Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Sekondari za Vipaji maalum takribani miaka 40 tangu kuanzishwa kwake umaalum wake uko kwenye nini? Hatuoni ubunifu wowote

Watu wanataka UMAALUMU WAO kama walivyopewa status"SPECIAL". Kama ni utendaji tu wa kawaida hata wasioenda special school wanafanya.
China mwanafunzi akipewa hio status tegemea innovation za ajabu.
Kiujumla wanafanya vitu ambavyo haviwatofaitishi sana na wengine.
Sababu sio kwamba hawawezi kufanya vitu special ila wameathiriwa na mfumo.
Imagine Elon Musk angeamua kubaki SA je angeweza kufanya anayofanya ? Big no, Africa haisapoti ubunifu.
Well
 
Kwa mifano yako uliyoitoa hapo mwishoni bila shaka hujaelewa lengo la uzi.
Lecturer wa sayansi anafundisha chuo ujerumani-ana utofauti gani na lecturer wa UDSM?
Mwingine daktari anaishi New castle-ana utofauti gani na daktari wa Muhimbili?
Hapa lengo la uzi ni kujua wamefanya uvumbuzi gani wenye kuletq impact kwa jamii,hatuongelei kupata kazi ya kulipwa mshahara mkubwa au kukimbilia ulaya
Kufundisha ujerumani na kuwa dokta uingereza kuna tofauti kubwa sana na kuyafanyia hayo hapa bongo ambapo unaweza kupenya kwa connection na ujanja janja tu, mpaka wazungu wakuchukue lazima uwe finnest kwenye field yako. Wazungu hawatoi scholarship kwa vilaza.

Suala la uvumbuzi mtu anaweza kuvumbua mambo hapo hapo kwenye field yake, mfano dokta anaweza kuja na njia ya kurahisisha ufanyaji wa oparesheni, huo tayari ni ubunifu.
 
K

Kiukweli hata mimi sikupenda jamaa kuwatolea mfano wakina Mwijaku sijui Mobeto hao ni wakaa uchi mitandaoni hawapaswi kutolewa mfano kwenye mada yoyote inayohusu mambo ya msingi.
Sasa tukiendelea mbele na mada yetu katika mifano yako uliyoitoa bado hatujaona ugunduzi hapo kuendesha AI means AI tayari ilishagunduliwa na watu wengine wa nchi za mbali yeye anaitumia tu au sivyo hivyo?
Hata internet iligunduliwa na wengine kabla wakina mark zuckerberg hawajaja na facebook. Gunduzi za fizikia nyingi zilishawekwa na Isack Newton, wakina Albert Eistein wakaja kuziendeleza tu. As long as mtu kaonyesha utofauti apewe maua yake.
 
Kila mtu akijiweka bize kwenye kukariri anaweza.
Kinachotofautiana ni mazingatio na kipaumbele katika muda huo husika.
Mwanafunzi mwingine utakuta kipaumbele chake ni michezo,mwingine kipaumbele chake ni kuangalia movies na mwingine kipaumbele chake ni kukesha na notsi kila siku hana muda na mambo mengine na hana muda na stori au kuongea na watu ndio hao mnawaita kipaji maalum.
Suala sio kukariri tu ambapo nyie mmepakazania. Viwango vya uelewa pia vinatofautiana. Kuna watoto wa kaka zangu na dada zangu huwa nawasaidia masomo yao ya shuleni. Ninapowafundisha naona tofauti zao za uelewa, kuna wanaoelewa haraka na wanaoelewa taratibu. Katika mfumo wa elimu ambao mwanafunzi ana-qualify kwa kupimwa na mtihani suala la kukariri ni lazima ili uwe na kumbukumbu kuweza kujibu maswali. Lakini sio kwamba hawa vipanga wanakalili halafu wakiingia kwenye mtihani wanashuka tu wakiwa hawajui wanachokiandika. Wanaelewa kwanza concept ya mada ndio linafuata suala la kukariri kwa ajiri ya kujibu mtihani. Infact hata vilaza nao wanakariri lakini bado wanafeli au wanafaulu kwa viwango vya kawaida sana
 
Well noted.
Hapo kwenye mitaala nakubaliana na wewe.
So ilitakiwa viongozi washtuke waibomoe hiyo mitaala na kutengenezwa upya hii ndio solution.
Hapo sasa ndipo umegusa kwenye msingi wa tatizo. Sera zetu za elimu pamoja na uwwkezaji kwenye tafiti na ubunifu ni duni sana. Hawa vipanga sio rahisi ku-utilize akili zao katika mazingira kama hayo. Bahati mbaya sana tumetembea na biti za wakina mwijaku na musukuma halafu hatuangalii mfumo mzima unaopika hao wasomi
 
German Engineers wao wanaanza kusomea Engineering kuanzia primary school hadi akifika level ya Diploma huyo mtu ni noma sana hashikiki na ndio maana unaona products zao kwenye ubora hawashikiki wakati huku kwetu unakuta mtu ana Phd ya Mechanical Engineering na hajui hata kutengeneza toroli au mtu ana Phd ya Electrical Engineering na hajui hata kutengeneza bulb kwa vitendo.
 
