Hoja sio kushitakiwa nje hoja iliopo ni IGA,ina poor terms na mojawapo ni kuwa na athari kwenye katiba na sheria za nchi,nayo ni mojawapo ya mapungufu kwenye mkataba
Sasa mbona unaninukuu na kurudia nilichoandika? Sisi tunakubaliana.
Hiyo habari ya arbitration kufanyika nje tuiache, hiyo si point.
Kwa sababu, ukiwa na mkataba mzuri, hata arbitration ukifanya nje, kama umeonewa, utashinda tu.
Nimetoa mfano wa kesi moja ya Tanzania Harbours Authority (kabla haijawa Tanzania Ports Authority), walishinda arbitration London.
So, sehemu itakayofanyika arbitration siyo issue, issue ni hivyo vipengele vingine.
The devil is in the detail, na hapo ndipo tuna matatizo kwa sababu hatuna mazungumzo yenye nuance.
Kwa mfano, kuna sehemu nimesikia wanasheria wanasema sheria zitakazotumika ni za Uingereza, na zinaondoa incumbency ya sheria za Tanzania kwenye umiliki ardhi, wakati Tanzania tunajua rais ndiye muhifadhi wa mwisho wa ardhi.Hili lina maana gani? Hili lina maana kuwa mkataba unaondoa nguvu za rais kuwa mtu wa mwisho mwenye amri katika mambo ya ardhi, na akitumia nguvu zake hizi za kikatiba Tanzania, anaweza ku trigger arbitration na Tanzania ikatakiwa kulipa mamia ya mamilioni ya US dollar.
So, unaweza kufanya mkataba mzuri, ambao utakuwa na arbitration London, lakini ukawa na vipengele vya kuheshimu sheria za Tanzania.