Sekretariet ya ajira katika utumishi wa umma kuendesha usaili siku ya ibada Jumapili

Sekretariet ya ajira katika utumishi wa umma kuendesha usaili siku ya ibada Jumapili

Darula huwa haipangwi!! Siku ya usaili siyo dharula na ina nafasi ya kupangiwa tarehe!! Dharula ni kama ajali, au ugonjwa ambao haujui utatokea lini kwa hiyo huwezi kupanga tarehe ya kwenda hospitali kwa ugonjwa unaoweza kukupata ghafla. Hapa hakuna dharula yoyote iliyosababisha usaili upangwe jumamosi na jumapili.
we umeendekeza udini mbele sana sasa usiende kwnye usaili tuone nani atafaidika na atakaepta hasara
 
Huku ni KUPITILIZA na tunasema HAIKUBALIKI KABISA. Haiingii akilini watu na akili zao kuamua kutokuheshimu kwa makusudi imani ya watu ambao wanapaswa kuwa kwenye ibada KANISANI na kuipanga siku hiyo kuwa ni siku ya kuwasaili waombaji wa ajira.

Ina maana wanaoendesha usaili huu kama ni wakristo watakuwa wamedhulumiwa haki na uhuru wao wa kuabudu. Ina maana pia waombaji wa ajira walio wakristo watakuwa wamedhulumiwa haki na uhuru wao wa kuabudu. Hili tunalikataa kwa nguvu zetu zote!!

Tarehe 18/06/2022 siku ya JUMAMOSI (SIKU YA IBADA KWA WASABATO), na tarehe 19/06/2022 siku ya JUMAPILI (SIKU YA IBADA KWA WAKRISTO) zimetangazwa kuwa ni moja ya siku ambazo usaili wa waombaji wa ajira utafanyika. Kwanza jumamosi na jumapili siyo siku za kazi, kwa nini hawa sekretarieti ya ajira wameamua kuzifanya kuwa siku za kazi? Hii JEURI WANAIPATA WAPI? Ushahidi upo kwenye tovuti yao- www.ajira.go.tz na ninatupia kipande hapa:

KADA: ASSISTANT VOCATIONAL TEACHER – ELECTRICAL INSTALLATION MWAJIRI: MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) TAREHE YA USAILI WA VITENDO: (1-37) 18 JUNI, 2022 (38-74) 19 JUNI, 2022 MAHALI: VETA DODOMA TAREHE YA USAILI WA MAHOJIANO: 22 JUNI, 2022 MUDA: SAA 1:00 KAMILI ASUBUHI. MAHALI: OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZILIZOPO MAJENGO YA DKT. ASHA ROSE MIGIRO, UDOM - DODOMA.

Ninamwomba waziri mwenye dhamana na sekretarieti hii kufanya mambo yafuatayo kwa dharula:
1. Kubatilisha hizo tarehe haraka na kagiza zipangwe tarehe zingine.
2. Kuwawajibisha wote waliofanya ujeuri huu wa kuleta utaratibu unaoashiria UDINI kwenye nchi yetu.
Wewe chukulia tu kuwa kazi ni ibada, na usaili wa kupata kazi ndio mlango wa kuingilia nyumba ya ibada. Wacha usaili ufanyike siku yoyote au muda wowote, wewe nenda tu. Kama huna amani na huo usaili basi achana nao nenda zako kaabudu, sio lazima uajiliwe na wabagani.
 
Hili jambo limepangwa hivyo kimkakati ili kubagua baadhi ya watanzania. Kama unafikiri kuwa jambo hili ni dogo subiri na ulifuatilie jinsi litakavyoishia jambo hili!! Suala hili litaenda hadi mahakama ya juu kabisa kama akithubutu mtu kulishughulikia kivyepesi vyepesi!!
Hahahaha acha vitisho ndugu yangu piga msuli paper za utumishi sio za mchezo,,

Kama kweli unataka utoboe kaza kabisa haya mengine achana nayo!!

Mi sioni cha ajabu hapo coz mungu yupo siku zote hizi siku maalum zimewekwa tu ili mwenye wasaa apate kujumuika kwa pamoja na kufanyika maombi yapamoja na mafundisho kidog kama yatakuwepo ila vinginevyo nikuomba tu mwenyewe kwenye mda ambao unaohisi unahitaji zaidi msaada wa mungu..
 
