Sekretariet ya ajira katika utumishi wa umma kuendesha usaili siku ya ibada Jumapili

Sekretariet ya ajira katika utumishi wa umma kuendesha usaili siku ya ibada Jumapili

Nioneshe mstari wa Biblia uliosema kufanya kazi siku ya Jumamosi au Jumapili ni haramu! biblia imesema tu "Ikumbukwe siku ya saba na itakaswe" wasabato wanatafsiri kuwa siku hiyo hutakiwi kufanya kazi, wanaosali Jumapili hakuna sehemu inayosema wasifanye kazi...na mwisho kazi ni nini kwa tafsiri ya kisayansi au hata ya dini? halafu tujiulize je usahili unafit kiasi gani kwa "definition" hiyo ya kazi?
Hata kama haikuhusu ila jaribu tena kasome vyema huo mstari imesema vyema hawaruhusiwi kufanya kazi siku hiyo...ni siku ya kupumzika.

Kuna vitu kama huna uelewa navyo ni vyema ukawa kimya tu kuliko kujitia mjuaji kumbe mshamba tu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nina wasiwasi na akili za mtoa mada
Je, wewe unayedai una akili, ni kweli haujui kuwa JUMAMOSI NA JUMAPILI SI SIKU ZA KAZI AU umeamua kujitoa ufahamu? Je haujui kuwa hizo ni siku za ibada na kuna waombaji wa ajira wanatakiwa kuwa kwenye ibada siku hiyo? Wewe ndio una matatizo ya kiakili kama kweli hizi za msingi huna habari nazo!!
 
Ya Mungu mpeni Mungu na ya Kaisari mpeni Kaisari
 
Mkuu, mbona ijumaa ni siku ya kazi na waislam hawajalalamika?
Cha muhimu hapo ni kuomba au kwenda kanisani mapema ili uwahi usaili. Serikali yetu haina dini!
Si haramu kwa mwislamu kufanya kazi siku ya ijumaa na hakuna aya yoyote kwenye msahafu wao unaowazuia kufanya kazi siku ya ijumaa. Ila waislamu huruhusiwa kwenda kwenye ibada masaa ya ibada yakifika siku ya ijumaa.
 
Hawajawahi kubaguliwa! Wametimiziwa matakwa yao kwa kadri walivyoyahitaji. Waislamu hawajawahi kudai kuwa hawapaswi kufanya kazi siku ya Ijumaa wala msahafu wao haujawataka hivyo. ILA muda wa sala ukifika serikali imewapa ruhusa ya kusali. Shule zote humaliza program zao mapema siku ya ijumaa ili kuwapa nafasi wanafunzi na watumishi kuabudu kwa mujibu wa imani yao.
Asante..lakini pia hakuna sehemu Biblia inasema wakristo hawapaswi kufanya kazi siku ya Jumamosi au Jumapili!
 
Ya Mungu mpeni Mungu na ya Kaisari mpeni Kaisari
Kaisari wa Tanzania hajawahi kudai wala kulazimisha watu wafanye kazi jumamosi au jumapili. Ndiyo maana huyu aliyepanga usaili siku ya jumamosi na jumapili AMEKIUKA taratibu maana usaili siyo dharula!!
 
Hata kama haikuhusu ila jaribu tena kasome vyema huo mstari imesema vyema hawaruhusiwi kufanya kazi siku hiyo...ni siku ya kupumzika.

Kuna vitu kama huna uelewa navyo ni vyema ukawa kimya tu kuliko kujitia mjuaji kumbe mshamba tu.

#MaendeleoHayanaChama
Asante mjanja mie mshamba...inawezekana umesema huo mstari wasinye kazi...sasa kazi ni nini? kwa hiyo siku hiyo hao walioambiwa wasifanya kazi ni kweli huwa hawafanyi kazi....hawapiki, hawaendi shamba? hawafanyi usafi majumbani kwao? wao hukaa tu wakipumzika?....wajanja kama wewe mara nyingi hukimbilia kutoa kashfa wanapokuwa hawana hoja...haya basi na msusie huo usahili maana ni haki yenu kupumzika!
 
