mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Huku ni KUPITILIZA na tunasema HAIKUBALIKI KABISA. Haiingii akilini watu na akili zao kuamua kutokuheshimu kwa makusudi imani ya watu ambao wanapaswa kuwa kwenye ibada KANISANI na kuipanga siku hiyo kuwa ni siku ya kuwasaili waombaji wa ajira.
Ina maana wanaoendesha usaili huu kama ni wakristo watakuwa wamedhulumiwa haki na uhuru wao wa kuabudu. Ina maana pia waombaji wa ajira walio wakristo watakuwa wamedhulumiwa haki na uhuru wao wa kuabudu. Hili tunalikataa kwa nguvu zetu zote!!
Tarehe 18/06/2022 siku ya JUMAMOSI (SIKU YA IBADA KWA WASABATO), na tarehe 19/06/2022 siku ya JUMAPILI (SIKU YA IBADA KWA WAKRISTO) zimetangazwa kuwa ni moja ya siku ambazo usaili wa waombaji wa ajira utafanyika. Kwanza jumamosi na jumapili siyo siku za kazi, kwa nini hawa sekretarieti ya ajira wameamua kuzifanya kuwa siku za kazi? Hii JEURI WANAIPATA WAPI? Ushahidi upo kwenye tovuti yao- www.ajira.go.tz na ninatupia kipande hapa:
KADA: ASSISTANT VOCATIONAL TEACHER – ELECTRICAL INSTALLATION MWAJIRI: MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) TAREHE YA USAILI WA VITENDO: (1-37) 18 JUNI, 2022 (38-74) 19 JUNI, 2022 MAHALI: VETA DODOMA TAREHE YA USAILI WA MAHOJIANO: 22 JUNI, 2022 MUDA: SAA 1:00 KAMILI ASUBUHI. MAHALI: OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZILIZOPO MAJENGO YA DKT. ASHA ROSE MIGIRO, UDOM - DODOMA.
Ninamwomba waziri mwenye dhamana na sekretarieti hii kufanya mambo yafuatayo kwa dharula:
1. Kubatilisha hizo tarehe haraka na kagiza zipangwe tarehe zingine.
2. Kuwawajibisha wote waliofanya ujeuri huu wa kuleta utaratibu unaoashiria UDINI kwenye nchi yetu.