Sekretariet ya ajira katika utumishi wa umma kuendesha usaili siku ya ibada Jumapili

Dah tutaonaga mengi mwaka huu.
 
Kwani Mungu na Usaili kipi bora!! Wewe km Una imani kweli,Achana na Usaili nenda kanisani.
Huo ni ubaguzi na uonevu ambao tunaupinga kwa nguvu zote na HAUTAFANIKIWA. Fuatilia uone jambo hili litakavyokwisha na si jambo rahisi kama unavyotaka kulichukulia.
 
Zaidi ya kansa,Yaani huyo jamaa,Usikute hata Usaili haumhusu!!
Ni kweli mimi huu usaili haunihusu mimi binafsi lakini unanihusu kama mtanzania. Ninapigania haki ya kuheshimiwa kwa dini zote! Ibada lazima iheshimiwe. Siku ya SABATO ni siku ya Bwana na ni siku ya mapumziko kwa mujibu wa dini ya Kikristo hususan Wasabato!!
 
Kwani Mungu na Usaili kipi bora!! Wewe km Una imani kweli,Achana na Usaili nenda kanisani.
Vyote ni muhimu na vyote vina haki ya kufanyika! Lazima mamlaka zinazohusika zipange kwa namna ambavyo raia wake watalindiwa haki zao zote. Tunadai uwajibikaji kwa mtumishi yeyote aliyepanga katika namna ambayo watanzania wengine watakosa haki zao za msingi.
 
kwa hiyo waislamu hawaheshimu siku yao ya ibada
 
Asante sasa nimeelewa kuhusu kumpumzika kwamba ni takwa la maandiko matakatifu na ni haki yenu kabisa hapo sina ubishi....kama ulivyonifafanulia hili naomba pia unifafanulie kwa kati ya Jumamosi na Jumapili ni siku ipi imelengwa na andiko hili?
Hilo swali si sehemu ya mjadala uliopo. Ndiyo maana mimi sijazibagua nimeziweka zote mbili. Lakini pia kutokufanya kazi siku ya jumamosi na jumapili si suala la kidini tu lakini ni la kisera pia. Taratibu za kazi hapa Tanzania zimetenga siku hizo mbili kuwa siku za mapumziko (isipokuwa watumishi wenye nafasi ya kushughulikia dharula kama askari, madaktari nk). Kukiuka hilo ni kukiuka utawala wa sheria kitu ambacho hakikubaliki.
 
kwa hiyo waislamu hawaheshimu siku yao ya ibada
Si haramu kwa mwislamu kufanya kazi siku ya ijumaa na hakuna aya yoyote kwenye msahafu wao unaowazuia kufanya kazi siku ya ijumaa. Ila waislamu huruhusiwa kwenda kwenye ibada masaa ya ibada yakifika siku ya ijumaa.
 
Hii sio inchi ya kidini afu usipangie serikali kitu cha kufanya hutaki kufanya usaili usiendee sio lazima kuna watu mna vitu vya ajabu
Hii siyo nchi ya kidini ni kweli lakini ni nchi inayofuata utawala wa sheria. Kwa mujibu wa sheria za kazi hapa nchini kwetu JUMAMOSI NA JUMAPILI NI SIKU ZA MAPUMZIKO isipokuwa kwa wale wanaoshughulika na kazi za kushughulikia dharula kama askari, madaktari nk. Usaili siyo dharula. WATAELEWA TU.
 
We embu tulia mbona kuna dini nyingine siku ya ibada wanatinga job na wapo kimya?
 
Kwa kweli
 
Usighadhabike hawajasema Ijumaa.
 
Kumbe hata nyie mnalialia eeh? Mkitoka hapo mnasema RC ndio ina run hii kantri
 
We embu tulia mbona kuna dini nyingine siku ya ibada wanatinga job na wapo kimya?
Ni kweli kwa kuwa "dini" yao haina kizuizi hicho. Lakini siku ya SABATO ni siku ya BWANA na ya mapumziko. Ndio maana wana wa Israel hawakuruhusiwa kwenda kukusanya mana siku ya SABATO. Siku ya sita walitakiwa kukusanya kiasi cha mana mara mbili ili kesho yake siku ya saba (SABATO) wasiende kukusanya mana.
 
Kama ibada yangu ni kuchinja na kula nyama za watu Serkali Iheshimu Ibada yangu! Sivyo?!
Tuna uhuru wa kuabudu kwa mujibu wa sheria na si kinyume na sheria. Kwanza dini yako ni lazima isajiliwe serikalini. Na ili usajiliwe ni lazima katiba ya dini yako ikubalike. Kwenye katiba ni lazima uainishe hicho unachoamini na misingi ya dini yako. Kama wewe unakula nyama za watu ni kwamba serikali haitakubali kuisajili dini yako na hautaruhusiwa kuabudu.
 
Na-log off, hoja yangu imeeleweka na tusubiri matokeo!!
 
Kwa hiyo unataka usaili ufanyike Jumatatu hadi Alhamisi tu??
 
Sasa msabato wetu,wakifanya weekdays hizo sehemu za kufanyia usahili watazitoa Wapi? Maana mara nyingi wanafanya weekends kwa sababu ya venue kama wangekuwa na venue zao wangefanya weekdays
 
Halafu hapo juu umeandika siku ya ibada ya wasabato na wakristo,hivi wasabato sio wa kristo?
 
Mtoa mada Yuko sahihi kabisaa, Kwa mujibu was taratibu za dini yake, na Kwa mujibu wa Sheria za kazi kwa mujibu wa katiba jumamos na jumapili ni mapumziko, hata hao wasimizi wa hizo interview wamekubali kwasababu watapata hela ingekuwa kinyume na hapo wasimgekubali na wangekuwa na hoja.Tarehe lazima zibadilishwe kuondokana na huu mgongano, tayarii tuna mfano wa yule mfanyakazi wa NMB aliyefukuzwa kazi kwa sababu aligoma kufanya kazi siku ya jumamosi, mahakama ilichoamua na akalipwa sawa sawa na madai yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…