Vyote ni muhimu na vyote vina haki ya kufanyika! Lazima mamlaka zinazohusika zipange kwa namna ambavyo raia wake watalindiwa haki zao zote. Tunadai uwajibikaji kwa mtumishi yeyote aliyepanga katika namna ambayo watanzania wengine watakosa haki zao za msingi.
Ukute siku yenyewe ameikumbuka baada ya kuambiwa usaili ni jumapili na jumamosi
 
Huku ni KUPITILIZA na tunasema HAIKUBALIKI KABISA. Haiingii akilini watu na akili zao kuamua kutokuheshimu kwa makusudi imani ya watu ambao wanapaswa kuwa kwenye ibada KANISANI na kuipanga siku hiyo kuwa ni siku ya kuwasaili waombaji wa ajira.

Ina maana wanaoendesha usaili huu kama ni wakristo watakuwa wamedhulumiwa haki na uhuru wao wa kuabudu. Ina maana pia waombaji wa ajira walio wakristo watakuwa wamedhulumiwa haki na uhuru wao wa kuabudu. Hili tunalikataa kwa nguvu zetu zote!!

Tarehe 18/06/2022 siku ya JUMAMOSI (SIKU YA IBADA KWA WASABATO), na tarehe 19/06/2022 siku ya JUMAPILI (SIKU YA IBADA KWA WAKRISTO) zimetangazwa kuwa ni moja ya siku ambazo usaili wa waombaji wa ajira utafanyika. Kwanza jumamosi na jumapili siyo siku za kazi, kwa nini hawa sekretarieti ya ajira wameamua kuzifanya kuwa siku za kazi? Hii JEURI WANAIPATA WAPI? Ushahidi upo kwenye tovuti yao- www.ajira.go.tz na ninatupia kipande hapa:

KADA: ASSISTANT VOCATIONAL TEACHER – ELECTRICAL INSTALLATION MWAJIRI: MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) TAREHE YA USAILI WA VITENDO: (1-37) 18 JUNI, 2022 (38-74) 19 JUNI, 2022 MAHALI: VETA DODOMA TAREHE YA USAILI WA MAHOJIANO: 22 JUNI, 2022 MUDA: SAA 1:00 KAMILI ASUBUHI. MAHALI: OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZILIZOPO MAJENGO YA DKT. ASHA ROSE MIGIRO, UDOM - DODOMA.

Ninamwomba waziri mwenye dhamana na sekretarieti hii kufanya mambo yafuatayo kwa dharula:
1. Kubatilisha hizo tarehe haraka na kagiza zipangwe tarehe zingine.
2. Kuwawajibisha wote waliofanya ujeuri huu wa kuleta utaratibu unaoashiria UDINI kwenye nchi yetu.
Wakipanga kuanzia jumatatu utawajibika kusafiri jumamosi au jumapili, napo utaacha ibada. Hurazimishwi kwenda, una jumapili 52 za kwenda kanisani, kupanga ni kuchagua.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Siyo suala la kuwa mfia dini, bali ni suala la watu kuheshimu ibada ya watu wengine> Hivi haujaona hata hotuba za kitaifa kusitishwa kwa muda kupisha muda wa ADHANA? Wakristo na Wasabato wanaheshimu siku yao ya ibada na serikali ITAMBUE HIVYO na hapo HAKUNA MJADALA.
Kondoo wako akitumbukia kisimani siku ya ibada hutamtoa?

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mwanzo 2:3, kutoka 16:29-30, kutoka 20:8-11. "Ikumbuke siku ya saba uitakase, siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo USIFANYE KAZI NYOYOTE, wewe wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa".
Kama lengo lako ni kutaka kuelewa bila shaka umeelewa.
Mungu alistarehe, wewe una muda wa kustarehe? Wa zamani waliishi muda mrefu, hata wakipumzika wangeweza pata muda wa kutimiza majukumu yao, wewe leo muda huo unao?

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Tuna uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa sheria na si kinyume na sheria. Kwanza dini yako ni lazima isajiliwe serikalini. Na ili usajiliwe ni lazima katiba ya dini yako ikubalike. Kwenye katiba ni lazima uainishe hicho unachoamini na misingi ya dini yako. Kama wewe unakula nyama za watu ni kwamba serikali haitakubali kuisajili dini yako na hautaruhusiwa kuabudu.
Ibada na haqi ya ibada nini kinatangulia??
 
Watu mnaongea kishabiki bila kuangalia matakwa ya kisheria na haki ya kikatiba ya mtanzania. Waajiri wenye jeuri wamekuwa wakilipa mamilioni ya sjilingi kama fidia kwa ajili ya kuwanyima watu haki ya kuabudu kwa kuwapangia majukumu kwenye siku zao za ibada. Hapa nawawekea mfano mmoja tu kati ya mingi.