Suala sio kukariri tu ambapo nyie mmepakazania. Viwango vya uelewa pia vinatofautiana. Kuna watoto wa kaka zangu na dada zangu huwa nawasaidia masomo yao ya shuleni. Ninapowafundisha naona tofauti zao za uelewa, kuna wanaoelewa haraka na wanaoelewa taratibu. Katika mfumo wa elimu ambao mwanafunzi ana-qualify kwa kupimwa na mtihani suala la kukariri ni lazima ili uwe na kumbukumbu kuweza kujibu maswali. Lakini sio kwamba hawa vipanga wanakalili halafu wakiingia kwenye mtihani wanashuka tu wakiwa hawajui wanachokiandika. Wanaelewa kwanza concept ya mada ndio linafuata suala la kukariri kwa ajiri ya kujibu mtihani. Infact hata vilaza nao wanakariri lakini bado wanafeli au wanafaulu kwa viwango vya kawaida sana
Ngoja nikuulize swali fulani hivi ili tuondoe contradiction.
Kuna jamaa mmoja hivi tulisomaga naye sekondari yule jamaa yeye udhaifu wake alikuwa hajui kabisa somo la kiingereza yaani kwa kifupi yeye sentensi yoyote iliyoandikwa kwa kiingereza yeye alikuwa hajui kabisa inaongelea nini na likija somo lile la kiingereza alikuwa anaambulia D akipata C ni kwa kubahatisha.
Lakini yule jamaa yeye ujanja wake ilikuwa ni kukesha usiku na mchana kukariri notsi na mitihani ikija alikuwa anapata A nyingi tu za masomo ya Sayansi na kwenye Darasa lake alikuwa anaingia 3 bora kwa watu wanaofaulu sana.
Je huyu jamaa naye ni kipanga au sio kipanga kwa uwelewa wako?
 
Mfano wako ni kama hauna uhalisia, kwamba hajui chohote kabisa kuhusu english sasa hayo masomo ya physics alikua anakalili vipi? ni sawa na mimi sijui neno wala herufi hata moja ya kichina halafu nikariri notes za kichina, it makes no sense. Labda tuseme basic english alikua anaijua lakini advanced english ndio inampiga chenga.

Suala la kuwa mzuri kwenye somo fulani na kuwa mbovu kwenye somo jingine iyo ipo ndio maana kadiri unavyopanda ngazi kielimu unapunguziwa masomo kulingana na mchepuko unaoutaka, mfano mimi wakati nasoma shule ya msingi somo la kiswahili lilikua linanipiga chenga kidogo ingawa nilikua nafaulu kwa maksi za wastani lakini masomo ya hisabati, sayansi, maarifa ya jamii na english hayo hata uniletee mtihani nikiwa mgonjwa mahututi kitandani lazima nipige A. Udhaifu wa somo la koswahili pekee haukunizuia kupata daraja la juu na kupangiwa kuendelea sekomdari katika moja ya izo shule maalumu
 
Mkuu nimekuuliza kitu kingine wewe umenijibu kitu kingine tofauti au ni kama umelikwepa swali.
Hilo jambo la kuwa mtabe kwenye masomo fulani na kuwa mdhaifu kwenye masomo mengine hilo linafahamika hata mimi pia kuna baadhi ya masomo nilikuwa vizuri na mengine nilikuwa dhaifu kidogo hilo lipo.
Swali nililokuuliza ni kuhusu yule classmate wangu na namjua nje ndani ndio maana nikamtolea mfano yeye na si wengine.
Ishu ni kwamba yule jamaa yeye hajui kutafsiri sentensi yoyote iliyoandikwa kwa kiingereza lakini alikuwa anakesha kukariri na anafaulu mitihani je huyu naye ni kipanga?
Na ukiongelea habari za advanced English sidhani kama Olevel kuna Advanced English hiyo ni Form 5 na 6 kwa watu waliospecialize kwenye Comb. za HGL/HKL.

Hakuna umaalumu wowote wengi tumesoma shule hizo hata ufundishaji wao ni wa kupiga msuli binafsi(kujisomea) vinginevyo utafeli
Special School in Tanzania, is just a congregation of elites simply for the GoT to sort out Special Characters later on! So the huge advantage of being a Student at that School is the probability of being under Surveillance!
 
