Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Mleta mada..
Naomba kufahamu kama umesoma special school?
Kama ulipata alama za kukokoteza huwezi soma huko.
 
Zilikua zinasaidia kutoa top 10 tu. Baada ya hapo hakuna jipya .
 
Hii mada inarudiwa Kila baada ya muda humu.

Hoja hii ni Sawa na ile inayojengwa na Dotto Magari kuwa degree hazina maana yeyote kwakuwa wenye degree hawana hela!

Trust me, 80% za PhD Tanzania zimetoka shule hizo. 80% ya policy makers wamepita shule hizo!

Lakini liangalie kwenye context ya uchumi wa nchi husika! Tuna nuclear scientists Tanzania Mfano Mohammed Gharib Bilal aliyekuwa makamo wa RAIS, je wamegundua Nini kwenye nishati ya nuclear?
 
Hao ndo wanakuendeshea maisha mkuu,

Wamejaa mawizara yote, wamejaa mataasisi yote makubwa,

Kama haujui Hao ndo muhimili wa watanzania, sio wote ila like 20% wanafanya vzr na wanazibeba saana taasisi wanazozifanyia kazi
Watu concentration yao ipo kwa wakina chief godlove na show off zao mitandaoni. Kwaiyo wanafikiri wasomi wote ni useless
 
Hizo ni shule maalumu kwa waliopata alama za juu tu.
Nafikiri jina sahihi ni shule maalumu/special schools kama ulivyoandika na si vipaji maalumu.

Wazee wa mongwe wanywa nyuka na wenzao wa mkoani Arusha, Pwani, Dodoma na Tabora wanaelewa hivyo. Sema mtaani watu walikuza mambo na kutoa sifa ambazo hata wao hawakuzipenda wala kutaka waitwe vipaji maalum
 
Hakuna elimu ya maana zaidi ya kuzalisha majobless wenye matokeo makubwa kila mwaka na hizi ndio ndoto zao wanasiasa, yaani serikali haina maono yoyote wao furaha yao kuona kila mtoto anapata Masomo A zote, division 1, na GPA ya kutisha, masuala ya kazi na baada ya shule wao hayawahusu.

Upuuzi wa hali ya juu karne hii kukomalia katika matokeo ya ufaulu badala ya matokeo yanayohusu vitendo vya uzalishaji wa nguvu kazi ktk matumizi sahihi ya rasilimali, ubunifu na solution kwa changamoto za kiafya, kijamii, kiuchumi, yaani tupo tupo kupigana na walimu wafaulishe matokeo makubwa ambayo hayana impacts yoyote.

Elimu ya form5+6 ni takataka haina maana wala faida kwa sasa lakini bado tumekomalia huu upuuzi, baadhi ya masomo na topics hazina maana wala faida lakini bado tumekomalia kukalilisha watoto upuuzi usio na maana.
Matokeo ya kuongozwa na serikali isiyo na vision ndio haya bado tungali gizani.
 
Vipaji maalum weru ni div one

Which is a veeybwrong factor yw kuwa special student
 
Nikiwa m1 wa waliopita special schools, itoshe kusema kule ni kusoma sana, kukariri na kugombania u TO.

Ila kuna ka hype fulani kusoma special schools. Tchaos.

Sent from my Infinix X669 using JamiiForums mobile app
Utakubaliana na mimi hizi special schools wengi wanafaulu kwa uwezo wao maana hata walimu ni wa kawaida sana kuliko hata wanafunzi.

Ukitaka kuona uwezo wao peleka huduma zote zilipo Fedha schools halafu uone watakachofanya. Huko kuna vichwa kwelikweli sio mchezo. Kuyaelewa masimple pendulum inahitaji ubongo tulivu kwelikweli. Hata sasa matokeo ya shule hizi ni mazuri sana.
 
Kukariri kipaji pia usifanye mchezo kukariri,kwanini wao waweze kukariri halafu wengine washindwe?
Uko kukalili Kuna faida gani kwa mwanafunzi na taifa? Nyie ndio wale ambao bado mko gizani mnadhani elimu ni kupata marks za juu wakati huo mkishamaliza hiyo shule mnarudi mtaani hata kujiajiri hamuwezi wala kubadili hiyo elimu kutatua changamoto hamuwezi mnasubiri ajira za kugombania.

