Seif Gulamali azungumzia mafanikio ndani ya miaka miwili ya Rais Samia katika Jimbo la Manonga

Seif Gulamali azungumzia mafanikio ndani ya miaka miwili ya Rais Samia katika Jimbo la Manonga

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Jimbo la Manonga Wilaya ya Igunga, Mhe. Seif Khamis Gulamali ameainisha miradi ya Elimu na Afya ambayo imefanyika jimboni kwake huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupeleka fedha.

WhatsApp Image 2023-04-04 at 09.42.52.jpeg

Jimbo la MANONGA Wilaya ya Igunga lilipokea Jumla Shilingi 543,400,000/= fedha za mradi wa Boost Shule za Msingi kwa mchanganuo ufuatao;

1. Kata Mwashikumbili. - Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Kijiji cha MATINJE namba 6 Mkondo 1, Milioni 361,000,000/=.

2. Kata Igoweko Kijiji cha MWINA Shule ya Msingi Selegei - Ujenzi wa Vyumba 4 vya Madarasa, Milioni 104,000,000/= na Ujenzi wa Vyoo Matundu 3 Milioni 6,600,000/=.
WhatsApp Image 2023-04-04 at 09.42.53(2).jpeg

3. Kata ya Simbo Kijiji cha Simbo Shule ya Msingi Ushirika - Ujenzi wa Madarasa 2 Mapya ya Awali ya Mfano, Milioni 71,800,000/=.

Zanahati ya Chapela Jimbo la Manonga limepokea fedha Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kupaua, kupiga lipu, kuweka dari (jipsambodi), kuweka vigae, kupiga rangi, kuweka mfumo wa maji, kuweka mfumo wa umeme, kujenga kichomea taka, kuchimba na kujengea shimo la kondo, kuweka madirisha grili, kuweka madirisha ya aluminiam, kujenga vyoo matundu 5 ikiwemo bafu na choo cha wenye ulemavu.

Zahanati ya Imalilo Jimbo la Manonga lilipokea Shilingi Milioni 75 kwa ajili ya Zahanati ya Imalilo ambapo Milioni 50 ni kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo na Milioni 25 kwa ajili ya Ununuzi wa Vifaa Tiba ambapo jumla 75 milioni iliingia Katika Akaunti ya Zahanati.
WhatsApp Image 2023-04-04 at 09.42.55(1).jpeg

Kazi zilizofanyika ilikuwa ni pamoja na Kufumua bati na kuweka bati mpya na Mbao Mpya, Kuweka Dari, Kuweka Vigae, Madirisha ya Aluminiam, Kuweka Frem za Grill, Kupaka rangi, Kujenga Vyoo Matundu 5, Kuweka Mfumo Maji na Kuweka mfumo Umeme.

Katika hatua nyingine Mhe. Seif Khamis Gulamali amezungumzia Ujenzi wa Daraja la Mondo katika Mto Manonga ambalo limekamilika kwa Shilingi Milioni 420 huku Serikali ikiwa imetoa Shilingi Milioni 500.
WhatsApp Image 2023-04-04 at 09.42.53(1).jpeg

Mhe. Seif Khamis Gulamali ametoa pongezi kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kushusha fedha hizi ambapo ameahidi kazi itakamilika Kwa Wakati ikiwa ni pamoja na Kata ya Ziba Kituo cha Afya na Sekondari ya Ziba.
 
Nonsense! Haya yamefanuywa na Kodi za watanzania wakiwemo wana-Igunga. Mbunge anayemshukuru rais kwa kazi ambazo ni majukumu yake (rais) ya kawaida hajitambui .

Tuna wabunge wajinga Sana nchi hii kama huyu wa Igunga.
 
Back
Top Bottom