kwenye Uislamu kuna kitu kinaitwa dharura na dharura inabatilisha wajibu
Kipindi nipo chuo mitihani tunfnya mpk siku ya ijumaa wala hatusemi kitu ila sasa ikatokea dharura flani ivi ya kitaifa itabidi semester iyo mitihani ifanyike mpk j1 na j2.
Chuo ni cha serikali kikatoa tamko asotaka kufnya mtihani aandike barua ya kupostpone tu
Wasabato walikataa katakata kufnya pepa j1 wakaja kufnya mda wa probation m mpk nikawashangaa sasa dini haina dharura wkt ww mwnywe mda mwingine huhudhurii shughuli zako bcz ya dharura

Uislamu unaendana na maisha halisi ya mwanadamu
 
Mkuu, mbona ijumaa ni siku ya kazi na waislam hawajalalamika?
Cha muhimu hapo ni kuomba au kwenda kanisani mapema ili uwahi usaili. Serikali yetu haina dini!
( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ )

الجمعة (9) Al-Jumu'a

Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.

( فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّهِ وَاذْكُرُوا اللَّهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ )

الجمعة (10) Al-Jumu'a

Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.
 
Asante..lakini pia hakuna sehemu Biblia inasema wakristo hawapaswi kufanya kazi siku ya Jumamosi au Jumapili!
Mwanzo 2:3, kutoka 16:29-30, kutoka 20:8-11. "Ikumbuke siku ya saba uitakase, siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo USIFANYE KAZI NYOYOTE, wewe wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa".
Kama lengo lako ni kutaka kuelewa bila shaka umeelewa.
 
Tayari JUMAMOSI na JUMAPILI si SIKU za kazi. Huwezi kuzipangia majukumu ya kiserikali bila kuvunja sheria. Dini yao HAIJAWAHI kudai kuwa ni HARAMU kufanya kazi siku ya IJUMAA isipokuwa ni yale masaa ya ibada tu, na serikali ilishaliheshimu hilo. Hotuba husitishwa kupisha ADHANA, na mashuleni masomo huisha baada ya break time na wanafunzi kuruhusiwa kwenda ibadani.
Kuna usahili wa ijumaa unasimamishwa masaa ya ibada?? Mbona hatulalamiki?? Ww usipoenda wenzako wanaenda,bythen ni usahili,ni kipimo cha uwezo wako wa kujitoa na kufanya kazi sababu maofisini tunafanya kazi sometimes mpaka jumapili,kama umesoma natumai umeona walimu wakitoa test na vipindi hadi siku za weekend za sikukuu,kama hutaweza waachie wengine wenye kuweza kujitoa siku zote
 
kwenye Uislamu kuna kitu kinaitwa dharura na dharura inabatilisha wajibu
Kipindi nipo chuo mitihani tunfnya mpk siku ya ijumaa wala hatusemi kitu ila sasa ikatokea dharura flani ivi ya kitaifa itabidi semester iyo mitihani ifanyike mpk j1 na j2.
Chuo ni cha serikali kikatoa tamko asotaka kufnya mtihani aandike barua ya kupostpone tu
Wasabato walikataa katakata kufnya pepa j1 wakaja kufnya mda wa probation m mpk nikawashangaa sasa dini haina dharura wkt ww mwnywe mda mwingine huhudhurii shughuli zako bcz ya dharura

Uislamu unaendana na maisha halisi ya mwanadamu
Darula huwa haipangwi!! Siku ya usaili siyo dharula na ina nafasi ya kupangiwa tarehe!! Dharula ni kama ajali, au ugonjwa ambao haujui utatokea lini kwa hiyo huwezi kupanga tarehe ya kwenda hospitali kwa ugonjwa unaoweza kukupata ghafla. Hapa hakuna dharula yoyote iliyosababisha usaili upangwe jumamosi na jumapili.
 
Kuna usahili wa ijumaa unasimamishwa masaa ya ibada?? Mbona hatulalamiki?? Ww usipoenda wenzako wanaenda,bythen ni usahili,ni kipimo cha uwezo wako wa kujitoa na kufanya kazi sababu maofisini tunafanya kazi sometimes mpaka jumapili,kama umesoma natumai umeona walimu wakitoa test na vipindi hadi siku za weekend za sikukuu,kama hutaweza waachie wengine wenye kuweza kujitoa siku zote
Wanapaswa wasimamishe usaili masaa ya ibada kama usaili ukifanyika siku ya Ijumaa. Wasipofanya hivyo ni MAKOSA PIA na wanapaswa KULALAMIKIWA.
 
Ulitaka ufanyike weekdays sio na hizo venue hao wanachuo wasisome? Mbona una kaubinafsi ndani yako?
 