Mjifunze kwa hao waliowaandikia hiyo mifumo ya elimu, wao walishaachana na huo upuuzi wenu wa kugombania marks za kukalili ambazo hazina impacts
 
Pia mifumo mingi ya IT wako hao wanaopuuzwa, watendaji wakuu wa wizara na taasisi za umma wako hao special schools alumni. Sehemu pekee ambako wako wachache ni kwenye siasa ndio unawapata wachache.
 
Vipaji maalum weru ni div one

Which is a veeybwrong factor yw kuwa special student
Watu wanatafuta sana sababu za kuwashusha hadhi waliosoma kama vile wao hawakutaka au walikatazwa kufaulu vizuri. Mimi nilipomaliza shule ya msingi ni peke angu nilipiga flat A ikiwemo hesabu nilipiga 50/50 nikapangiwa kwenda kuendelea form azania sekondary.

Wanafunzi wengine sio kwamba hawakutaka au walikatazwa kufaulu kama mimi, isipokua uwezo wao ulikua mdogo. Hao sasa wakiyabahatisha maisha ndio hawa wakina dotto magari, kutwa kuwapopoa wasomi wakati ajui kwamba takwimu zinaonesha illiteracy people wenzake ndio population kubwa zaidi ya watu wanaoishi maisha ya dhiki
 
Zote ni njia za kutafuta hela sio u maalum wa pekee tu. Tunategemea mwanafunzi akishajifunza katika shule hizo anakuwa bora zaidi katika masomo ya amali na vilevile tunapata madaktari bingwa ambao ni wepesi kuelewa katika masomo yao.
 
Ni kweli matokeo yao yako poa. How about Innovations?
 
Swali lako ni sawa na mtu kuuliza faida ya misikiti na makanisa ni zipi ...jibu ni hakuna faida yoyote ya maana
 
Una point nzuri sana ila nafikiri kwa watu ule shule za msingi hazikuandaa kutambua vipaji vya watoto ili wanapokwenda sekondari waende kutokana na vipaji vyao. Angalau majeshi enzi za Nyerere na mwinyi watu waliingia kutokana na walichonacho. Kuna wazee waliingia jeshi kwa kusakata kabumbu, riaza, ufundi, kuimba na vipaji vingine.

Hizi shule zingine kigezo ilikuwa uwezo kuelewa. Sikubaliani na wazo la kukariri. Serikali ndio haikuweka mifumo mizuri ya kuhakikisha wanatumika kugundua vitu na hata wakigundua au wakibuni wanawekewa vikwazo. Na wengi wamechukuliwa na mataifa yaliyoendelea ili wakanufaishe nchi zao. Wachache serikali huamua kuwarudisha nchini ingawa mazingira huwa magumu kwao
 
Niliwahi kusikia waligundua Namba ya Panya kugundua Magonjwa ya TB kwenye Sample za Makohozi. Hadi leo sijajua imefikia wapi ile project
Na pia kutegua mabomu kule Afghanistan na kwingineko kwenye vita, panya mtaalamu alikufa,baadae tukasikia alipata warithi wake,sijui hadi sasa waliishia wapi!!?
 
Ni kweli matokeo yao yako poa. How about Innovations?
 
Well
Zote ni njia za kutafuta hela sio u maalum wa pekee tu. Tunategemea mwanafunzi akishajifunza katika shule hizo anakuwa bora zaidi katika masomo ya amali na vilevile tunapata madaktari bingwa ambao ni wepesi kuelewa katika masomo yao.
 
Umeeleza vizuri boss. Hawa vipaji maalumu wapo na wanatumika kwenye mataifa yaliyoendelea. Sera za nchi haziwapi nafasi ya kutumia uwezo walio nao. Wakigundulika na mataifa mengine wanabebwa nankupotelea huko. Nawafahamu wengi hawapo nchini wako ughaibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…