Sekretarieti ya Bunge: Kuna mapungufu katika Mkataba wa Bandari na DP World; ukomo wake uwekwe wazi

Yale yale ninayokueleza, lakini hata moja haliingii akilini mwako.

Kinachozungumziwa hapa ni "Mkataba/contract", halafu wewe unakwenda na 'common sense?

Hayo yaliyo na "kichwa na miguu" toka kwako ni yapi sasa hapa?
 
Hii sekretarieti ya bunge nahisi ilikuwa likizo wakati ule, ama namna gani!
Hapo wanatafuta njia ya kutoka Kwa kusema CCM ndio wamerekebisha na wakati huo huo wanatumia hatua za ngamia niweke kichwa Tu mwishowe anakutoa kabisa
 
Hiyo unayoongea ww ni hoja mpya,hivyo kuukubali ukweli kwamba IGA ina mapungufu yanayopingana na katiba pamija na sheria za nchi,na lengo la hzo sheria ni kuepuka kuja kulipa billioni za pesa kwa kujitetea kwa lugha tusio kuwa na uzoefu nayo
 
Hili nalielewa na mtu anayetaka usuluhishi ufanyike mahakama za ndani anaonesha hajui mikataba ya kinataifa inaendaje.

Bandari ishakuwa na migogoro iliyokwenda kusuluhushwa London Court of International Arbitration, na Tanzania ikishinda, kati ya kesi chache ambazo Tanzania ilishinda. Miaka ya nyuma sana nafikiri ni 1990s.

Kuna wakati nilikuwa nasoma The Economist, wakatoa takwimu za usuluhishi za London Court of International Arbitration, walisema katuka kila kesi 10, 9 wawekezaji wanashinda, 1 tu ndiyo serikali zinashinda. Na hapo kuna watu wana mikataba mizuri kuliko huu.

Ila, mkataba huu (IGA) una matatizo mengi sana hata ukiondoa hilo la arbitration, tukifika kwenye arbitratiin kwa mkataba huu, ni vigumu sana kushinda.
 
Hiyo unayoongea ww ni hoja mpya,hivyo kuukataa ukweli kwama IGA ina mapungufu yanayopingana na katiba pamija na sheria za nchi,na lengo la hzo sheria ni kuepuka kuja kulipa billioni za pesa kwa kujitetea kwa lugha tusio kuwa na uzoefu nayo
Sijakataa hiyo sheria ipo; ila hakuna mwekezaji ataingia mkataba kupitia hiyo sheria kwa sababu the risk za kunyimwa haki yake huko mbeleni are too high.

Hayo mambo washajifunza huko nyuma na kufanya kosa sio kosa; kurudia kosa ndio kosa.

Waulize Enron waliingia mkataba na British Gas uingereza wakajisahau kuweka neutral area kwenye dispute resolution; mgogoro ulipotokea kesi ikaenda mahakama ya uingereza kilichowakuta walibaki kulalamika kwa miaka mingi sana.

Wenyewe kwa wenyewe awaaminiani ndio waje kuingia mikataba third world isiyo na neutral area ya kutatua migogoro hilo swala halipo dunia kote; that’s not how things work.

Naona ata wao wamestuka huko serikalini ndio maana wanafanya amendment kwenye hiyo sheria; it was ill advised.
 
Hoja sio kushitakiwa nje hoja iliopo ni IGA,ina poor terms na mojawapo ni kuwa na athari kwenye katiba na sheria za nchi,nayo ni mojawapo ya mapungufu kwenye mkataba
 
Kushinda au kushindwa kwa kesi kwenye arbitration or any other court; pertaining commercial dispute matters inategemea na breach husika and whose right or wrong from the contract perspective.

Kinachoangaliwa huko ni mkataba wenyewe na terms zake; kwenye kuamua.

Quality of lawyers might also influence outcome even when the defendant loses; how so? By limiting the amount of liability/damages they might have to pay.
 
Kwa hyo mbeya kesi tunashinda kwa kuvunjwa kwa sheria za nchi na katiba ya nchi,hivyo hoja IGA kuwa na poor terms zinazoathiri katiba ya nchi
 
Kwa hyo mbeya kesi tunashinda kwa kuvunjwa kwa sheria za nchi na katiba ya nchi,hivyo hoja kuwa na poor terms zinazoathiri katiba ya nchi
Hiyo treaty na yenyewe ni sheria kama hiyo ilivyo hiyo sheria ya mwaka 2017.

I don’t see how mahakama inaweza futa hiyo treaty labda kama awapendi maendeleo. Ukizingatia serikali imeshapeleka muswada wa mabadiliko kufanya amendement ya hiko kipengele tata kwenye sheria husika.
 
