Maana yake ni kuwa kama inaonekana itakuwa fujo, basi kusiwe na majengo ya kuabudia ya dini yoyote airport ili kuondoa upendeleo kwa dini fulani (ya mtawala)
Huu utatuzi ni simple and clear.
Ila watu fulani hawautaki kwa sababu wanataka kujiweka juu ya dini nyingine.
Tatizo la dini ni kwamba, ukishaamini dini yako ndiyo ya kweli, unawabagua watu wengine na dini zao kwa kuona hawa hawaijui dini ya kweli.
Unakosa hata kuwa na ukarimu wa kusema na hawa nao ni watu wanahitaji kuabudu kama mimi.
Hapo ndipo utaona mtu anayeamini Mungu, imani yake hiyo ya Mungu inavyoweza kumfanya awe mbaguzi asiye na upendo kwa watu wengine, hususan wasio wa dini yake.
Kifupi utaona jinsi dini, kitu ambacho kinanadiwa kuwa na lengo la kusambaza upendo, inavyoleta ubaguzi na migogoro.
Ndiyo maana wengine tumezikataa hizi dini.
Tunaona wazi hata hao walio na dini ambao wanatakiwa kutuonesha mfano wa upendo wanavyobaguana kati ya dini na dini, na hata ndani ya dini utakuta madhehebu kibao.
Yani hata hao Waislamu kuna migogoro ya madhehenu huyu Shia, huyu Sunni, kila mtu anavutia kwake.
Dini ni ubaguzi mtindo mmoja.