NATIONAL MICROFINANCE BANK LTD (NMB) VERSUS NEEMA AKEYO, CIVIL APPEAL NO. 511 OF 2020, CAT.

Mwandishi: Zakaria.
Taaluma: Mwanasheria.

Hii kesi inahusu mfanyakazi (Neema Akeyo) ambaye alifutwa kazi isivyo halali kwa sababu za ubaguzi wa kidini ambapo alikuwa anaenda kufanya ibada siku za jumamosi kama haki yake Kikatiba ya uhuru wa kuabudu.

Lakini pia, sheria haikufatwa ipasavyo wakati wa kumfuta kazi Neema Akeyo, mfano hakupewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuamua kumuachisha kazi.

Watu wengi wameshaiongelea sana. Lakini kutokana na umuhimu wake nimeamua kuitafsiri tena na kuipost ili iwafikie watu wengi hasa waajiri. Kumekuwa na hulka ya kuwanyima wafanyakazi uhuru wa kuabudu, kwa kuwapangia kazi siku za Ibada.

Wahanga wakubwa ni Waadventista Wasabato wanaosali Jumamosi. Kidogo kidogo, Jumamosi imeanza kuzoeleka kama siku ya kazi. Hata interviews nyingi za kazi sasa zinapangwa Jumamosi. Ina maana wasabato wengi watakosa kazi.

Dini zote ni sawa, na bahati nzuri nchi hii haina dini (ni secular State), hivyo isionekane dini au dhehebu moja linapendelewa sana au kuonewa. Naamini wahusika mtalishughulikia.

Turudi kwenye kesi yetu.

Tuanze na FACTS (STORI YA KESI):

-Neema Akeyo aliajiriwa na Bank ya NMB kama Bank teller, Wilaya ya Karatu.

-Ajira hiyo ilianza tarehe 27/10/2010 mpaka tarehe 5/6/2015 alipofutwa kazi na NMB kwa sababu ya kutoenda kazini (utoro) siku za jumamosi na kutotii mwajiri.

-Neema akaenda kushtaki au kulalamika kwenye Commission for Mediation and Arbitration (CMA) yaani Tume ya Usuluhishi na Uamuzi/Upatanishi, akidai kwamba alifutwa kazi kimakosa na kwamba alipwe fidia kwa kitendo hicho cha NMB kuvunja mkataba wa ajira.

MBELE YA TUME:

-NMB ikakana kuvunja mkataba, ikasema mlalamikaji (Neema) alifutwa kazi kwa sababu halali na kwamba taratibu zote zilifuatwa.

-NMB ikasema kwamba, mlalamikaji alifutwa kazi KWA SABABU YA KUSHINDWA KWENDA KAZINI SIKU ZA JUMAMOSI (UTORO) ambapo ilikuwa ni kinyume na makubaliano ya kazi na kinyume cha sera na kanuni za NMB.

-Baada ya kusikiliza kesi mpaka mwisho, mwamuzi wa Tume aliridhika kwamba, mlalamikaji (Neema) hakufutwa kazi kihalali (was unfairly terminated), na kwamba utaratibu haukufatwa.

-Tume ikasema kwamba, hakuna ushahidi kutoka NMB unaothibitisha kwamba Neema hakuwa anaenda kazini siku za Jumamosi.

-Pia, hata baada ya mlalamikaji kukutwa na makosa, hakupewa nafasi ya kujitetea.

-Hivyo Tume ikasema Neema hakufutwa kazi kihalali.

-Tume ikaamuru, Neema alipwe mshahara wa miezi 36 kama fidia.

NB: (Usiporidhika na maamuzi ya Tume (CMA) unaomba revision (mapitio) kwenye Mahakama ya kazi (Labour Court) - ambayo ni Mahakama Kuu divisheni au kitengo cha Kazi. Zingatia sijasema unakata rufaa (appeal), kuna tofauti kati ya Appeal na Revision.)

-NMB hawakuridhika na maamuzi ya Tume, wakafungua maombi Mahakama kuu, wakiomba maamuzi ya Tume yapitiwe upya.

MAHAKAMA KUU:

-Neema akashinda kesi tena dhidi ya NMB.

- Mahakama Kuu ikatupilia mbali maombi ya NMB, na kupigilia msumari maamuzi ya Tume yaliyompa Neema tuzo ya kulipwa mshahara wa miezi 36.

-Mahakama Kuu nayo ikasema Neema hakufutwa kazi kihalali, na kwamba utaratibu haukufatwa.

-Mahakama Kuu pia ikasema, NMB wameshindwa kuthibitisha kwamba mlalamikaji alikuwa haendi kazini siku za jumamosi.