Mkuu nimekuuliza kitu kingine wewe umenijibu kitu kingine tofauti au ni kama umelikwepa swali.
Hilo jambo la kuwa mtabe kwenye masomo fulani na kuwa mdhaifu kwenye masomo mengine hilo linafahamika hata mimi pia kuna baadhi ya masomo nilikuwa vizuri na mengine nilikuwa dhaifu kidogo hilo lipo.
Swali nililokuuliza ni kuhusu yule classmate wangu na namjua nje ndani ndio maana nikamtolea mfano yeye na si wengine.
Ishu ni kwamba yule jamaa yeye hajui kutafsiri sentensi yoyote iliyoandikwa kwa kiingereza lakini alikuwa anakesha kukariri na anafaulu mitihani je huyu naye ni kipanga?
Na ukiongelea habari za advanced English sidhani kama Olevel kuna Advanced English hiyo ni Form 5 na 6 kwa watu waliospecialize kwenye Comb. za HGL/HKL.
Mfano wako haujakamilika mkuu, yaani mtu akiulizwa what is physics? hajua kaulizwa nini halafu aweze kukariri achmedes principles.! haiingii akilini. Labda kama unamaanisha english alikua anaijua juu juu lakini sio kwa undani, lakini kusema hajui chojote kabisa yaani kama mimi nikisoma kihindi au kikorea hii ni ngumu kumeza mkuu
 
Usitolee mfano wa kihindi au kichina hawa wana muundo wao tofauti wa Alphabet.
Lakini Alphabet za kiingereza na zetu za kiswahili ni sawa so alikuwa ana idea ya kujua kuyasoma matamshi ya kiingereza lakini hajui kutafsiri hope umenielewa?
 
Tumejionea wenyewe kule chini na mahala pengine kama ulaya Watoto wadogo wanaandaliwa kiwa Wanasayansi na mainjinia wabobezi. Watoto hao wanasukwa na kufinyangwa kiasi kwamba wanaanza kubuni na kuvumbua Mitambo na teknolojia za kipekee zenye mchango mkubwa ktk maendeleo ya kiuchumi kwenye nchi zao.

Hapa Tanzania mfumo wa Shule za Vipaji maalum umekuwepo kwa miaka mingi sasa.

Binafsi sikuwa na bahati ya Kujiunga na shule hizo hivyo nilitarajia pia kunufaika na Ubunifu/ innovations kutokana na kundi hili kubwa wenye vipaji Maalum/ special inteligence.

Tuna sekondari nyingi kama
1. Ilboru Arusha
2. Msalato Girls Morogoro
3.Mzumbe Boys Morogoro
4.Kibaha Boys Pwani
5. Tabora girls na Tabora Boys.

Ndio kusema Maelfu kwa Maelfu ya Wanafunzi waliopita humo hakuna hata wawili watatu walioonesha Ukipaji wao?

Tuseme basi Mtaji ni Mkubwa ku invest, hata Basi Kuwa Social influencer/ matumizi ya tech zilizopo je?

Tunaona Watu wenye elimu kiasi tu ndio wanaofaidi matumizi ya Technolojia na kunufaika na kuitangaza Tanzania.
Watu kama akina Maulid Kitenge, Kipanya, Zembwela, Diamond, Millard Ayo, Mwijaku, Baba Levo, Mobeto.

Angalau hawa hawakugundua chochote kama walivyo wale wa vipaji maalum ispokuwa wameweza kugundua matumizi sahihi ya teknolojia iliyopo.

Vipaji maalumu katika sekondari hizo ni vya mchongo au tunakwama Wapi?

Bonjour, Je M'apelle Bush Dokta habité à Makerere universite.

Bonvenué de discusio reun̈ion
Umaalum unaishia form six.
Wakifika UDSM wanawekwa digrii moja na waliotoka Nkung'ungu sekondari, na wanafundishwa na profesa mmoja kwa kufuata mtaala wa hiyo digrii. Baadaye wote wanashauriwa kwenda kusoma VETA.
 
Mada nzuri.
Kwa kuwa ume declear kuwa hukubahatika kuchaguliwa shule hizo basi moja kwa moja umekiri wengi huwajui na hujawahi wafuatilia.

BInafsi nawatambua vijana kadhaa waliopita shule hizo na wana mchango mkubwa kwa taifa katika nyanja mbalimbali.

Mfumo wa elimu zetu hazikutuwezesha kufanya gunduzi mbalimbali kwa sababu ya mazingira na vifaa. Lakini pia ugunduzi si mpaka urushe ndege. Matumizi sahii ya akili yako yanaweza kuleta matokeo chanya katika jamii.

Mfano juzi tumeona wanafunzi wa kibaha wakiwekeza mfumo wao wa kupiga kura kidigitali na kufanya uchaguzi.

Vipaji maalumu wengi walivyofika chuo wameendelea katika taaluma mbali mbali na pia wengi wapo na kampuni kadhaa....

