzoefu na kazi yenyewe lazima mtu usiwe nao shaka ukiwa kiwanja anapopiga..... Flash Back huwa tamu sana aisee askwambie mtu, zina radha yake.
 
Ukiachana na Haile salasie strip, ambazo kuna Elements, SamakiSamaki na sehemu nyingi zengine za starehe. Clubs kama Maison na Havoc, Tips na wavuvi camp.

Sehemu kwengine Most ni average hata Bar iwe nzuri vipi. Kwanza the selection ya music ni ileile, Ma dj wanapiga nyimbo zile zile trendy Wala hawana exposure za mood na upana wa muziki.

Ila ndio hivyo consumers wengi wa Tanzania hawana exposure, hivyo ndio maana watu hawapo aware. Wamestuck na subpar music and a whole concept of fun.
Sema sehemu ulizoenda ndio hazina utofauti, utakuwa huijui dar vizuri
 
DJ Peter Moe, DJ JD (John Dilinga), DJ PQ na wengine wachache Hawa jamaa wakongwe toka enzi za kutumia masanturi wanajua nini maana ya kuburudisha mtu au watu wanataka nini kwenye kiwanja cha burudani toka clubs kongwe za enzi hizo wao ndo walianza nazo so wana uzoefu na kazi yenyewe lazima mtu usiwe nao shaka ukiwa kiwanja anapopiga..... Flash Back huwa tamu sana aisee askwambie mtu, zina radha yake.
Sure,DJs wa zamani wanajua sana aisee sio wavivu kuexplore na wanaexposure sana
 
Safi sana mkuu. MaDJ wengi wa bongo itakua ndo michezo yao kupeana nyimbo na wanakua wamemaliza hawajiongezi. Unaweza zunguka bongo nzima usikute DJ anapiga Afro -house music wakati ni nyimbo tamu mno na lazma ushake ukiskia. Ni mara moja tu nimewahi sikia sehemu pub moja kule Goba wanapiga Afro house music tena napo walikua wamedownload playlist ya Black coffee ambayo naijua ila nilienjoy na nikawaona wajanja sana [emoji38][emoji38]
[emoji23][emoji23][emoji23] Sio itakua ndo kinachofanyika hata sasa kwani nipo kwenye hii carrier naelewa kinachofanyika, huwa nalaumiwa sana na hawa vijana kwamba mimi mchoyo wakisikia kuna ngoma nazipiga radio na wao hawana basi lazima nikute nimetafutwa kwenye simu " Oya mwana hizo ngoma ulizopiga hapo radioni naomba nije ungei basi mimi sina [emoji23]" hawajui nmezipata kwa tabu au nmenunua exclusive package kwenye online DJ Pool.. Wao wanapenda vya kushare hovyo tu hawapendi kuwekeza pesa ili kupata upekee katika kazi zao...

Mfano, siku izi DJs wengi wa HipHop wanapiga HipHop laini hizi wanaita HipHop biashara za kina Bando MC, Boshoo Ninja, Manengo, Young Lunya, Kontawa, Tanna, Rosa Ree na wengine hawa wasanii vijana wa kizazi kipya wanao rap, Kupata DJ ambae ana ngoma za HipHop NGUMU za enzi hizo kina Nash MC, Chabba, Nikki Mbishi, P The MC, Dark Master, Black Spear, Chid Benz, Songa, Stereo, Ghetto Ambassador, Chiku Kee, Cjamoker, Deddy n.k ni tizi wengi hawana kabisa na hawana idea nazo kabisa ila ndo HipHop halisi ya TZ ukisikiliza Classic HipHop ya Bongo ya enzi hizo kina Fid Q wanaimba mpaka unawaza walikua wanatoa wapi tungo zile za kipekee na zina ujumbe mzuri sana....
 
Mambo ya starehe mpaka masaki na posta yalikuwa zamani...siku hizi popote penye pisi kali na serengeti lite na misosi...mziki sio issue sana tunaunganisha Bluetooth tunasikiliza tunachotaka...siku hizi sio siri uswazi patamu kuliko ushuani
 
[emoji23][emoji23][emoji23] safi sana..

Yaah kikubwa upate burudani... it's good kama umeenjoy,mi pia kuna miziki huwezi kuta naiskiliza ila nikiona watu wanacheza naenjoy
yani nilicheka nikapafurahia sana yani hawana habari wanacheza wana enjoy ilibaki kidogo nikajiunge ila muda ukawa umenitupa mkono
mwaka mpya ntakua mgeni wao 😂
 
Ukiachana na Haile salasie strip, ambazo kuna Elements, SamakiSamaki na sehemu nyingi zengine za starehe. Clubs kama Maison na Havoc, Tips na wavuvi camp.