-Zaidi sana, Mahakama Kuu ikaongezea kwamba, kwanza KITENDO CHA NMB KUTAKA MFANYAKAZI WAO AENDE KAZINI SIKU ZA JUMAMOSI (wakati yeye jumamosi ni siku yake ya Ibada) ILIKUWA NI UBAGUZI AU UNYANYASAJI WA KIDINI (DISCRIMINATION) ambapo ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, na sheria za kazi. (Emphasis added).

-Nanukuu kwa kiingereza, “High Court found the appellant's (NMB) conduct to have amounted to discrimination against the respondent on religious basis which was contrary to the Constitution of the United Republic of Tanzania, 1977 and the Labour Laws.”

-Mahakama ikasema kila mtu ana haki ya uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 19, ibara ndogo ya kwanza na kifungu cha 7(a) cha sheria ya Ajira na Mahusiano kazini. [Article 19(1) of the Constitution and section 7(4) (a) of ERLA].

-Hivyo basi, Mahakama ikasema kwamba sera na Kanuni za kazi za NMB zinakiuka Katiba pamoja na Sheria ya Ajira, kifungu cha 7(4).

-NMB haikuridhika na maamuzi ya Mahakama Kuu.

NB: (Usiporidhika na maamuzi ya Mahakama Kuu, unakata rufaa kwenda Mahakama ya Rufaa ambayo ni Mahakama ya juu na yenye Mamlaka ya mwisho nchini Tanzania.)

-NMB ikakata rufaa Mahakama ya Rufaa.

MAHAKAMA YA RUFAA

-Kesi ilisikilizwa na Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa.

-Mawakili wa pande zote mbili wakawasilisha hoja zao (ambazo sitaziandika hapa ili hii makala isiwe ndefu sana ikakushinda kusoma).

-Baada ya kuwasikiliza Mawakili wa pande zote, Mahakama ya Rufaa ikakaa sasa kuamua, ‘Je, Mlalamikaji alifutwa kazi kihalali na kwamba sheria ilifatwa au la!’

-Mahakama ikakuta Neema, akiwa katika eneo la kazi, alikuwa anatendewa tofauti na wafanyakazi wengine kuhusu haki ya Ibada.

-NMB waliruhusu baadhi ya wafanyakazi akiwemo Branch Manager kwenda kusali wanavyotaka lakini wakati huo huo wakamzuia Neema asiende kusali.

-Mfano Waislam waliruhusiwa kwenda kusali Ijumaa, lakini Neema alikataliwa siku ya Jumamosi.

-Mahakama ya Rufaa ikakubaliana na Mahakama Kuu na kusema kwamba, hicho kitendo cha mwajiri (kumzuia mfanyakazi kusali siku ya Jumamosi), ni kinyume na ni ukiukwaji wa sheria ya kazi kifungu cha 7(4)(g).

-Hicho kifungu kinakataza ubaguzi dhidi ya mfanyakazi kwa sababu mbali mbali ikiwemo dini au Imani.

-Nanukuu kwa kiingereza “as correctly found by the learned Judge of the High Court, the act of the appellant (NMB) as an employer contravened the provisions of section 7(4) of the ELRA which abhors discrimination at place of work”

-Mwisho Neema Akeyo akashinda kesi tena.

-Mahakama ya Rufaa ikasema imejiridhisha kwamba mlalamikaji hakufutwa kazi kihalali (the termination of Neema Akeyo was substantively unfair).

-Mahakama ya Rufaa ikasema, Tume ya usuluhishi (CMA) na Mahakama Kuu walikuwa halali kuamuru alipwe mshahara wa miezi 36 kama fidia.

-Rufaa ya NMB ikatupiliwa mbali, hivyo NMB wakawa wameshindwa kesi. (The appeal was dismissed)

-Na kwa kuwa Mahakama ya Rufaa ndiyo Mahakama ya juu na yenye Mamlaka ya mwisho nchini Tanzania, ukishindwa hapo basi hamna pa kwenda labda uombe review (marejeo) ambapo Mahakama ya Rufaa itakaa tena kupitia (ku review) uamuzi wake upya.

Wito wangu kwa waajiri, heshimuni uhuru wa kuabudu kwa watu wote. Acheni kuwapangia wafanyakazi majukumu siku za Ibada. Ni heri umpe shift, badala ya Jumamosi afanye hiyo Kazi Jumapili, au umuongezee masaa ya kazi katikati ya week ili siku yake ya Ibada aende kuabudu.

Hata interview zisipangwe siku za ibada. Ukiweka interview siku au masaa ya ibada kuna watu watakosa kazi. Alafu, unakuwa umefaidika nini? Ukipewa nafasi na Mungu usiitumie kunyoosha au kukomesha wenzio.

