Sekretariet ya ajira katika utumishi wa umma kuendesha usaili siku ya ibada Jumapili

Ulitaka ufanyike weekdays sio na hizo venue hao wanachuo wasisome? Mbona una kaubinafsi ndani yako?
Kwa bahati mbaya unaandika bila ufahamu wa ndani. Usaili unafanyika tarehe weekdays pia. Kwa hiyo sababu yako haiingii hapa.
 
Hivi ukienda kusali kisha ukaenda kwenye usahili...kuna kitu kitaharibika?
 
Safi sana. Kumbe mara baada ya sala wanatakiwa wachachalike kufanya kazi kutafuta fadhila!! Na serikali haijawahi kuwaingilia katika muda wao wa ibada!!
 
Wapi kwenye biblia panasema kuwa kuabudu Jumapili lazima uende kanisani.
Wewe amka siku ya Jumapili, tenga nusu saa yako au saa nzima sali na abudu in private hapo nyumbani kwako kisha kapige usaili.

Au wakati unasubiri usaili nenda jitenge na watu pembeni kule kaabudu kisha rudi kafanye usaili.
 
Dini ni ugonjwa mbaya sana wa akili kuwahi kuikumba dunia.

Anyway wamekusikia naamini wata reschedule ili wafia dini mfanye kwa uhuru.

#MaendeleoHayanaChama
Zaidi ya kansa,Yaani huyo jamaa,Usikute hata Usaili haumhusu!!
 
Hivi ukienda kusali kisha ukaenda kwenye usahili...kuna kitu kitaharibika?
Kutoka 20:8-11. "Ikumbuke siku ya saba uitakase, siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote, lakini siku ya saba ni sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo USIFANYE KAZI NYOYOTE, wewe wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa".
Kama lengo lako ni kutaka kuelewa bila shaka umeelewa.
 
Asante sasa nimeelewa kuhusu kumpumzika kwamba ni takwa la maandiko matakatifu na ni haki yenu kabisa hapo sina ubishi....kama ulivyonifafanulia hili naomba pia unifafanulie kwa kati ya Jumamosi na Jumapili ni siku ipi imelengwa na andiko hili?
 
Hii sio inchi ya kidini afu usipangie serikali kitu cha kufanya hutaki kufanya usaili usiendee sio lazima kuna watu mna vitu vya ajabu
 
Hatokujibu huyo Wa mchongo tuu!
Si haramu kwa mwislamu kufanya kazi siku ya ijumaa na hakuna aya yoyote kwenye msahafu wao unaowazuia kufanya kazi siku ya ijumaa. Ila waislamu huruhusiwa kwenda kwenye ibada masaa ya ibada yakifika siku ya ijumaa.
 
Hatuongei kibinafsi, bali tunaongea kisera! Unataka kuniambia wakristo WOTE hawahusiki na usaili huo?
Serikali ilisema Haina Dini kwa Ajili ya watu km Ninyi,Kila kitu Dini...Kwa hiyo waislamu nao wasiende kazini Ijumaa au hawana haki.
 
Hiyo ni mojawapo ya usaili.Kama vipi usiende.
 
Kuwakomoa tusiende
Lazima wabatilishe hiyo siku, vinginevyo matokeo ya usaili yatabatilishwa mahakamani maana yamefanyika kwa kuwabagua baadhi ya watu!! Hakuna namna LAZIMA wabatilishe na LAZIMA waliopanga hivyo WAWAJIBISHWE>
 
We mzee hivi kweli hili jambo nilakumsumbua waziri aache kufanya jambo la msingi ashughurike na hizi tarehe kwanii yaani??

Mungu yupo kila siku bhana nenda kwenye usaili au hata kabla ya huo usaili wako fanya ibada muombe mungu utakavyo nenda kwenye usaili sio lazima saana kuwepo na mtukati kati yako na mungu kwa ajili yakukuombea.


Achana na hizi lalamalama ambazo hazina maana,

Si tunapambania hizi saili zifanyike kwa zonal,, maana huko dodoma yaani nikama vile ishakuwa mbinu yakwanza kushortlist watu daaaaa!

Hivi hawaoni hili au makusudi yao tu jamanii nina shortlisted nyingi kwenye portal Ila naziangalia tu yaani.
 
Si haramu kwa mwislamu kufanya kazi siku ya ijumaa na hakuna aya yoyote kwenye msahafu wao unaowazuia kufanya kazi siku ya ijumaa. Ila waislamu huruhusiwa kwenda kwenye ibada masaa ya ibada yakifika siku ya ijumaa.
Kwani Mungu na Usaili kipi bora!! Wewe km Una imani kweli,Achana na Usaili nenda kanisani.
 
Serikali ilisema Haina Dini kwa Ajili ya watu km Ninyi,Kila kitu Dini...Kwa hiyo waislamu nao wasiende kazini Ijumaa au hawana haki.
Si haramu kwa mwislamu kufanya kazi siku ya ijumaa na hakuna aya yoyote kwenye msahafu wao unaowazuia kufanya kazi siku ya ijumaa. Ila waislamu huruhusiwa kwenda kwenye ibada masaa ya ibada yakifika siku ya ijumaa.
 
Hili jambo limepangwa hivyo kimkakati ili kubagua baadhi ya watanzania. Kama unafikiri kuwa jambo hili ni dogo subiri na ulifuatilie jinsi litakavyoishia jambo hili!! Suala hili litaenda hadi mahakama ya juu kabisa kama akithubutu mtu kulishughulikia kivyepesi vyepesi!!
 
Lazima wabatilishe hiyo siku, vinginevyo matokeo ya usaili yatabalishwa mahakamani maana yamefanyika kwa kuwabagua baadhi ya watu!! Hakuna namna LAZIMA wabatilishe na LAZIMA waliopanga hivyo WAWAJIBISHWE>
Hahahaha ndo maana sipendagi kwenda kwenye makanisa ya ovyo ovyo yanaondoa ubongo wako kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…