Unatunga vp sheria inayopingana na sheria iliyopo,kwenye muongozo kabla ya IGA kuwa ratified illitakiwa kuangalia k.m mkataba unaathari kwenye katiba na sheria za nchi,na hicho ni kipengele tu kwenye muongozo kuhisiana na kuwa ratified kwa IGA vinavyopelekea mktaba kuwa na "poor terms" (k.m usemavyo ww zingeonyeshwa na kina kivy" , hivyo kupelekea kujiuliza je wadau k.m TLS walipelekewa IGA watoe hoja zao k.m muongozo ulivyo
 
ASKOFU MWAMAKULA AMESEMA WANA TAARIFA ZOTE ZA KILICHOFANYIKA KUHUSU MKATABA HUO (RUSHWA) KWANI TAARIFA HIZO WANAPEWA NA WASHIRIKA WAO WALIO KWENYE SYSTEM SERIKALINI.
HUYU MAMA ANATAKIWA KUANGALIWA KWA JICHO LA TATU. SIYO MTU MZURI. TUNAVYOMCHUKULIA SIVYO ALIVYO. OGOPA SANA MWANAMKE.
 
Tuendelee kupigania raslimali zetu wazalendo, tuachane na haya mafisadi ya ccm!
Baada ya vidume wazalendo kuja juu leo ndio wanasema una mapungufu? Shame!
ccm sio watu wa kuwachekea kabisa kwani watatuuza hadi sie
 
Sheria sio katiba

Uwezi tunga sheria iliyo tofauti na katiba

Unapotunga sheria tofauti inayokindhana na nyingine iliyopo; inabidi ufanyie moja amendments.

That’s a no brainer ndio maana serikali imepeleka muswada wa kubadili hiyo sheria. Hiko kipengele sio rafiki kwa uwekezaji kama lengo ni kuvutia FDI.
 
Najaribu kufikiria namna ya kuvunja makubaliano (mkataba) ambao tayari umesha sainiwa na pande zote mbili.
Je, itakuwa ni kirahisi rahisi tu?​
Kitu kikishakuwa FAKE na BATILI, lazima uwepo uwezekano wa kuondokana nacho.
 
Hoja sio kushitakiwa nje hoja iliopo ni IGA,ina poor terms na mojawapo ni kuwa na athari kwenye katiba na sheria za nchi,nayo ni mojawapo ya mapungufu kwenye mkataba
Sasa mbona unaninukuu na kurudia nilichoandika? Sisi tunakubaliana.

Hiyo habari ya arbitration kufanyika nje tuiache, hiyo si point.

Kwa sababu, ukiwa na mkataba mzuri, hata arbitration ukifanya nje, kama umeonewa, utashinda tu.

Nimetoa mfano wa kesi moja ya Tanzania Harbours Authority (kabla haijawa Tanzania Ports Authority), walishinda arbitration London.

So, sehemu itakayofanyika arbitration siyo issue, issue ni hivyo vipengele vingine.

The devil is in the detail, na hapo ndipo tuna matatizo kwa sababu hatuna mazungumzo yenye nuance.

Kwa mfano, kuna sehemu nimesikia wanasheria wanasema sheria zitakazotumika ni za Uingereza, na zinaondoa incumbency ya sheria za Tanzania kwenye umiliki ardhi, wakati Tanzania tunajua rais ndiye muhifadhi wa mwisho wa ardhi.Hili lina maana gani? Hili lina maana kuwa mkataba unaondoa nguvu za rais kuwa mtu wa mwisho mwenye amri katika mambo ya ardhi, na akitumia nguvu zake hizi za kikatiba Tanzania, anaweza ku trigger arbitration na Tanzania ikatakiwa kulipa mamia ya mamilioni ya US dollar.

So, unaweza kufanya mkataba mzuri, ambao utakuwa na arbitration London, lakini ukawa na vipengele vya kuheshimu sheria za Tanzania.
 
Kwa hiyo hawa akina chongolo wanatumia kodi zetu kuaminisha watu bogus treat!!
 
Na mimi ndiyo nasema hivi, kupinga mkataba kwa sababu una clause ya arbitration kufanyika nje ni kutoelewa mikataba hii ya kimataifa, kwa sababu that is a standard clause kwenye mikataba mikubwa hii.

Na pia, arbitration kufanyika nje haimaanishi kwamba hicho ni kitu kibaya na tutashindwa arbitration, kwa sababu tushafanya arbitration nje tukashinda.

Kitu muhimu ni kuwa na mkataba mzuri, hizi habari za arbitration itafanyika wapi ni distraction.

Na katika hilo la mkataba kuwa mzuri, tuna point nyingine nyingi tu za kuu criticize mkataba, hatuihitaji hii point ya kukataa arbitration kufanyika nje.

Kama tunaweza kuzungumzia nuance, kwa mfano kuondolewa incumbency ya Tanzanian land laws na last custodian role ya rais kwenye land Tanzania, hapo labda tunaweza kuwa na point.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…