Na wakuu wa shule, vyuo, waalimu, wahadhiri (lecturers), n.k msiwapangie wanafunzi vipindi na mitihani siku za Ibada.

Yeyote ambaye Mungu amekupa dhamana ya kuongoza watu wake, usitumie nafasi yako kukandamiza uhuru wa dini. Watu wakiomba ruhusa kwenda kuabudu, wape ruhusa. Tunapoomba tunaombea taifa, shule, chuo, ofisi, kampuni n.k. Mtu anakuomba ruhusa akasali unakataa je angekuwa anaenda kuvuta bangi? Kusali ni kitu cha kukataliwa, tena mara moja tu kwa wiki!

Hiyo nafasi yako hapo ofisini ni Neema. Umekalia hicho kiti kwa Neema, Mungu anaweza kuamua ukaondoka. Hivyo usimhuzunishe Mungu kwa kuonea watoto wake. Watendee wote sawa sawa. Awe ni Muislam au Mkristo wape wote uhuru wa kuabudu.

Kesi hii ipo mtandaoni kwa lugha ya kiingereza. Ukitaka kujisomea kwa undani zaidi. Ingia Google (Tanzlii website) andika National Microfinance Bank Ltd (NMB) Vs Neema Akeyo, 2020.

IMEANDALIWA AU KUTAFSIRIWA na kuletwa kwako nami Zakaria (0754575246 - WhatsApp). Lawyer by profession.

Thanks Quote Reply
 
TAHADHARI: Kwa watendaji ambao hawawaambii ukweli mabosi wao kwa kutumwa kufanyisha usaili kwenye siku za ibada. Waathirika wakishitaki, mahakama itabatilisha zoezi zima la usaili hivyo serikali kuingia hasara ya pesa nyingi ilizotumia kuendesha usaili huo. Kitakachofanyika ni kuwa serikali itaamua KUMSAKA MCHAWI aliyesababisha hasara kubwa kwa serikali na hapo ndipo WATENDAJI NA MABOSI wao watageuzwa kuwa MBUZI WA KAFARA!! Watafukuzwa kazi kwa kuisababishia serikali hasara!! Waziri atawaruka KIMANGA! atasema kwani mlipokuwa mnapanga hamkujua kuwa nchi yetu huheshimu uhuru wa ibada kikatiba? Nimewatahadharisha mapema!!
 
Siku ukiambiwa wewe ndio mchawi na umeifedhehesha serikali usishangae! kila siku wanasiasa ni mabingwa wa kutafuta mchawi mambo yakiharibika! Ni tahadhari tu msije kusema haukujua!!
 
Huko NMB mwisho wa siku alitafutwa mchawi na mambo yakamlalia!!
 
Huko NMB mwisho wa siku alitafutwa mchawi na mambo yakamlalia!!
Ila kwa sasa kabla mambo hayajaharibika wanasiasa wanapita hapa kimya kimya tu, lakini siku ya siku wakati sekretarieti ya ajira mmewekwa kikaangoni, watawatazama utafikiri hawawajui!! NI tahadhari tu!!
 
Siyo suala la kuwa mfia dini, bali ni suala la watu kuheshimu ibada ya watu wengine> Hivi haujaona hata hotuba za kitaifa kusitishwa kwa muda kupisha muda wa ADHANA? Wakristo na Wasabato wanaheshimu siku yao ya ibada na serikali ITAMBUE HIVYO na hapo HAKUNA MJADALA.
Mjadala upo! Usaili siku ya Ijumaa ni sahihi? Ukitanguliza Dini mbele katika kila jambo lazima utapata matatizo. Huu mfumo wa kupumzika Jumapili tumerithi toka kwa wakoloni wa Kiigereza kwasababu dini yao ilikuwa ya kikristu. Nchi ya Tanzania ni moja ya nchi chache sana duniani ambayo sherehe za Kikristu na Kiislamu zimepangiwa mapumziko. Nchi nyingi utakuta ni sherehe ya dini moja tu hupewa mapumziko ya kitaifa. Ukiwa mtu usiyependelea upande wowote - lazima ungetegemea swala hili la kuendelea na shughuli za kitaifa Ijumaa na kupumzika Jumapili lazima litaleta changamoto. Je haki ya kuhudhuria ibada siku ya Ijumaa - imekaaje? Je huu si udini uliyojificha kwenye mazoea- tangu Uhuru siku ya Jumapili imekuwa ni siku ya mapumziko na watu hawajajiuliza maswali!
 
Back
Top Bottom