Wewe usiende siku ya usaili, sio lazima muende watu wote.
Ni haki ya kila aliyeitwa kwenye usaili kufanya usaili. Huwezi ukafukuza watu kwa kuwawekea mtego wa kufanya usaili siku ya ibada. haikubaliki na PATACHIMBIKA!! Hii nchi inaendeshwa kwa kufuata utawala wa sheria. Sheria imekiukwa kupanga usaili siku ya mapumziko ya shughuli zote za serikali. Usaili siyo dharula!!
 
Huku ni KUPITILIZA na tunasema HAIKUBALIKI KABISA. Haiingii akilini watu na akili zao kuamua kutokuheshimu kwa makusudi imani ya watu ambao wanapaswa kuwa kwenye ibada KANISANI na kuipanga siku hiyo kuwa ni siku ya kuwasaili waombaji wa ajira.

Ina maana wanaoendesha usaili huu kama ni wakristo watakuwa wamedhulumiwa haki na uhuru wao wa kuabudu. Ina maana pia waombaji wa ajira walio wakristo watakuwa wamedhulumiwa haki na uhuru wao wa kuabudu. Hili tunalikataa kwa nguvu zetu zote!!

Tarehe 18/06/2022 siku ya JUMAMOSI (SIKU YA IBADA KWA WASABATO), na tarehe 19/06/2022 siku ya JUMAPILI (SIKU YA IBADA KWA WAKRISTO) zimetangazwa kuwa ni moja ya siku ambazo usaili wa waombaji wa ajira utafanyika. Kwanza jumamosi na jumapili siyo siku za kazi, kwa nini hawa sekretarieti ya ajira wameamua kuzifanya kuwa siku za kazi? Hii JEURI WANAIPATA WAPI? Ushahidi upo kwenye tovuti yao- www.ajira.go.tz na ninatupia kipande hapa:

KADA: ASSISTANT VOCATIONAL TEACHER – ELECTRICAL INSTALLATION MWAJIRI: MAMLAKA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI STADI (VETA) TAREHE YA USAILI WA VITENDO: (1-37) 18 JUNI, 2022 (38-74) 19 JUNI, 2022 MAHALI: VETA DODOMA TAREHE YA USAILI WA MAHOJIANO: 22 JUNI, 2022 MUDA: SAA 1:00 KAMILI ASUBUHI. MAHALI: OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA ZILIZOPO MAJENGO YA DKT. ASHA ROSE MIGIRO, UDOM - DODOMA.

Ninamwomba waziri mwenye dhamana na sekretarieti hii kufanya mambo yafuatayo kwa dharula:
1. Kubatilisha hizo tarehe haraka na kagiza zipangwe tarehe zingine.
2. Kuwawajibisha wote waliofanya ujeuri huu wa kuleta utaratibu unaoashiria UDINI kwenye nchi yetu.
Deen inakuletea pilau??
Kazi ya Serkali ni kuleta Maendeleo na sio kuchonga Misalaba na kutengwa miskiti [emoji12][emoji12]
 
Mwanzo 2:3, kutoka 16:29-30, kutoka 20:8-11. "Ikumbuke siku ya saba uitakase, siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo USIFANYE KAZI NYOYOTE, wewe wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa".
Kama lengo lako ni kutaka kuelewa bila shaka umeelewa.
Nimeelewa hayo maandishi ndugu...lakini nisichoelewa sasa ni ipi hiyo siku ya saba aliyosema itakaswe...ni Jumamosi au Jumapili au zote? na je hayo ya kutofanya kazi yoyote kwa mjakazi, binti, mtumwa wanyama wala mgeni hutumizwa kweli? au hayo tuwaachie wenyewe!
 
Siku ya Jumapili kuna misa nyingi pia kukosa siku moja kwa jambo la muhimu hata alie juu atakubariki maana anaona mpaka moyoni mwako
 
Siyo suala la kuwa mfia dini, bali ni suala la watu kuheshimu ibada ya watu wengine> Hivi haujaona hata hotuba za kitaifa kusitishwa kwa muda kupisha muda wa ADHANA? Wakristo na Wasabato wanaheshimu siku yao ya ibada na serikali ITAMBUE HIVYO na hapo HAKUNA MJADALA.
Kama ibada yangu ni kuchinja na kula nyama za watu Serkali Iheshimu Ibada yangu! Sivyo?!
 
Back
Top Bottom