Naweza kukutajia mbili tu. Anayeendesha AI ya kiswahili ni kipaji maalumu. Aliyeandika code za kampuni moja ya mawasiliano ni kipaji maalumu.

Nyerere ni kipaji maalumu n.k

Kwa namna ulivyotaja hao influencer wako ni dhahiri wewe ni mtu wa social media unayedanganywa na mafanikio ya picha.
Tatzo la watanzania wengi hudhania mafanikio ni hela nyingi au umaarufu.

Mimi nikuhakikishie tu. Kusanyiko la vilaza sio sawasawa na kusanyiko la vipaji maalumu. Kuna tofauti tu mtaonyesha kwenye kufikiri na kwenye kuamua.

Leo form 1 failure anaweza kutamba kuwa ana hela kuliko aliyesoma chuo. Lakini anasahau kuna watu behind walioweka mifumo imara inayofanya yeye apate hela.

Uvivu wa kufikiri unafanya tunakuwa na jamii isiyo na misingi imara na iliyokosa fikra timamu. Leo mtu mzima ana praise wauza uchi na machawa kuwa ndio wenye mafanikio. Huu ni ugonjwa wa akili.
Umeambiwa utaje innovation yoyote ya maana iliyoleta significant impact kwenye jamii iliyofanywaa na hao wahitimu wa shule zinazoitwa za "vipaji maalumu" kwa muda wa miaka 40 iliyopita, halafu wewe unaleta maelezo meeeengi ambayo hayana kichwa wala miguu.

Tunataka significant impact zilizofanywa na nyie mliosoma shule maalumu, na sio kututajia mifano sijui anayeendesha AI ya kiswahili sasa huyo nae kafanya gunduzi gani? Kubadilisha lugha au??? Mara sijui wanafanya kazi kwenye makampuni sasa ya nini yote hayo?

Binafsi mimi namuheshimu ntu aliyesoma Technical school kama Musoma tech, Moshi Tech.. n.k huko ndio angalau huwa tunawapata hawa akina mello

Ila nyie mliosoma sijui kibaha,mzumbe, ilboru hamna innovative skills zozote mnachojua nyie ni kushindana kupata division one ya point 3 tu baasi kisha baada ya hapo muende Udsm mwisho wa siku mnaishia kugaombania kazi za TRA au TANROAD
 
Umaalum unaishia form six.
Wakifika UDSM wanawekwa digrii moja na waliotoka Nkung'ungu sekondari, na wanafundishwa na profesa mmoja kwa kufuata mtaala wa hiyo digrii. Baadaye wote wanashauriwa kwenda kusoma VETA.
😅😅😅
 
Umeambiwa utaje innovation yoyote ya maana iliyoleta significant impact kwenye jamii iliyofanywaa na hao wahitimu wa shule zinazoitwa za "vipaji maalumu" kwa muda wa miaka 40 iliyopita, halafu wewe unaleta maelezo meeeengi ambayo hayana kichwa wala miguu.
Yaani....sijui kwanini Watz wana maneno mengi. Hoja ikp wazi lkoni watu wanazunguka mno.

Asante
 
Ila nyie mliosoma sijui kibaha,mzumbe, ilboru hamna innovative skills zozote mnachojua nyie ni kushindana kupata division one ya point 3 tu baasi kisha baada ya hapo muende Udsm mwisho wa siku mnaishia kugaombania kazi za TRA au TANROAD
Ofcourse wote hawawezi kuwa wagunduzi. Lakini mpaka uzi umefik hapa hakuna hata mfanno mmoja uliotolewa.
 
Mfano wako haujakamilika mkuu, yaani mtu akiulizwa what is physics? hajua kaulizwa nini halafu aweze kukariri achmedes principles.! haiingii akilini. Labda kama unamaanisha english alikua anaijua juu juu lakini sio kwa undani, lakini kusema hajui chojote kabisa yaani kama mimi nikisoma kihindi au kikorea hii ni ngumu kumeza mkuu
Heehehe. Archimedes principle and law of Floatation.
 
Tusitake kujipa moyo kuwa waliosomea shule za vipaji hakuna kitu. Wengi wao walifika chuo kikuu na kuja kupata ajira au kujiajiri kisha kubadili maisha yao na familia zao. O - level nilisoma shule mojawapo na darasa lilikuwa vipanga tupu. Nakumbuka nilikuwa na average ya 71% nikashika namba 15 kati ya watu 30. Ilikuwa hatari. Katika niliosoma nao ni wachache ambao hawako kwenye green pastures. Kuhusu ubunifu au kugundua kitu ni jambo kubwa lenye mambo mengi. Hata ambaye kaishia darasa la pili anaweza kuibuka na ugunduzi wake na akasaidia jamii. Tusiwatwishe waliopita special schools mizigo isiyokuwa na ulazima.
 
Back
Top Bottom