Sehemu kwengine Most ni average hata Bar iwe nzuri vipi. Kwanza the selection ya music ni ileile, Ma dj wanapiga nyimbo zile zile trendy Wala hawana exposure za mood na upana wa muziki.

Ila ndio hivyo consumers wengi wa Tanzania hawana exposure, hivyo ndio maana watu hawapo aware. Wamestuck na subpar music and a whole concept of fun.
Kwenye Ishu ya Music kuna TATIZO kubwa sana.. Kuna sherehe moja nilienda aisee DJ hana content, ikabidi niingilie Show, huwezi amini kila mtu ana SHAZAM nyimbo kila nikiweka CHUMA watu wanahipe! Baadae nikachek hadhira yangu nikaona kuna watu wa 80s - 90s nikashusha THROWBACK jams... Bhanaaa wee mbona na MBUSUSU nilipewa.
 
Ukitaka kunifukuza sehemu nianze kusikia amelowaaa amelowaaa! Unakuta Dj ndio wanasema top kwasasa ila anapiga zile zile trending hadi baa za vichochoroni! Siku hizi kupata nyimbo ni rahisi sana, why usipate time kusikiliza vitu vipya hata mastation kama Hot 99.5 usikie mangoma makali, style za mixing uwape vitu vipya wateja!

Ukitaka kutoka nenda wanakopiga Djs wakongwe ndio utapata taste tofauti huku kwingine ni kama wameridhika na vibe la walevi ambao wakishalewa wanacheza kila nyimbo. Kuna watu wengine hawatumii kilevi zaidi anaenda sehemu kutuliza nafsi na good taste of music! Sio makelele na dj kupanda juu ya meza kukata viuno!
 
DJ Peter Moe, DJ JD (John Dilinga), DJ PQ na wengine wachache Hawa jamaa wakongwe toka enzi za kutumia masanturi wanajua nini maana ya kuburudisha mtu au watu wanataka nini kwenye kiwanja cha burudani toka clubs kongwe za enzi hizo wao ndo walianza nazo so wana uzoefu na kazi yenyewe lazima mtu usiwe nao shaka ukiwa kiwanja anapopiga..... Flash Back huwa tamu sana aisee askwambie mtu, zina radha yake.
Ukienda pale The marz au zamani club regends Kwa John dillinga...aisee Kuna ngoma Kali sana ingawa nyingi za zamani lakini it's hot Sana...ma DJs wa zamani wanajua sana
 
Yaani ovyo kabisa,kuna wakati unatupa macho unaona bar imejaa watu wazima tupu kwa muda huo ila Dj kakomaa na nyimbo za bongo flavor badala ya kupiga nyimbo kulingana na umri na hadhi ya wateja kwa muda huo
Mdj wetu wanapiga nyimbo wanazopenda wao hamjawastukiaga Tu.

Ndio maana wengine tunamuwelewaga Sana John Dilinga na project zake za oldies.

Nikienda pub za kawaida live band inabonda nyimbo za copy naenjoy kuliko kwenda club Kwa sasa, utalazimishwa kucheza nyimbo za wavuta cocaine wa ulaya wakati hazina mzuka wowote ila watu wanafuata mkumbo wa madj tu.

Ukiwa umefuta tongotongo umetembeatembea kidogo Kwa wenzetu mamtoni kuna mziki unaujuwa kabisa huu ni wa wavuta cocaine tu, mziki siyo reggae siyo Rnb, siyo Pop wala siyo hip-hop, wala siyo country unakufurahisha nini kama siyo kufuata mkumbo tu?
 
Halafu aliyewaambia maDj ikifika sasita waanze kupiga amapiano mpaka asubui sijui ni nani?
 
Halafu aliyewaambia maDj ikifika sasita waanze kupiga amapiano mpaka asubui sijui ni nani?
Hayo ndio mambo yamenikata stim kabisa za kwenda disco Tec za Bongo.

Badala ya kupoteza muda wako na hao wapuuzi unaweza kwenda kukonga nyoyo Kwa Wacongo na kuburudika na miuno ya standard gauge na masebene ya kufa mtu.
 
Back
Top Bottom